Siku itakayibadilisha maisha yako kabisa

Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2017
Posts
10,491
Reaction score
20,065
Salamu waungwana JF[emoji1538]

Niongee na vijana wakike na kiume hasa vijana wa kati ya miaka 20 hadi 30.

Leo ni mwaka wa tatu tangu umalize elimu ya juu pale UDOM, UDSM, MZUMBE, TUMA, SAUTI, AU, TICD, TUDARCO au pale KCMC

Umerudi nyumbani yalipo maskani uliyolelewa tangu mdogo hadi umekuwa, pale ndipo kilipo chanzo/shina la mizizi yako kimafanikio na kimapungufu.

Ndani ya miaka mitatu hii au hata zaidi au pungufu bado haujawa na uwezo wa kujikimu kimaisha wala uwezo wa kukusanya kipato, hali inayokupa hofu ya maisha, ndugu wanakuona mzigo, uliowategemea wakupe michongo nao huwaoni tena, unaitaji kujenga mahusiano na mdada/mkaka kwa ndoto ya kufika mbali pamoja humpati wanakudharau huna kazi huna pesa, unapiga moyo konde unajisemea "huyu angejua nina elimu siku mambo yakikaa vyema nimetoka kimaisha angetulia na mimi"

Haya yote hayatakusaidia kubadili maisha yako kaka/dada yangu. Unahitaji KUBADILIKA, unahitaji kubadili mtazamo wako juu ya maisha, unahitaji kuyakumbuka uliyoyasoma kwenye vitabu vya fasihi sekondari na kuyatafakari kwa mazingira halisi ya sasa na ujiulize je, yanawezekana? Vaa uhusika kamili.

Baada ya hapo, amua maamuzi magumu, maamuzi ya kuondoka lilipo shina la mizizi ya maendeleo yako, ondoka sehemu/mtaa/kijiji/kata na wilaya uliyozaliwa na kukulia. Ondoka kabisa nenda katafute mafaniko mbali na hapo. Hapo ulipo wanakufahamu na watakuchukulia kama mtu anaejiandaa na kukua si anaetafuta mafanikio. Kumbuka "mtoto kwa mama hakui" na "nabii hatambuliki kwao" basi ONDOKA

Ukiisha kuondoka jiepushe na mambo yafuatayo huko ugenini:-

1. Epuka makundi rika, kaa nayo kwa akili kubwa
2. Epuka mahusiano ya kingono na wenyeji hiyo si shughuli iliyokupeleka huko
4. Fanya maamuzi kwa haraka bila kuhofia huyu atanionaje au nitapata hasara gani au siyawezi haya
5. Jitume sana kua na adabu ishi vizuri na wazee, wakina mama na watu wazima wa miaka 45 kuendelea kwa lengo la kujifunza maisha.
6. Mwisho usiwe mlevi wala mshirikina, jiweke karibu na imani yako sali/swali kwa juhudi na unyenyekevu ila usitegemee miujiza hiyo HAIPO

Kijana mwenzangu ukitaweza haya hakika utabadili maisha yako, ila kumbuka kuwa usitafute utajiri bali tafuta maisha yatakayokuhudumia wewe na wale utakaopenda kuwahudumia ili yakupe furaha maishani.

Sote tuwe na siku njema

VIIXCCCL GrandLodge,ARUSHA
 
Ushauri mzuri sana ,nakumbuka miaka ya nyuma sana mchungaji wangu alimishauri the same...kuhama nilipokulia.

It worked fine kabisa.

Hili jambo huwa vijana wengi hawalitambui sijui ni kwanini mkuu.

Ubarikiwe
 
ww ulishawahi kufanya hivo na kuonja

mafanikio? Au nyie ndo wale mnahubiri msioyatenda. ([emoji23][emoji23][emoji23]natania)

Huu ni ujumbe wa kweli ambao kijana akiufuata lazima atatoboa. Ni vigumu sana kufanya mishe za kutumia nguvu na kuchafuka ukiwa maeneo ambayo watu wengi wanakujua. Ni vizuri ukaingia kusikojulikana ukapiga mishe ukapata hela ya kutosha kisha unarudi kwenu.

Nimepanga kufanya hivo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hakika mchagua jembe si mkulima, ukizungusha bahasha bila mafanikio kuna haja ya kujichanganya na kujaribu option nyingine kikubwa uthubutu
 
Back
Top Bottom