Siku Tanzania "ilipotoa" msaada

Siku Tanzania "ilipotoa" msaada

Sijali

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2010
Posts
2,700
Reaction score
1,853
Wengi wetu tuna hii dhana kuwa Tanzania ni nchi ya kupokea misaada tu. La hasha! Kulikuwa na wakati Tanzania ilikuwa ikitoa misaada, tena ya kifedha!
Mwaka 1975 ulikuja ujumbe wa Vietnam ukakutana na rais wa wakati huo Julius Nyerere. Ujumbe huo ulikuwa unatembelea nchi za duniani kuomba msaada baada ya vita vikubwa, virefu vilivyoanza 1955 dhidi ya Ufaransa na kumalizika April 3, 1975 kwa kuyashinda majeshi ya Marekani na washirika wake.
Vita hivi viliharibu kila kitu, kiasi wakuu walishindwa waanze wapi. Ndipo wakawa wanatembelea nchi zenye huruma duniani kutaka msaada.
Katika nchi zote za Afrika nyeusi ni Tanzania pekee iliyojitolea dola milioni 1 (sawa na dola milioni 6.5 hivi sasa). Wakati huo uchumi wa Tanzania ulikuwa ni dola bilioni 5 hivi kwa mwaka, wakati ule wa Vietnam ulikuwa dola bilioni 3.6
Hii ndiyo sababu Vietnam, katika balozi mbili au tatu ilzonazo Afrika, haikuisahau Tanzania.
Hivi sasa uchumi wa Vietnam ni dola bilioni 261 kwa mwaka, wakati ule wa Tanzania ni dola bilioni 61 tu!
Msaada wa hali na mali pia umetolewa na Tanzania kwa nchi nyiiingi zilizokuwa bado ziko chini ya utawala wa mabavu wa Wazungu, hadi Equatorial Guinea, nchi tairi zaidi Africa.
Uganda, ilipokea msaada mkubwa wa hali na mali hadi Tanzania kulemewa. Angalau nchi hiyo ilifanya uungwana mwaka 1999 na 'kuilipa' Tanzania dola milioni saba.
Angalau Afrika ya Kusini inakumbuka fadhila. Lakini hii ni kwa utashi wake, si kwa mipango ya viongozi wa Tanzania.
Watanzania wengi wanajiuliza: kwa nini Tanzania haikuifanya hisani hiyo kubwa ya wakati wa dhiki, kama ngazi ya kupandia angalau kupata upenyo wa kiuchumi na nchi hizo? Leo hii, Rwanda inafaidika zaidi na Msumbiji kuliko Tanzania, ingawaje Tanzania ina mpaka nayo, na ilimwaga hadi damu za wananchi wake huko.
Jawabu: ni ule ule ugonjwa wa Tanzania wa kufanya mambo kiholela, uvivu wa kupanga, ajizi, kupuuza na kutokuwa na clue.
Swali jingine: jee, tuwaombe hawa, kama Vietnam, warudishe fadhila?
 
Kumbe tulianza kuwa dona kantri kitambo!!! Pongezi nyingi kwa serikali ya ccm
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom