Siku inakuja ambayo kila msaliti atalipia usaliti wake kwa gharama anayostahili .

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
72,866
2,000
Hiki nilichoandika hapa si kitisho kwa mtu yeyote yule , lakini ifahamike wazi kwamba USALITI NI DHAMBI na ni dhambi iliyobeba LAANA KUBWA SANA , kumbukeni kwamba tangu enzi na enzi Mungu amekataza dhambi , na isisahaulike kwamba dhambi ya usaliti haina msamaha na wakati huo huo inaweza kutafuna mpaka kizazi cha 4 cha mhusika ( hii ni kwa mujibu wa maandiko matakatifu ) .

Kila aliyeumizwa na Usaliti hana haja ya kusikitika wala kukata tamaa , Mungu hajawahi kuwa fala na ndio maana mpaka leo hakuna uovu uliowahi kushinda wema katika jambo lolote , wala hakuna muovu aliyewahi kuwashinda watu wema , Nelson Mandela pamoja na kutandikwa kifungo cha miaka 27 jela bado aliweza kusimama na kuongoza nchi yake katika cheo cha Urais.

Ewe Mzazi mkanye mwanao ajiepushe na usaliti na hasa usaliti wa kisiasa , wakumbusheni wapendwa wenu maneno ya Mungu juu ya adhabu ya Msaliti , maana MCHUMA JANGA HULA NA WA KWAO.

A dreamer be the one  A winner be the one  A fighter be the one.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom