Siku nikifa

Siku nikifa

KHM 1995

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
461
Reaction score
731
Siku nikifa maisha mapya yataanza, nuru ya macho yangu itapotea taratibu, tazama watu wanaonizunguka watalia na kuomboleza lakini haitasaidia nimelala siwezi kuamka tena.

Wataandaa kaburi langu, watalichimba kwa futi kadhaa waufukie mwili wangu, huzuni imetanda kwenye nyuso zao, mwili wangu umebebwa ndani ya jeneza, sasa unapelekwa katika nyumba ya milele.

Tazama jeneza langu linatupiwa taratibu katika kaburi langu,tazama wanatupia udongo katika kaburi langu, tazama Giza totoro limetanda safari, wameniacha.

Kifo
 
Utakufaje...!!!Unaweza kufa kama P.lumumba ukatupwa kwa tindikali,Au Ukaliwa na fisi mithili ya james hadley a virture is patient bird Au ukafukiwa na kifusi katika migodi ya mabepari Au ukaliwa nyama mbichi na antibalaka:
 
Kifo ni kifo roho itaondoka katika mwili
 
Siku nikilala lala mautiiii, hakuna awezaye kuniqmshaaaa,Ni vilioooo
 
Huyo mtoa post atakuwa ajielewi.
Kifo ni fumbo kubwa sana Kwa wanadamu.
Sio watu wote wanaokufa wanazikwa kaburini
 
Kifo ni kifo roho itaondoka katika mwili
Nimejaribu kutoa picha kubwa ya aina za vifo,Je waweza kuipata adhabu ya kaburi wakati umemezwa na chatu au umetafunwa na simba wa RUAHA NATIONAL PARK..,???
Kifo ni kifo roho itaondoka katika mwili
Nimejaribu kutoa picha kwa upana juu ya vifo,Je unaweza kupata adhabu ya kaburi ikiwa umemezwa na chatu wa pori tengefu la sumbawanga au umetafunwa na simba wa RUAHA NATIONAL PARK..?
 
Huyo mtoa post atakuwa ajielewi.
Kifo ni fumbo kubwa sana Kwa wanadamu.
Sio watu wote wanaokufa wanazikwa kaburini
Nadhani kufahamu aina za vifo watu hupitia dunia hii na tamaduni za watu wengine katika kila kona ya dunia ni nzuri zaidi, nimehudhulia mazishi ya kuchoma maiti/mwili kwa jamii ya wahindi mara tano!
 
Tone ya uzi wako inanikumbusha wimbo wa KAMANDA-DAZNUNDAZ...Alazwe mapeponi kamanda,,hizi tone zote na yako ni matokeo ya world view za abramic religions(islam,christianity& judaism), kumbuka kuna rebith-hindiusm,sikhism.
 
Siku nikilala lala mautiiii, hakuna awezaye kuniqmshaaaa,Ni vilioooo
Ni kilio mkuu kwa wanaokuzunguka lakini itakuwa ushindi mkubwa sana kwangu,safari ya amani inapowadia,sitakuwa na stress kama nilivyo hai, maisha yangu yote yanakua ya ndotoni
 
Ni kilio mkuu kwa wanaokuzunguka lakini itakuwa ushindi mkubwa sana kwangu,safari ya amani inapowadia,sitakuwa na stress kama nilivyo hai, maisha yangu yote yanakua ya ndotoni
Mkuu,una maanisha wewe una prefer kifo kuliko uzima ? ,Kifo kinatisha kwa sababu hatujui tuendako kupoje
 
Mkuu,una maanisha wewe una prefer kifo kuliko uzima ? ,Kifo kinatisha kwa sababu hatujui tuendako kupoje
Mkuu kifo ni daraja la kupumzika dhidi ya changamoto za duniani zisizokuwa na mwisho,zimejaa maumivu makubwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom