Los técnicos
JF-Expert Member
- Sep 14, 2014
- 3,010
- 2,604
Kisa hiki ni sehemu ya mlolongo wa matukio mbalimbali katika historia ya maisha ya Mwalimu Nyerere.
Inaelezwa kuwa mwaka 1994 Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi walimfuata Mwalimu Nyerere nyumbani kwake Butiama wakamwambia anakishusha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwasiliana na wapinzani. Walipomaliza Mwalimu akakaa kimya kwa muda kisha akaanza kuwauliza maswali. Je mnaponiita Baba wa Taifa ninakuwa kwa ajili ya wana CCM tu? Je hapa kwangu mmekuja kunikamata sababu mna Jeshi na Polisi?
Mawaziri wale wawili waliomfuata Mwalimu wakamjibu kuwa wametumwa na Halmashahuri Kuu ya CCM. Baada ya kuona hawampi majibu ya maswali aliyokuwa akiwauliza Mwalimu akawaacha wamekaa akaingia ndani. Mzee Kasori aliyekuwa Katibu wake anasema Mwalimu aliingia ndani kuchukua kadi yake ya CCM ili airudishe ila yeye akamzuia.