Siku Vijana Watakapowageuka CHADEMA.

leroy

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
1,589
2,140
Nimekuwa mtu ninayepinga ukuaji wa umaarufu na kukubalka kwa chadema kutokana na udhaifu wa chama tawala.

Nimekuwa nikijaribu kuishawishi chadema kuwashawishi vijana hata kama chama tawala kitatekeleza matakwa na matarajio ya watanzania kupitia uenezi wa sera na mwelekeo.

Ninawaza siku Vijana wa kitanzania watakapowageuka chadema na viongozi wake.
 
ITAKUWA KAMA VIJANA WALIVYOMGEUKA KIKWETE NA CHAMA CHAKE MKUU USIJALI HILO! Ly
 
Ni mawazo yako, ila Vijana wanajua jema na baya.

Hapo kwenye nyekundu WENGI NI WAFUATA MKUMBO, wakighafilika kutokana na madhila yaliyoletwa na ccm pasi kujua hata mwelekeo na katba ya chadema
 
Kweli Saa nyingine watu wanaandika ***** kwenye Jukwaa la Siasa; Kwanza haujafanya Uchunguzi, haujawapigisha kura

Kwanini unaongelea hayo? Inasikitisha sana, yaani hauna cha kuongelea Mpaka Unaandika yasiyofaa?

This forum one day will fail not because of network it is because of us writing bogus news
 
1. Ulitaka niongelee yapi? Au unanifundisha cha kuongea?
2. Inasikitisha au inahamasisha jitihada zaidi?
3. Hayafai kwa nini?
4. Define why this you think (may be b'se of your dwarf mind) is a bogus news.
 
Mkuu leroy kuna hoja ya msingi hapa.

Vijana huwa wana mategemeo makubwa. Kumbukumbu zinaonyesha kwamba vijana walikuwa wakishangilia sana wakati Rais JK anaingia madarakani. Walimpigia kura wakidhani sasa ni wakati wa vijana kutesa, waliona vijiwe sasa kwaheri wanaenda kupata wote kazi njema zinazolipa huko maofisini.

JK alianza kwa kutembelea wizara na kuna muda alikuwa anatembea toka wizara moja kwenda nyingine akiwa analakiwa kwa nderemo na vifijo vya vijana waliokuwa wakijipanga kumuona mkombozi wao. Baada ya kuona matokeo si sawa na matarajio yao basi wamejikita CDM wakitegemea hali bora toka huko.

Hakika CDM ina vijana kila kona na wote wanaitimbulia macho CDM iingie ikulu iwaokoe na hali duni. Hivyo CDM kama hawatafikia matarajio ya vijana basi vijana hao hao ndio watawageuka tena na kutafuta mbadala. CDM inabidi ijipange kutekeleza matarajio ya vijana
 
1. Wakati mwingine mategemeo haya hujengwa na peer pressure.
2. Who can assure us of this, labda kama tumeamua kuwa Wajinga wa kuamini kila kitu.
 
Huna hoja. Hayo ni mawazo ya kigambagamba.Vijana waigeuke CHDM ili waende wapi?. CCM? Ndoto za mchana.
 
Siku Vijana watakapo wageuka CDM, CDM itakuwa IKULU na CCM kitakuwa chama kikuu cha UPINZANI na hiyo ndiyo demokrasia.
 
Back
Top Bottom