Wachokonozi
Member
- May 2, 2025
- 7
- 11
Nawaza je siku hiyo mke WANGU atajua sijaoa jinsia yake ya kike Wala hajaolewa na umbile langu la kiume? Je atajua umri wangu na wake si kiini chetu, Wala uzuri wake si nguzo yangu ya kudumu?
Siku nikimuoa mke wangu sitamvika pete kwanza, nitamvika maswali.
Kwasababu ndoa si sherehe ya kupiga picha; ni mkataba wa kukutana na ukweli.
Na ukweli huja bila mapambo, bila manukato, bila nyimbo za harusi.
Nitamuuliza kwa sauti chungu: nimeoa nini?
Je, nimemuoa jina lake, herufi zilizorithiwa kabla hajajua kujiita?
Jina linalobeba maamuzi ya watu waliokufa, wazazi waliotamani, jamii iliyotegemea, na mababu waliokabidhi alama zao kwa makosa na matumaini?
Kama nitamuoa jina, basi nitamuoa wosia wa wengine, si mapenzi yangu.
Je, nitamuoa historia yake, mikusanyiko ya majeraha aliyojifunza kuyaita kumbukumbu?
Historia ya mapenzi yaliyomvunja, ya ahadi zilizomwacha akijijenga upya kwa vipande, vya hofu alizozigeuza tabasamu ili aishi?
Kama nitamuoa historia, basi mimi ni kumbukumbu inayoendelea, na ndoa yetu itakuwa makumbusho, si makazi ya uhalisia wetu.
Je, nitamuoa uzoefu wake, habari mpya zinazobadilika kama upepo wa jioni?
Mitazamo aliyoiga jana, misimamo aliyokopa leo, ndoto alizotengeneza kwa mikopo ya mitandao na maoni ya watu?
Maana mazoea hayakai; yanahama.
Ukioa uzoefu, unaoa msimu, na msimu ukipita, ndoa inabaki baridi.
Je, nitamuoa kabila lake, mizizi ambayo haijawahi kumuuliza kama anataka kuwa huo mti?
Mila zinazomvisha wajibu kabla ya ridhaa, miiko inayompa heshima kwa kumfunga, na fahari inayomwambia ajivune kwa kitu ambacho hakukichagua?
Je anajua akili zangu fupi zinafikiri ukioa kabila, unaoa baraza la wazee,ndoa inageuka mahakama, na upendo unakaa kizimbani?
Au je, nimemuoa yeye, yule asiye kamili, asiye tayari, asiye kamusi ya majibu?
Yeye anayebadilika bila kuomba ruhusa, anayekosea bila udhuru wa kifalsafa, anayekua bila ratiba ya kijamii?
Yeye ambaye hakuja kunifurahisha, bali kunielewa?
Yeye ambaye mapenzi kwake si pumzi ya kingo za uwanja wa seremala bali ni kazi endelevu?
Siku nikimuoa mke wangu, nitamuoa mtu, si kifurushi.
Nitamuoa kwa makubaliano ya kikatili:
Nitamwambia:
Usinipe jina lako, niletee nafsi yako.
Usinionyeshe historia yako, nionyeshe jinsi unavyoijenga upya.
Usiniuzie mazoea, nioneshe dhamira.
Usiniletee kabila, niletee utu.
Siku nikimuoa mke wangu, sitamchukua kutoka kwa wazazi wake tu, nitamchukua kutoka kwenye ndoto zake, hofu zake, na historia iliyojificha nyuma ya tabasamu lake la jua. Nitamuoa kama swali, si kama jibu. Kwa maana ndoa si mwisho wa kutafuta; ni mwanzo wa kuuliza kwa sauti ya ukimya: je, ananijua kama mume, mume wake, au amenijua kama kivuli cha matarajio yake?
Je, atanijua kama mume au kama mhusika wa hadithi aliyoandikiwa kabla hatujakutana? Atanijua kama mtu anayechoka, anayeshindwa, anayekosea, anayejifunza? Au atanijua kama sanamu ya ndoto zake, akinishikilia nisitetereke hata pale maisha yanapovuma kama upepo wa jangwani?
Lakini na mimi nitajiuliza. Je, ninamjua kama mke au kama jukumu? Je siku zote nitamtazama kama safari, si kituo. Nitamheshimu kama roho, si mali. Nitamuuliza kila siku, kimya kimya: je, namwona kama alivyo, au kama ninavyomtaka awe? Maana mapenzi hufa pale tunapopenda picha badala ya mtu.
Na kama atanijua kweli, atanijua si kwa kile ninachompa, bali kwa kile ninacholinda: utu wake, uhuru wake, na ndoto zake.
Na kila mara nitamwambia: siwezi kukupa dunia; lakini nitakupa macho yanayoona, masikio yanayosikia, na mikono isiyokimbia wakati ukweli unapoonekana mchungu. Na kifua kinachopooza pindi akijisikia kuchemsha vijito vya machozi yake maana mapenzi hayachipui kwenye maneno matamu, bali kwenye ujasiri wa kukaa mezani na ukweli ulio uchi wa uchi.
Siku nikimuoa mke wangu, nitakuwa nimevuka mpaka wa macho na kuingia kwenye nchi ya maana. Nitakuwa nimeacha ibada ya ngozi na kuanza utimamu wa fikra. Maana ndoa si tamasha la miili, ni agano la akili zilizoamua kuchoka kukimbia. Siku hiyo, atajua kuwa sikutafuta kifua chake kama hifadhi ya upweke, wala sauti yake kama kifaa cha kunilaza usingizini. Nilimtafuta kama swali gumu linalonilazimisha kuwa jibu bora zaidi kila siku.
Siku nikimuoa mke wangu, sitavaa pete ya kuvimbisha kidole changu kwa sifa za mmeliona bangili langu lililolambishwa rangi ya dhahabu? La hasa nitavaa dhamana. Nitapokea mzigo mtakatifu unaoitwa mtu, mzigo unaopumua, unaota, unaumia, unao uliza. Maana ndoa si tukio la siku moja, ni ahadi ya kila siku; si sherehe ya saa chache, ni mazoezi ya maisha.
Ndipo swali la chungu linapojitokeza: je mke atajua yeye ni mke, au atabaki kuwa mpangaji katika moyo wangu?
Kwasababu kuwa mke si cheo kinachotolewa na hati; ni lugha inayojifunzwa kwa vitendo. Ni hekima ya kujua lini ukimya ni busara na lini sauti ni tiba. Ni ujasiri wa kubeba jina langu bila kufuta utu wake. Mke si kivuli cha mume; ni uso unaoakisi jua kwa namna yake. Siku nikimuoa, natamani ajue kuwa kuwa mke wangu si kufa, ni kuzaliwa upya katika heshima ya utupu wetu.
Nawaza siku nikimuoa mke wangu, nitakuwa nimemkataa kwa mara ya kwanza ili nimkubali kwa umilele. Nitakuwa nimemkataa kama mali na kumkubali kama dhamiri. Nitakuwa nimemkataa kama mapambo ya jina langu na kumkubali kama mhimili wa kusimamia maumivu yangu. Kwa sababu anayemuoa mwanamke kwa tamaa, humaliza tamaa na kumaliza ndoa; anayemuoa kwa maana, humaliza ubinafsi na kuanza safari.
Siku hiyo, atajua kuwa sikumchagua kwa sababu alinipendeza, bali kwa sababu alinikasirisha kwa ukweli. Alinivua visingizio, alinivunja vioo vya kujipendeza, alinifanya nione upweke wangu hadharani. Alinisoma bila kunipapasa, akanisahihisha bila kunidharau. Na hapo nikajua: huyu si mwanamke wa kunifariji, ni mwanamke wa kunijenga.
Siku nikimuoa mke wangu, nitakuwa nimekubali kuoa hofu yangu. Kwa maana ndoa si kukimbia majeraha, ni kuyapa ratiba ya kupona. Tutakaa mezani si kwa chakula, bali kwa majuto. Tutalala kitandani si kwa usingizi, bali kwa maswali. Na asubuhi tutainuka si kwa ushindi, bali kwa uamuzi wa kuendelea kuwa waaminifu hata pale uaminifu unapouma.
Siku hiyo, atajua kuwa sina miujiza ya kumwahidi. Sina mbingu za bei rahisi. Ninamleta katika ardhi inayodai kazi, jasho, na mazungumzo marefu yasiyomalizika. Ninamleta katika nchi ambayo upendo si neno la kutamka, bali ni nidhamu ya kila siku: kusikiliza kabla ya kujitetea, kukiri kabla ya kushinda, na kusamehe kabla ya kuhukumu.
Siku nikimuoa mke wangu, nitakuwa nimechagua mwanamke anayeweza kuniacha huru bila kuniacha. Atajua kuwa sitamfunga kwa wivu, sitamlea kwa hofu, sitamfanya kifungo cha ndoto zangu. Nitamruhusu awe mkubwa kuliko mapenzi yangu, kwasababu mpenzi mwenye kichwa cha kuazima huogopa ukuu wa anayempenda hivyo nitataka auone ukuu wa kichwa changu kwamba si mlima tu wa kukuzia nywele. Na yeye ataniruhusu nishindwe bila kunidharau, nikose bila kunipoteza, nikue bila kunipunguza.
Nawaza siku hiyo nitamuuliza kimya kimya: je unajua maana ya kuwa wangu? Ni kukua nami bila kukosa nafasi ya kukua peke yako. Ni kunikosoa bila kunidharau, kunipenda bila kunimiliki, kunisubiri bila kujisahau. Kuwa wangu ni haki ya kuniambia “hapana” kwa upendo, na “ndiyo” kwa uhuru. Ni kujua kuwa nguvu ya ndoa haipo katika kushinda mabishano, bali kuelewa tofauti zetu?
Siku hiyo, tutakuwa tumeona wajibu wa kusema ukweli hata unapochelewesha furaha. Tutakuwa tumeona kimya kinachojua lini kuzungumza kunaua. Tutakuwa tumeona adabu ya kutokimbia mazungumzo magumu. Kwasababu ndoa si kukubaliana kila wakati; ndoa ni kukubaliana kubaki hata pale kukubaliana kunaposhindikana.
Siku nikimuoa mke wangu, nitakuwa nimemkuta mwanamke anayejua kuwa upendo haupimwi kwa sauti ya “nakupenda” bali kwa uzito wa “nipo”. Mwanamke anayejua kuwa ahadi si kile kinachosemwa siku ya sherehe, bali kile kinachofanywa siku ya mvua. Na mimi nitakuwa mwanaume anayejua kuwa uume si sauti ya amri, bali uti wa mgongo wa kuwajibika.
Siku nikimuoa mke wangu, natamani ajue kuwa nimechagua safari, si kituo; nimechagua kazi, si tuzo; nimemchagua yeye, si picha yake. Na hapo, labda, nitaanza kujua maana ya kuwa mume kuwa si kwa kumiliki, bali kustahili.
Siku nikimuoa mke wangu, sitamwomba anifanye mfalme. Nitamuomba anikumbushe kuwa utu. Kwa maana ndoa si kiti cha enzi, ni uwanja wa majeraha na uponyaji.
Nawaza je ikitokea siku moja tukazeeka, nyuso zetu zikikosa kumbukumbu ya urembo, miili ikaanza kuandika barua za uchovu, je nitamkumbusha kwa ukimya ule ule wa siku zetu za gizani?
Na ikiwa siku moja atauliza,
“Ulinioa nini?”
nitamjibu kwa maneno tisa.....