Siku hizi kuchanganya siasa na dini Rukhsa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku hizi kuchanganya siasa na dini Rukhsa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Aikaotana, Jan 1, 2011.

 1. A

  Aikaotana Senior Member

  #1
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilizoea kusikia kauli za msichanganye dini na siasa kwa kasi kipindi chote kabla ya mwaka 2005, viongozi wa serikali , dini walisimama imara kuwakemea mashehe wakiwatuhumu moja kwa moja kuacha kujadili siasa misikitini. Kipindi hicho ufisadi uliokuwa ukifanywa na viongozi wa kisiasa haukuwa miongoni mwa mada za kujadiliwa, na watu waliojaribu kujadili walikemewa kutochanganya siasa na dini.
  Nakumbuka mambo kadhaa ya kifisadi yalitendeka ambayo yamekuja kuwekwa bayana kipindi cha awamu ya 4 ya JK yakiwemo:
  • Ununuzi tata wa Rada (watanzania acheni uvivu wa kufikiri)
  • Ununuzi tata wa ndege ya rais(hata mkila majani ndege ya rais itanunuliwa)
  • Meremeta
  • Mikataba mibovu ya madini ,ambayo ilifanywa kuwa siri awamu iliyopita,
  • Kuuzwa kwa bei ya kutupa NBC, na ubinafsishaji tata wa Shirika la Reli
  • Mkapa kujimilikisha mradi wa kiwira.
  • Kuuza Nyumba za serikali kwa bei ya kutupa
  • EPA saga
  • Ujambazi uliokithiri (umehusishwa na viongozi wa jeshi na watawala ref. hotuba ya Mkapa ‘Hakuna nchi isiyokuwa na majambazi, Marekani, Uingereza …..
  • N.k,…N,k
  Katika mlolongo wa matukio ya kifisadi hapo juu, sikuwahi kusikia kauli za viongozi wa juu wa Makanisa kukemea au kuonya serikali juu ya kuwepo kwa ufisadi huo,aidha masuala ya Katiba Mpya yaliongelewa sana na Watu wa haki za binadamu na hayakupewa uzito wowote na wanasiasa na viongozi wa Makanisa, Miaka michache baada ya utawala wa JK ulitoka waraka kutoka kanisa Katoliki ulioitwa wa elimu ya kupiga kura lakini kwa kiasi kikubwa ukiongelea suala la ufisadi. Leo kuna vuguvugu kubwa la kutaka katiba mpya lililoibuliwa na , Viongozi wa kanisa wamekuja juu kushabikia suala hili la kisiasa, Kanisani na nje ya Kanisa . Imefikia wakati Kiongozi wa Kikristo -CCT anataka katiba Mpya ipatikane haraka iwezekanavyo, lakini baada ya utafiti wa kina kufanyika(Mwananchi tarehe 17/12/2010). What a controversial statement? ,eti iwe haraka, lakini baada ya utafiti wa kina, utafiti wa kina wa harakaharaka?.
  Hivi karibuni nimesoma tena Mwanachi, Maaskofu sasa wambana JK , ndani yake kuna masuala ya kisiasa ambayo bila shaka yaliyojadiliwa kanisani au viunga vyake.

  Wapo wapi viongozi waliokuwa wanawakemea Mashehe wasijadili Siasa ?

  Wapo wapi wazee wa Msichanganye dini na Siasa?
   
 2. m

  mzambia JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Ndo utandawazi unafikiri kingunge anaweza kumkemea mufti mkuu au askofu mkuu wkt yeye si msafi?
   
 3. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #3
  Jan 1, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hakuna kuchanganya siasa hapa. Jambo likienda mrama lazima likemewe na mwananchi yeyote tena kwa nguvu zote. Viongozi wa dini ni sehemu ya jamii kwa hiyo sioni tatizo.
   
 4. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #4
  Jan 1, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,831
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  Tatizo lenu mnataka muachwe tu mfanye madudu yenu na kuwaumiza wananchi halafu watu wakae kimya.Hivi hufahamu kuwa viongozi wa dini pia ni wananchi wa nchi hii na wanaathiriwa na hayo madudu yenu?Sasa wakikemea uovu,wanachanganya dini na siasa,bah!
   
 5. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  mimi nadhani viongozi wa dini wote kwa pamoja wana haki ya kutoa maoni yao iwe viongozi wa kiislam, kihindu, kikristo hata wa kipagani, il mradi wanataka nchi yetu isonge mbele sio kutetea mtu yoyote kisa ni wa dini yako au sio wa dini yako. usiwalaumu viongizi wa dini ni moja ya kazi yao
   
 6. A

  Aikaotana Senior Member

  #6
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ok naona wachangiaji wote hapo juu wanakiri kuwa ni haki kwa viongozi wa dini kutoa maoni yao, na pengine mimi sibishani na hili sana , issue hapa kwa nini wakati huu, kama ni matukio ya kifisadi yalifanyika sana kipindi cha awamu iliyopita, ni kwa nini hawa viongozi wamekurupuka kipindi hiki cha JK, walikuwa wapi wakati madudu makubwa ya maangamizi ya taifa yanafanyika, ni kwa nini leo? kuna nini? ikumbukwe kuwa ni hawa hawa walituambia tumchague JK ni chaguo la Mungu, sasa ni nchaguo la nani? ni ufisadi tuu?
   
 7. T

  Topical JF-Expert Member

  #7
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ndio demokrasia inakuwa, hakuna tena wa kumuzuia askofu/sheikh kuanzisha chama cha siasa..haina tatizo wewe changanya tu..

  Ndio maendeleo yenyewe..na kukua kwa demokrasia.
   
 8. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,148
  Likes Received: 1,882
  Trophy Points: 280
  Katiba inampa haki ya kuongea chochote ili mradi havunji sheria lini aongee sisi hayatuhusu shauri yake ili mradi haja vunja sheria!
   
 9. M

  Mwanaume Senior Member

  #9
  Jan 1, 2011
  Joined: Oct 11, 2009
  Messages: 122
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  kwani kama wakati huu tatizo nini? Kukusaidia, ni wakati huu kwa sababu watu sasa wamechoka kuendelea na hayo madudu ya viongozi wenu wasio waadilifu
   
 10. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #10
  Jan 1, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ngugu Aikaotana, tafasiri sahihi ya kwanini sasa, ni kukua kwa demokrasia na kuzidi kuamka kwa watu. Na tegemea mamkubwa zaidi siku za usoni; kumgomea Rais wa nchi itakuwa ni kawaida, kama inavyojiri leo Bolvia. Serikali ilipandisha bei ya petroli, nchi nzima ikazizima na vurugu mtindo mmoja; jana kaamua kufutilia mbali ongezeko hilo. Leo hii Tanzania bei ya umeme juu; watu wanalalamika chini chini; miaka zijazo uvumilivu utakoma, na wataanza andamana kwa vurugu kulazimisha serikali yeyote iliyoko madarakani kuzuia uovu unaoumiza wananchi kwa maamuzi ya ki imra!! Kwa hiyo mabadiliko ya kifkri ni swala la wakati na si "VINGINEVYO"
   
 11. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #11
  Jan 1, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mzee Mkapa wa watu alidanganywa na wanamtandao mafisadi wakubwa waliohakikisha jk anaingia madarakani. Msimsingizie mzee wa watu. Wezi ni jk na timu yake.
   
 12. M

  Mtwike Senior Member

  #12
  Jan 1, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kweli lakini? Si udini tu. Waislamu hawalaumu, kwa nini? na wakristo walinyamaza wakati ule , kwa nini? jawabu iko wazi
   
 13. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #13
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  jamani wengine tumeamua angalau kwa leo tusahau siasa za bongo tu enjoy mwaka mpya. Nipo na mke wangu jungle club, fox hill parade. Tunasherekea mwaka mpya. Heri ya mwaka mpya kwa wote.
   
 14. A

  Aikaotana Senior Member

  #14
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapa unadanganya na sijui unaficha nini? Mkapa ndio imedhihirika kuwa rais aliyekuwa fisadi kiasi cha kufanya biashara akiwa ikulu mf. issue ya mradi wa kiwira, na kama nilivyoonesha hapo juu ufisadi wote ambao unaitikisa nchi leo kwa kiasi kikubwa umetokana na utawala wake.
   
 15. J

  JokaKuu Platinum Member

  #15
  Jan 1, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,958
  Trophy Points: 280
  ..mmeshaambiwa wizi ulitokea wakati wa Mkapa.

  ..sasa mlitaka Mkapa ajikamate mwenyewe??

  ..anayetakiwa kumshitaki Mkapa au watendaji wake ni Kikwete.

  ..tatizo la Kikwete ni kwamba analeta ubabaishaji ktk kushughulikia suala hili.

  ..kule kwa Mramba alikwenda na kumpigia debe kuwa ni "panga la zamani lakini makali yaleyale."

  ..Chenge naye anatajwa kuchukua hongo ya rada lakini Kikwete hakumuondoa ktk cabinet mpaka alipoomba mwenyewe.

  ..panapotokea matatizo wananchi wanamuangalie kiongozi aliyepo madarakani achukue hatua.

  ..hata sasa hivi huwezi kusikia Wamarekani wakimlaumu George Bush, wanamlaumu Obama kwa kushindwa kurekebisha uchumi.
   
 16. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #16
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  Nikupe mfano. Ukipanda basi la abiria na dereva akaendesha vyema hutosikia watu wakimlalamikia dereva yule. Basi hilo watu wengi hushikwa na usingizi kwa asilimia kubwa. Akiendesha vibaya, watu hawatosinzia tena na watalalamika na kumuomba aangalie bumps nk. Tatizo la hawa viongozi wa dini kudai katiba halikuwepo kwa kuwa waliokuwa wakiongoza hawakuwa kama waliopo. Ubinafsi umekuwa nk. Hali hiyo itaendelea na kwa bahati mbaya haitakemewa kwa kuwa waongozaji si wasafi kwa kiasi kikubwa. Thats my thinking.
   
 17. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #17
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  walifikiri ni chaguo la mungu. Na mimi nikiwemo nilitarajia angechukua hatua kuwashtaki wote waliokwiba. Hakufanya hayo na anaendelea kufanya zaidi ya hapo. They are right na ni haki yao kikatiba na kiuchungaji pia.
   
 18. A

  Aikaotana Senior Member

  #18
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NAONA WOTE MNAJICHANGANYA, mtazamo sahihi ni kuwa WAKATI WA nyerere KANISA LILIPEWA KIPAUMBELE KATIKA SIASA ZA NCHI HII, UTAKUMBUKA IMMEDIATELY BAADA YA MWINYI KUKABIDHIWA MADARAKA, KANISA KATOLIKI LILIONA LINAWEZA KUPOTEZA PRIORITY WALIYOPEWA KWA MIAKA MINGI, PAPA WA KATOLIKI ALIKUJA TANZANIA WAKATI HUU ILI KUWEKA MAMBO SAWA!, IKUMBUKWE KUWA ALIPOINGIA MKAPA KANISA HALIKUWA NA TENSION YEYOTE KWA SABABU ALIYEINGIA NI MTU WAO, WALIKUWA NA UHAKIKA KUWA MOU WALIOIPENYEZA ITAFANYA KAZI YAKE BILA MATATIZO YEYOTE, KILICHOFANYIKA MKAPA ALITEKELEZA MOU YA KANISA NA YA KWAKE MWENYEWE*KUJITWALIA MALI ATAKAVYO NA KWA NJIA YEYOTE) NA MARA ALIPOINGIA KIKWETE WAKAONA NJIA PEKEE NI KUMTANGAZIA KURA YA MASLAHI, MAANA KWA WAUMINI KUAMBIWA KUWA FULANI NI CHAGUO LA MUNGU INA MAANA UMEWAAMBIA WAMCHAGUE MTU HUYU, NA KWA KWELI WALIMCHAGUA HATA AKAPATA USHINDI WA KISHINDO, KUNA KITU KIMETOKEA AMBACHO JK AMETOFAUTIANA NA HAWA MAASKOFU NA HIVYO KUANZA KUMSHAMBULIA NA HATA KUWAAMBIA WAUMINI WASIMCHAGUE TENA, MIMI NAONA NI ULE ULE UMAFIA WA KANISA KATOLIKI DUNIANI KUENDELEA KUFAIDI PESA KUTOKA SERIKALI ZA KISECULAR KUPITIA KUJIZATITII KWAKE KATIKA MIPANGO NA PROPAGANDA, HAYA YOTE YA UTEKELEZAJI WA MOU YA SERIKALI NA KANISA YANAWEZA KUWA BAADHI YA SABABU.
   
 19. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #19
  Jan 2, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hao ndo wakristo waTanzania. Ni zaidi ya uwajuavyo. Lakini safari hii hamna kulala. lazima tuongoze wote. Hamna mgao kwa kanisa, kodi zote kwenye mashirika ya dini zifutwe isipokuwa zile zenye tija tu na hasa kama kutakuwa na ulazima. Miaka 49 wameongoza peke yako na wapo karibu kila nyanja, hamna maendeleo yoyote waliyofanya zaidi ya kutuibia tu. sio sisi tu na hata wao wenyewe ambao hawako kwenye system tupo nao huku mtaani wamechoka kama sisi. sasa basi, IMETOSHA.
   
 20. A

  Aikaotana Senior Member

  #20
  Jan 12, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo ambalo Kanisa hailijui na pengine linapendelea iwe hivyo ili vita vije kama walivyofanya huko Rwanda ni kuwa kwa kawaida , you can fool the people for some times but you cant fool the people all the time! Baada ya Nguvu walionayo kujulikana na wananchi walio wengi wakaamka watawapunguza kwa nguvu ya kura, maana baada ya waislamu kupata elimu uwezo wa kuwapunguza upo. N a elimu ya bure ni hii ya uchaguzi uliopita ambao ilifikia wakristo wakamfananisha Slaa na Yesu moja kwa moja
   
Loading...