Siku Mwalimu Nyerere alipotaka kurudisha kadi yake ya CCM

Los técnicos

JF-Expert Member
Sep 14, 2014
3,011
2,604
Kisa hiki ni sehemu ya mlolongo wa matukio mbalimbali katika historia ya maisha ya Mwalimu Nyerere.

Inaelezwa kuwa mwaka 1994 Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi walimfuata Mwalimu Nyerere nyumbani kwake Butiama wakamwambia anakishusha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwasiliana na wapinzani. Walipomaliza Mwalimu akakaa kimya kwa muda kisha akaanza kuwauliza maswali. Je mnaponiita Baba wa Taifa ninakuwa kwa ajili ya wana CCM tu? Je hapa kwangu mmekuja kunikamata sababu mna Jeshi na Polisi?

Mawaziri wale wawili waliomfuata Mwalimu wakamjibu kuwa wametumwa na Halmashahuri Kuu ya CCM. Baada ya kuona hawampi majibu ya maswali aliyokuwa akiwauliza Mwalimu akawaacha wamekaa akaingia ndani. Mzee Kasori aliyekuwa Katibu wake anasema Mwalimu aliingia ndani kuchukua kadi yake ya CCM ili airudishe ila yeye akamzuia.
 
MKAPA na CCM walikaribisha Mabeberu, Akina Barrick, Geita Gold, etc ...

MKAPA akaruhusu Mabeberu waibe Hold

Wasukuma Bulyankulu na Nyamongo, wakauawa na kupigwa...

Magufuli na CCM yake wakachekelea na hawakukemea... Magufuli akafurahia posho Nene Nene na mshahara wa uwaziri...hakufungua mdomo kutetea wasukuma.

Lazima Watanzania tukumbushane.

Bavicha na Bawacha wekeni hii record kwenye social media..

Molemo Sky Eclat

Erythrocyte
 
Mjamaa aliefia kwny Hospitali ya Mabeberu then tukagoma Mwili wake usibebwe kwny Ndege ya Mabeberu ya British airways tukamrudisha kwa Air Tanzania kumuenzi kwa Siasa yake ya kujitegemea
 
Mungu amrehemu Mwl. Nyerere, alipenda na kusimamia haki na usawa kwa watu wote na ndiyo msingi wa amani aliotuachia . Upinzani siyo uadui ni kutofautiana mitazamo tu, utaifa , utu na undugu wetu bado upo pale pale.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom