Siku CCM ikifa Tanzania itainuka

Siku CCM ikifa Tanzania itainuka

Nafurahia sasa maana Ule ubishi wa kipumbavu wa ushindani kati ya MAMA na JIWE unayeyuka.

Adui namba MOJA ni CCM, maana ndani yake ndimo kuna magenge ya kiharamia yanayotukwamisha kama NCHI.

Ameeeen.
Wengi hudhani tatizo letu ni watu mmoja mmoja waliomo CCM, kumbe tatizo letu ni uwepo wa CCM yenyewe kwa ujumla wake!!
 
Kwa miaka zaidi ya thelasini CCM imekuwa ikifanya kila iliwezalo kusiwe na chama kingine cha siasa nchini Tanzania. Lakini juhudi hizo za CCM dhidi ya vyama vingine kumbe zilitakiwa zifanywe dhidi ya CCM yenyewe.

CCM ndiyo chama pekee kilichokuwa madarakani tangu Tanganyika ipate Uhuru na Zanzibar ifanye mapinduzi. kwa ivo kila baya unaloliona linatendwa na serikali ya Tanzania jua linatendwa kwa kuwa CCM iko madarakani.

Siku CCM isipokuwa madarakani ndipo Tanzania itainuka kiuchumi, kijamii, kimataifa na kwenye kila kitu kilichokwamishwa na uovu wa CCM.
CCM haiwezi kufa kama Viongozi wa Vyama vya Upinzani wamebaki kujikomba kwa CCM, inakufaje kwa mfano?
 
Ife alafu washike nchi kina nani? Na hata ikifa hakuna chama cha maana kwa sasa chenye maono ya kuweza kuinua hii nchi.

La muhimu si chama kufa bali kupata kiongozi sahihi anayeweza kutengeneza mifumo sahihi kwa nchi or otherwise mtabadili kila chama lkn matokeo yatakuwa ni yale yale

Ccm ni chama hovyo lkn huwez fananisha na hayo magenge ya wanaojiita wanademokrasia ilihali wao wenyewe demokrasia imewashinda ktk vyama vyao

Ombea kupata kiongoz sahihi anayeweza kuja kubadili rangi mbaya ya chama tawala ama kuwaunganisha wananchi wa vyama vyote vya siasa
 
CCM ni chama cha siasa ndio jeshi na ndio usalama wa Tanzania, ilijengwa katika misingi ya kutawala milele kama ilivyo nchi zote za kijamaa.

Mifumo yote nyeti ya nchi ni mali ya chama, wakati wa uhuru 1961, mabepari na wajamaa wote waliigombea hii nchi, JKN akachukua njia ya ujamaa lakini akasahau ujamaa hauna dini na yeye ana dini tena ile ile yawamiliki wa dunia, mabepari aka mabeberu ndio waliombatiza kanisani na dini aliyopo ni mali yao, bwana weeee kazi kwelikweli.

ukielewa hapo endelea mwenyewe kama wewe ni dip thinker.
 
Back
Top Bottom