Siku ya 4 inapita waliotaka kumuua Lissu hawajapatikana!

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,160
Wajibu mkubwa wa Jeshi la Polisi nchini ni kuwalinda Raia na mali zao.

Ingawa Jeshi la Polisi huwa linajidai kuwa na intelejensia ya hali ya juu kiasi ambacho kila mkutano wa kisiasa wa chama cha upinzani ukitaka kufanyika huwa wamepata taarifa za kiintelejesia kuwa mkutano huo utavamiwa na watu wasioutakia mema mkutano huo na hivyo kuufuta mkutano huo!

Lakini katika tukio hili la kuvamiwa kwa Tundu Lissu katika mji mdogo wa Dodoma, tena mchana kweupe Jeshi la Polisi limeshindwa kazi yao na hivyo viongozi wa juu wote wa Jeshi letu la Polisi wanapaswa kufutwa kazi!

Kwa kuwa kwa mtu kama Tundu Lissu, licha ya kuwa ni mbunge wa kuchaguliwa na wananchi wake wa Singida Mashariki kuwa ni mbunge wake, yeye pia ni mwanasheria mkuu wa Chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema, yeye pia ndiye Rais wa wanasheria wote wa Tanganyika.

Sasa ikiwa mtu kama Tundu Lissu anamiminiwa risasi 28 kwenye bunduki ya kivita na watu wasiojulikana, sembuse mimi na wewe?

Kama wajibu mkubwa wa Jeshi la Polisi ni kulinda Raia na Mali zao na Jeshi letu la Polisi limeshindwa kulinda uhai wa uhai wa Tundu Lissu na kuuweka mashakani, sembuse uhai wangu Mimi mlala hoi?

Tunatarajia Rais wetu alivyo mwepesi wa kuwatumbua viongozi wake pale wanapokosa kutimiza wajibu wao, tunatarajia kwa hili pia atafanya hivyo "faster" kwa kumuondoa kwenye nafasi yake IGP na Waziri wa Mambo ya ndani kwa kuwa wameshindwa kutuhakikishia usalama wetu na mali zetu!
 
Tuanzie kwenye geti linalolindwa na askari pale kwenye Nyumba za viongozi Dodoma. Makazi ya Lissu ni Jirani na Naibu speaker na geti ni moja.

Hao askari ilikuwaje wakawafungulia hao watu? Na kwanini baada ya vita!!! risasi 28 hiyo ni vita. Ilikuwaje wakawafungulia tena ili waondoke?
 
Tumeshuhudia nchi yetu katika kipindi kilichopita watu wasiojulikana wakimteka msanii Roma Mkatoliki kwa siku zaidi ya 4 na hadi hivi sasa hawajapatikana!

Tumeshuhudia watu wasiojulikana wakimteka Ben Saanane na hadi sasa hajulikani alipo!

Tumeshuhudia pia mtu asiyejulikana akimtolea bastola Nape Nnauye mchana kweupe mbele ya camera za vyombo vya habari na hadi sasa hajapatikana!

Tumeshuhudia pia watu hao wasiojulikana wakiingia kwenye studio za Clouds na kuwatishia watangazaji wa Studio hizo kuwa wataweza kubambikia kesi ya madawa ya kulevya na hadi Leo watu hao wamekuwa UNTOUCHOUBLES!
 
Tuanzie kwenye geti linalolindwa na askari pale kwenye Nyumba za viongozi Dodoma. Makazi ya Lissu ni Jirani na Naibu speaker na geti ni moja.

Hao askari ilikuwaje wakawafungulia hao watu? Na kwanini baada ya vita!!! risasi 28 hiyo ni vita. Ilikuwaje wakawafungulia tena ili waondoke?
Hapo ni mahali pazuri sana pa kuanzia.......

Inakuwaje mahali penye Ulinzi wa aina ile watu wasiojulikana wafyatue risasi 28 na kuondoka pasipo kukamatwa?????
 
Wanasakwa kwa udi na uvumba tuna imani na vyombo vyetu vya usalama ila na sisi raia tutoe ushirikiano sio tubaki kulalama tu,kuna baadhi ya viongozi hasa wa upinzani wamesha anza kunyooshea vidole watanzania wasiokuwa na hatia hatia yao labda ni kuwa wanachama wa chama cha mapinduzi.
 
Mashinji tayari kaitwa polisi ataje hao anaowajua, manaake jamaa ana kimbelembele sana.
 
Hapo sasa ndiyo tunashindwa kujua huo utaalamu wao wa kiintelejensia huwa unaishia kwenye mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani pekee?

Mbona kwenye mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani huwa hatusikii hiyo miito ya kututaka raia wema tutoe ushirikiano kwao Jeshi la Polisi, huwa tunasikia tu kuwa kutokana na taarifa zao za kiintelejensia wamebaini kuwa watu waovu wamepanga mbinu za kichafua mikutano hiyo?
 
Mashinji tayari kaitwa polisi ataje hao anaowajua, manaake jamaa ana kimbelembele sana.

Wale FFU pale getini kwa waheshimiwa wameshawekwa lockup??au walikuwa wamevaa head phone hawakusikia zile risasi zikitoka.Naona walivaa miwani ya mbao maana hata gari hawakuliona wakati linatoka.

Mngedanganya wakati wa JKN kwa sasa siyo rahisi. Bashite Dodoma alienda kufanya nini??

Hivi siku almasi day ilifanyika Dar Dodoma alienda kwenye Harusi??

Na muda mfupi baadaye alikuwa Morogoro alifikaje Morogoro??
Wanaccm muangaleni sana Bashite kuna siku mtakuja kujuta maana kwa sasa ananguvu kuliko hata Makamu wa Rais.

Yachekeeni matendo yake ila kuna siku mtalia na kuomboleza
 
Sasa unaandika insha ya nini wakati Mashinji keshasema anawajua wauaji. Au hukumsikia?
 
Mbona kwenye mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani huwa hatusikii hiyo miito ya kututaka raia wema tutoe ushirikiano kwao Jeshi la Polisi,
Viongozi wa vyama vya upinzani wengi wao si wanasiasa ni wanaharakati na hotuba zao nyingi ni za kuwachonganisha wananchi wema na serikali yao matokeo yake wananchj wema wanashawishiwa kuchukia vyombo vyetu vya usalama
 
Wale FFU pale getini kwa waheshimiwa wameshawekwa lockup??au walikuwa wamevaa head phone hawakusikia zile risasi zikitoka.Naona walivaa miwani ya mbao maana hata gari hawakuliona wakati linatoka.

Mngedanganya wakati wa JKN kwa sasa siyo rahisi. Bashite Dodoma alienda kufanya nini??

Hivi siku almasi day ilifanyika Dar Dodoma alienda kwenye Harusi??

Na muda mfupi baadaye alikuwa Morogoro alifikaje Morogoro??
Wanaccm muangaleni sana Bashite kuna siku mtakuja kujuta maana kwa sasa ananguvu kuliko hata Makamu wa Rais.

Yachekeeni matendo yake ila kuna siku mtalia na kuomboleza
Bora umempasha ukweli huyo gamba.....

Unajua kunusurika kwa Tundu Lissu kunawauma sana hao vijana wa Lumumba!

They wish they could be "satanic" Israel!
 
Back
Top Bottom