Siku hizi hamna vipindi vya Muziki kabisa

Siku hizi hamna vipindi vya Muziki kabisa

Migomba

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2013
Posts
945
Reaction score
1,339
Zamani kidogo clouds Fm walikuwa na doctor beats ambayo kwa sasa inaitwa xxL. Alikuwa anasimama Bony luv kama DJ na ML Chris kama Mc ilikuwa muziki mwingi, salamu kidogo na story kidogo. Akaja Steve B na baadae Venture still muziki ulikuwa mwingi.

Lakini ilipokuja Xxl sasa... Dj mmoja watangazaji watatu ni story mwanzo mwisho! East Africa nao vile vile wkt wa Soul train akiwa anapiga DJ Habib hakuwa mtu wa story tena alikuwa anasimama peke yake leo kila uki "tune in" ni story tuuuuu mbaya zaidi unakuta ni story ambazo wala hazijabeba habari ndani yake. Yaani very boring.

Hiyo ni mifano tu lkn hali iko hivyo radio zote.
 
Dj Habib ( H A B I B) aka H Sal. Sijui yuko wapi huyu mtu?
 
Habib nasikia alienda mbele huko na kuna club alikuwa anapiga
 
Hakuna kitu walichoniudhi Clouds FM kama kufuta kipindi cha African Bambataa. Halafu wameweka Jahazi ambacho kina Kibonde wanabwabwaja tu, hakuna la maana wanalotangaza
 
Yaa kiss FM kiss Fm ndio nilichokua nasikia muziki uliopangwa hakuna maneno sasa watangazaji wakipata kazi wanadhani kila kitu wanajua wao ni kuongea tuu,katikati ya muziki wanaongelea mpira wa ulaya..
 
Siku izi hakuna miziki yakupiga, kila nyimbo inayo heat ni rich mavoko, diamond na sijui akina nani hawa ali kiba.

Tena nyimbo zenyewe big G tu. Zaman wacha bana.

Mara J.mo, mara ngwair, mara nature, mara Gk.

top ten sasa usiombe, umemsikia Duly kule zey B mara sisiter P , mara Da Jo, mabaga fresh, gangwe mob, inspector mara dudu baya, est coast, daz nundaz. Mara sugu, prof j, aisee ni wengi. Ila park lane ni muhimu niwataje

Beat nzito za P.majani, master J, kameta, mika mwamba, aisee alale mahala pema marehemu Roy na beat za kijanja, John mahundi.

Yan Dj anapiga nyimbo za kibongo hadi raha, unaruka mzee mpk dah.

Magic, Rfa, PRT, radio one, times , clouds , mzee ilikuwa ku tune tu, ikifika saa 8:30 unachagua tu uende wapi?

Sasa leo miredio ni story tu na kila redio unayofungulia utasema B12 ndie mtangazaji radio zote.

Jaman zaman raha
 
Powerful 4 ilikuwa balaa. Ile ni crew nzima ya bills waliamua kutoka na kuanzisha disco lao "Mambos club" kwa sababu za kimaslahi. Habib, Jd, Rico, G Lover. Nadhani pia ni kweli mziki hauna ladha siku hizi nakumbuka JD aliwahi kukiri hilo pia Master J.
 
Shida ya hawa wasanii wa kisasa ni ubunifu mdogo wanaiga mno,ndio maana si ajabu katikati ya wimbo kusikia kibwagizo cha "kama Ronaldo",Siku hizi wimbo hausifiwi kwa uzuri wake kama wimbo,bali ubora wa video.Jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linaua Muziki ni rushwa.Watangazaji wa radio wanapokea rushwa kwa wasanii wenye uwezo kifedha,ili nyimbo zao zipigwe hata kama ni mbaya.
 
tena hao clouds fm hicho kipindi cha jahazi kiukwer mimi hua skielew kinamaanisha nin manake duh hao jamaa wanavyoviongea humu wakianza kipind mpaka wanamaliza ni kuongea tu hata hawajistukii
 
RFA show time ya kid bway...ilikuwa nzuri..siku hz wanaita show time new chapter
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom