Siku Kikwete akizungumza nchi itasimama

Ukiangalia vizuri utagundua JK kwenye siasa ni mbobezi na ndio maana hutamsikia akifungua mdomo ila vitendo utaviona muda si mrefu.
miiko ya viongozi wa staafu di yakuongeaongea hovyo
 
Matamanio yangu ni kuona maraisi wastaafu na viongozi wengine wastaafu, kwa namna fulani wanaingilia uongozi huu na kumuweka kwenye mstari sahihi huyu JPJM. Binafsi Nina was I wasi sana kama kweli anafanya maamuzi ya kimkakati. Naona anakuwa reactive badala ya kuwa proactive. Hotuba zake ni zile zile siku zote toka 2015 wakati wa kampeni.

Huyu 'mtukufu' ni lini atasema maneno ya kutia moyo na kuwaunganisha watanzania badala ya kuwagawa?
Ni lini atakapofariji badala ya kuumiza?
Ni lini atakapotenganisha kazi take, kama raising was JMT na kazi take kama mwenyekiti was ccm?
Ni lini atakapokoma kuwachukulia 'wapinzani' kama maadui na wasaliti na kuwachukulia kama wabia was maendeleo?
Ni lini atakapoacha mihimili mingine ifanye kazi take kwa Uhuru?

Nafikiri wakati ni muafaka kwa wenye hekima kuvunja ukimya na kumrejesha 'mtukufu' mstarini, kwa siri au uwazi.

Nchi hii inapelekwa kusiko na mwisho wa siku historian itatoa hukumu ya haki kwa serikali ya JPJM; lakini sisi tunaokaa kimya na kuendelea kuacha nchi hii ipelekwe kusiko kwa kuogopa tu "kinyago tulichochonga wenyewe", historia itatuhukumu bila huruma adhabu Kali tutaipata toka kwa kizazi kijacho.

Time will tell!
 
Hata msemeje, JK, hakufaa kuwa Rais, ukiniuliza mimi JK. kafanya nini ndani ya miaka 10 yake nitakuonesha UDOM tu na Rock City Mall ya Mwanza, sioni kitu kingine...

JK. alifanya vitu vyepesi mno, na muda mwingi akautumia ughaibuni, acheni ujinga...

Magufuli ndiye Rais, na namkubali kupita kiasi, nchi ilitakiwa ipate Rais kama huyu, manufaa ya uongozi wake wengine mtaanza kuyaona baadae...

ila najua wengine humu njaa ndo inawasumbua, fanyeni kazi acheni kuandika-andika humu haiwasaidii chochote....
 
Tulishuhudia wakati wa kampeni mgombea akimponda kiongozi aliyekuwa madarakani.Tukajiuliza lakini tukaona inaweza ni mbinu wametengeneza ili kupata ushindi.

Ushindi umepatikana lakini kila siku awamu iliyopita inasimangwa,inapondwa na inakejeliwa wakati anayeponda alikuwa humo humo.Wanadiriki kusema "nchi ilioza" wakati walikuwa sehemu ya kilichosababisha uozo.

Kauli hizi zitavuka threshold value na wanaojua kusema wakiamua kusema nchi itasimama.

Mungu mpe busara la sivyo,mmh.
Nyie watu acheni mahaba nchi hii ilioza haswa kwani uongo
 
Ni kweli yeye ndiye rais, kwani tumebisha..??

Kwa sababu unasema WEWE UNAMPENDA, no one anaweza kubadilisha maamuzi yko. Na unachokipenda wewe sio lazima wengine wakipende. Ni kama kumpenda mwanamke, hata waseme vipi, huwezi kusikia.
 
Nyie watu acheni mahaba nchi hii ilioza haswa kwani uongo
Ilioza sehemu gani? Na kama ilioza, ulihimilije kukaa ndani ya uozo? Unajikanganya na kujichanganya kwa kuamini nchi ilioza ilihali ninyi ni mazao ya uozo huo kwani hata mavazi uliyovaa sasa ulinunua ndani ya uozo ule. Kuwa mkweli kama tangu 2015 umemudu kununua hata boxer au hata v.i.p na sox jozi moja?
 
Nyie watu acheni mahaba nchi hii ilioza haswa kwani uongo
Ilioza sehemu gani? Na kama ilioza, ulihimilije kukaa ndani ya uozo? Unajikanganya na kujichanganya kwa kuamini nchi ilioza ilihali ninyi ni mazao ya uozo huo kwani hata mavazi uliyovaa sasa ulinunua ndani ya uozo ule. Kuwa mkweli kama tangu 2015 umemudu kununua hata boxer au bata v.i.p na sox jozi moja?
 
Tulishuhudia wakati wa kampeni mgombea akimponda kiongozi aliyekuwa madarakani.Tukajiuliza lakini tukaona inaweza ni mbinu wametengeneza ili kupata ushindi.

Ushindi umepatikana lakini kila siku awamu iliyopita inasimangwa,inapondwa na inakejeliwa wakati anayeponda alikuwa humo humo.Wanadiriki kusema "nchi ilioza" wakati walikuwa sehemu ya kilichosababisha uozo.

Kauli hizi zitavuka threshold value na wanaojua kusema wakiamua kusema nchi itasimama.

Mungu mpe busara la sivyo,mmh.
Hapana! Nchi italala kifo cha mende
 
Back
Top Bottom