Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,500
- 9,279
Tarehe 16 Oktoba ni Siku ya Chakula Duniani na pia ni maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO). Maadhimisho haya yanafanyika wakati dunia ikikabiliwa na janga la virusi vya Corona, ambavyo vimevuruga kwa kiasi kikubwa mnyororo wa uzalishaji wa chakula.
Siku ya Chakula Duniani inapaswa kuchukuliwa kama fursa ya kuleta ushirikiano na mshikamano wa kimataifa ili kuhakikisha tishio linalotokana na virusi vya Corona katika usalama wa chakula na kilimo linakabiliwa ipasavyo, na watu walio hatarini zaidi wanaweza kujiendeleza tena baada ya janga hilo kumalizika.
Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Chakula yenye kaulimbiu “Kesho Njema Inajengwa na Lishe Bora Endelevu”, karibu watu milioni 690 duniani wanakabiliwa na njaa, ikiwa ni ongezeko la watu milioni 10 zaidi tangu mwaka 2019. Janga la virusi vya Corona linaweza kuongeza tatizo hilo zaidi, kwani shughuli za kijamii na kibiashara katika nchi nyingi zimefungwa ili kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo.
Takwimu zinaonesha kuwa kila mwaka chakula kilichoharibiwa kote duniani kinaweza kuwalisha watu bilioni 2, na kila baada ya sekunde 5 mtoto mmoja anafariki kutokana na njaa ama ukosefu wa virutubisho.
Ili kujenga mfumo wa nafaka wenye afya na uendelevu, wanatakiwa kushirikiana na serikali, kampuni za chakula, idara za umma, taasisi na wateja kufanya juhudi kutimiza lengo la kutokomeza njaa na ukosefu wa virutubisho duiniani hadi kufikia mwaka 2030.
Siku ya chakula duniani: kila baada ya sekunde 5 mtoto mmoja anafariki kutokana na njaa