WHO yatoa wito wa kuongeza Ushuru kwenye Vilevi ili kupunguza Vifo vya Watumiaji

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa wito wa kuongezwa ushuru kwa bidhaa za pombe na vinywaji vyenye sukari ili kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya watu wanaokufa kutokana na unywaji pombe na ulaji usiofaa.

Baada ya kufanya tafiti za viwango vya ushuru, WHO imesema kuwa kiwango cha wastani cha ushuru kimataifa kwa "bidhaa zisizo bora kiafya" kilikuwa cha chini mno, huku ikisisitiza kuwa bidhaa kama vile mvinyo hazitozwi kabisa ushuru katika baadhi ya nchi za Ulaya.

Kulingana na WHO, watu milioni 2.6 hufariki kila mwaka kutokana na kunywa pombe huku watu milioni 8 wakifariki pia kwa mwaka kutokana na ulaji usiofaa.

Shirika hilo limesema kuongeza ushuru kutasaidia kupunguza matumizi ya bidhaa hizo na kutoa motisha kwa makampuni kutengeneza bidhaa zenye ubora kwa afya ya binaadamu.


DW
 
_20231206_132659.JPG
 
Kwani tukifa wao WHO wanapungukiwa nn? Hatuishi milele, watuache tufurahie maisha, life is short!
 
Back
Top Bottom