Siku niliyotaka kumuua mjomba wangu!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku niliyotaka kumuua mjomba wangu!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzizi wa Mbuyu, Jul 10, 2009.

 1. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Sina hakika kama hii habari hapa ni mahali pake, lakini naomba nivumiliwe...tuweze kushirikiana kwenye habari hii pamoja, fuatalia.......

  Nilikuwa nasoma darasa la 7, siku hiyo nimetoka zangu shule kurudi nyumbani. Wakati nakaribia kabisa na nyumbani nikamwona mjomba wangu mmoja hivi amesimama na mama yangu. Huyu mjomba alikuwa mtu wa kinywaji hivi na watu walikuwa wakimuogopa mno eti kwakuwa alikuwa askari mstaafu.

  Lilikuwa ni jambo la ajabu lililotokea yaani hadi leo nakumbuka vizuri tukio lile.
  Ilikuwa hivi, niliposogea kabisa nikaona mjomba anampiga mama ngumi usoni!!
  Sijui walitofautiana nini!? Muda ule sikujua wala sijawahi kuuliza hadi leo.

  Mama alianguka kwa namna ya kuhuzunisha sana sana sana!... Sijui nieleze vipi, lakini ninachokikumbuka vizuri ni wakati anatua chini kiubavuubavu huku akitanguliza kichwa aliita jina la baba kama kuomba msaada….!!

  Muda huo nilikuwa nimesogea karibu kabisa na walipo mjomba na mama, baada kuona mama analia vile nikapiga kelele kubwa “weweee mjombaaa!!”
  Alinisikia akageuka kunitazama, Sijui nini kilinipata nilikuwa nime changanyikiwa kwa kumuona mama yangu mpenzi katika hali ile..

  Nilimrukia mjomba, nikaenda kutua usawa wa kifua chake magoti na mikono yangu vikatua kifuani kwake huku nikiendelea kumpiga ngumi nyingi tu zisizo na hesabu hukohuko juu, naona hakutegemea shambulizi lile kutoka kwa kijana mdogo vile mwenye karibia miaka 14 hivi.
  Naona pia zile ngumi na kile kikumbo vilimchanganya akaanguka chini akitanguliza mgongo, lakini haraka haraka akainuka na kuinua jembe la mkono lililokuwa hapo karibu tu alipoangukia…
  Mimi bila kufikiri wala kujiuliza , nikamrukia tena safari hii kwa spidi na nguvu kubwa sana! Sijui niliitooa wapi! Nili ruka kama chui muwindaji mzoefu anavyo mrukia shingoni mnyama aliemzidi urefu!!
  Lilikuwa pigo la kichwa cha nguvu mno katikati ya pua na mdomo wake, hakuwahi kulitumia jembe lile,….nilimuwahi jembe likiwa juu….akalia kwa sauti kubwa na kwa kilugha NDIFWAAAAH!!
  Safari hii akadondoka chini nika mvaa tena kwa haraka mno, nikaruka juu kwa miguu yangu yote miwili nikatua kwenye kichwa chake upande wa sikio!! Akakoroma..
  Jamani mama mtamu iliniuma sana kumwona kalala pale chini kwa huzuni nyingi…ILE HALI ILINICHANGANYA!!, ikaniongezea nguvu za kumtandika mtu mkubwa vile..
  Nikamchota pale chini kama koleo lichotavyo mchanga, nika mkaba kwa mkono wangu wa kulia huku mkono wangu wa kushoto ukibana kikonyo cha ngumi yangu ya kulia ili ile kabali isifunguke kamwe!
  Akaanza kutapatapa, tukaangushana! Chini matope, mchanga vilitujaa lakini sikumwachia.,. nikazidi kummkaba kwa nguvu zaidi!! …Nikasikia ‘pepo’ mchafu akimtoka kwa sauti kubwa mara tatu! Yaani ilikuwa ajabu ndani ya sekunde kama mbili hivi pepo yule alitoka kwa sauti kubwa sana mara tatu lakini pia kwa milio tofauti!! “Wewe just imagine tu ilikuwaje!”

  Sikumbuki sawasawa kitu gani kilitokea, nikaona mama, dada yangu na mdogo wangu wana hangaika kuifungua ile kabali niliyomkaba mjomba, lakini hawakuweza! Dada yangu yeye alikuwa mkubwa wa kuweza kuelewa mambo muda huo, akaanza kulia maana sasa hali ya mjomba ilikuwa mbaya sana ……… niliendelea kumkaba huku nimetoa macho bila kuwa nadalili za kuchoka!!

  Mama yangu ndiye aliyemuokoa kaka yake yaani mjomba, yeye lilia kwa nguvu kubwa na kutaja jina langu ambalo alikuwa akiniita nikiwa nimemfurahisha kitu toka niko mtoto kama hivi “nananaa!” unaniuaaa!!!........
  Loh, nikazinduka, .. na kumwachia mjomba atua chini puu, mbende mbende, mguu mmoja huku mwingine kule na mkono mmoja huku mwingine kule! Kimyaaaaa!..
  Nilikuwa bado nimechanganyikiwa nikakimbilia nyuma ya nyumba huku nalia sasa kwa kwikwi!!...ah !

  Basi bwana, kwakumalizia ni hivi;
  Majirani wakaja wakasaidiana na mama kumzindua mjomba kwani alikuwa amepoteza fahamu!! Mimi muda huo akili zimeisha anza kunirudi nakaanza kuingiwa na hofu kwa kitendo kile nilichofanya…

  Baadae baba alikuja jioni akapewa mkanda mzima, yaani baba alikasirika sanasana! Sikuwahi kuona baba yangu akiwa katika hali kama ile akasema nimemdhalilisha! Akasema atanipiga sana hadi aniue! Eti kwanini nimempiga mjomba wangu! Alifoka, akafoka, nakufoka…kasha akaingia ndani na mama wakakaa kimya kama nusu dakika hivi, then akatoka na kusema anakwenda kunipa kipigo cha nguvu!!

  Akanishika mkono we bwana, yule mzee nilikuwa na mhara kwani alikuwa na mwili mkubwa na vidole vyake viliushika mkono wango kama vidole vya chuma! Akaanza kuniburuza,….tukatembea kama mita mia tatu hi toka nyumbani …nikaanza kuhisi mkono wake ukilegea, ukalegea na kulegea..mwisho akaniachia kabisa! Nkashangaa mno, akafunika uso wake kwa mikono yake, akakaa chini ndipo nilipogundua kuwa alikuwa anacheka sanasana! Sasa ndiyo akacheka kwa sauti kubwa mno……
  .
  He! Nikashangaa mno! Ndipo akasema umemkomesha mjinga yule!..akaendelea “hata ningekuwa mimi mtu ampige mama yangu ninge mkomesha!” akacheka tena sanaaa akasema alaa kumbe umekua sasa, hata nikifa leo ntajua mama yako nememuacha kwenye mikono salama! Mie bado nikawa nashangaa kitu kile kwani sikuamini kabisa kuwa baba kabadili msimamo kirahisi vile….

  Basi siku hiyo baba akaenda namimi bar moja hivi akaninunulia soda na ndizi za kuchoma2 pamoja na mishikaki mitatu…. Ah! Sikuamini, nikajichana, weee bwana we acha tu, nilipomaliza msikaki wa kwanza nikamtazama nikaona ananitazama kwa tabasamu kubwa lililoja upendo wa dhati kwangu……baadae nilipo maliza aliniambia nitangulie kasha ongea na mama nisisumbuliwe nikalale mojas kwa moja yeye akabaki na rafiki zake pale makunywajini..

  Hivyo ndivyo ilivyokuwa wapendwa…..

  ******************************************

  ….nimesimulia kisa hiki kama kumbukumbu kwa baba yangu mpendwa aliefariki siku kama ya leo miaka mitano ilyopita, ni majonzi sana kumpoteza mzazi mimi mwenzenu baba yangu alikuwa rafiki yangu pia alinipenda sana na mimi nili mpenda sana hata kabla ya kumpiga mjomba. Alipo staafu alirudi kijijini nilikuwa nikienda likizo tunapiga stori usiku kucha! Hadi mama ainglia kati na kitulazimisha kulala!...

  Basi, ndiyo ubinadamu kufa na kuzaliwa, … “lakini baba popote pale ulipo mie mwanao nakukumbuka sana, nakupenda… napenda siku moja mungu atukutanishe, tuje tuongee tena kwa upendo wa baba na mwana, nakulilia mara kwa mara baba yangu inaniuma kweli kwamba sitakuona tena!!?”

  Haya, Mwenyezi mungu akulaze mahali pema huko uliko………….

  10/07/2009

  ***************************************************
   
 2. fundiaminy

  fundiaminy JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2009
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 358
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Duh!mkuu cna usemi ila pongezi.kweli damu nzito.
   
 3. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  at u r 14?
  BIG NO!
   
 4. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Waswahili wanasema "Nani kama mama?!" Ni ukweli mtupu. Mkuu, asante kwa kutushirikisha tukio hilo hasa unapomkumbuka baba yako mpendwa aliyefariki siku kama ya leo. Apumzike kwa amani. Ni jambo jema kutazama nyuma ya maisha yetu na kukumbuka matukio muhimu. Yanatusaidia kukua, kujiweka sawa na kusonga mbele katika maisha.
   
 5. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Pole mzee kwa kumpoteza baba yako kipenzi.

  Wakati naanza kusoma hiyo story nilidhani utamalizia kwa kusema ilikuwa ni ndoto tu! Kumbe ni kweli yamekutokea!

  Hongera sana, umesimulia vizuri tukio hilo.
   
 6. IronBroom

  IronBroom JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 524
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Simply because wewe huwezi/usingeweza au?
   
 7. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Nashukuru ndugu yangu kunijibia, yaani hata mimi siamini kama niliweza kufanya jambo lile!! Thats why nimeliweka kwenye kumbukumbu zangu maishani!!!
   
 8. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Na wapendwa woote mlionipa pole asanteni mbarikiwe sana! Aluta continua maisha yanaendelea....
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thanks Mzizi... farther love is always special!!! especially kama umewahi kuipata. shukuru mungu you had that chance, i always thank God for that too..

  Thanks pia kwa kutuonyesha the other side of our beautiful life - pombe, domestic violence, pride ya mzee kwako na maisha baada ya ajira kwa mzee wako
   
 10. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Du ww!!!
   
 11. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Mkuu nashuru sana, maneno yako mazito mno kwangu. Ubarikiwe na Mungu aendelee kukupa Hekima hiyo iendelee kusaidia wanadamu kujitambua.
   
 12. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #12
  Jul 14, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kwa mzazi huwa ni furaha sana kuwa na mtoto anayekupenda na kuwa tayari kukulinda no matter what- I believe tukio hilo liko moyoni kwa mama yako na ni wazi huwa anatabasamu kila akikumbuka.

  Heri yako uliyenahatika kumpa furaha mama yako akingali hai!
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Jul 14, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hii mkuu mbona kama imekaa kihadithi za Shy au umeichomoa sehemu nini?
  Maana ilivyo kaa kaa kama Kishigongo gongo vile.
   
 14. M

  Msindima JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hongera sana,thread yako nimeipenda na imenikumbusha mbali sana,kwa kweli tunapaswa kuwalinda wazazi wetu kwa nguvu zetu,hongera sana.
   
 15. M

  Msindima JF-Expert Member

  #15
  Jul 14, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mhh Fidel80,mbona ameeleza vizuri tu,na kwa jinsi mimi nilivyoelewa ni kama dedication kwa baba yake ambae alifariki miaka mitano iliyopita.
   
 16. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #16
  Jul 14, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu, lakini Shy simjui kabisa wala sijui kama ni mtunzi, mtangazaji n.k
  Shigongo mie namwona kama mwandika makala, siyo mtunzi kwangu. Na huwa siwezi kusoma hadithi zake kwani zinanikifu aya ya kwanza tu!

  Hilo ni tukio la kweli lililotokea katika maisha yangu. Sema nimelitafutia maneno ambyo naliamini yatasaidia ndugu zangu woote humu ndani kunielewa.

  Mwisho nashukuru, kwa kuonyesha kuguswa na kisa changu.
   
 17. Ncha

  Ncha JF-Expert Member

  #17
  Jul 16, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Big up. May ur Dad RIP
   
 18. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #18
  May 9, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Ubungoubungo upooo!!?? kisa chenyewe ni hiki.
   
 19. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #19
  May 9, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Ubungoubungo upo?? ni hii..
   
 20. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #20
  May 9, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  kusema ukweli, mtu anayempiga mama yangu mimi kabisaaa, ananitaka ubaya. mama kabisaaaa, we acha bwana.
   
Loading...