siku 7 za CHADEMA kwa Nape

kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,727
2,214
Chadema kumfikisha Nape mahakamani wiki hii

Na Restuta James

4th September 2012

nape%281%29.jpg

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeazimia kwenda mahakamani wiki hii kumshtaki Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, baada ya kushindwa kukiomba radhi chama hicho pamoja na kutoa faini ya Shilingi bilioni tatu, baada ya kupita kwa muda aliopewa kufanya hivyo.

Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana, Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Chadema, Anton Komu, alisema chama hicho hivi sasa kinakamilisha taratibu za kisheria ili kwenda mahakamani.

Alisema "wakati wowote wiki hii tutakwenda mahakamani, leo jioni (jana) nitakutana na mawakili ambao wanashughulikia jambo hilo."

Komu alisema imelazimu suala hilo kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa Nape amekataa kuomba radhi kuhusu madai aliyoyatoa.

Chadema ilimtaka Nape aombe radhi baada ya kukituhumu kwamba kimekuwa kikichangisha fedha kwa wananchi katika mikutano yao wakati kinapokea mabilioni ya fedha kutoka nje ya nchi.

Nape alitoa tuhuma hizo Agosti 12 na kueleza kwamba anao ushahidi kuwa chama hicho kimekuwa kikiwahadaa wananchi kwa kuwachangisha fedha huku kikipokea mabilioni ya fedha kwa wafadhili kutoka nje na kwamba upo uwezekano wa chama hicho kupewa fedha hizo kwa mikataba yenye masharti ya kuiweka nchi rehani.

Baada ya kauli hiyo, bodi ya wadhamini wa Chadema iliagiza wanasheria wake wamwandikie Nape barua ya kumtaka kukiomba radhi chama, kwa kutumia vyombo vya habari.

Chadema inataka kuombwa radhi na fidia ya fedha ni kwa ajili ya fedheha na fundisho kwa kitendo cha uzushi na uongo kilichotolewa na Nape.

Nipashe - September 4
 
Hawa wanasiasa siyo wa kuwaamini sana. Huyo Mnyika na Nape kuna siku niliwakuta kwenye mgahawa mmoja hivi katikati ya jiji wakipiga kitu cha juisi ya matikiti huku wakicheeeeeka unaweza kusema ni mtu na shemeji yake. Narudia wanasiasa siyo watu wa kuwasikiliza hata kidogo. Watu wengine bwana.
 
hiyo mbaya mbaya sana
 
Tulia kwanza serikali ijikaange na nape aliyetabiri hizi vurugu za polisi.wana vikao visivyoisha akina nape wakijilaumu picha zilipotoka.
 
Hawa wanasiasa siyo wa kuwaamini sana. Huyo Mnyika na Nape kuna siku niliwakuta kwenye mgahawa mmoja hivi katikati ya jiji wakipiga kitu cha juisi ya matikiti huku wakicheeeeeka unaweza kusema ni mtu na shemeji yake. Narudia wanasiasa siyo watu wa kuwasikiliza hata kidogo. Watu wengine bwana.

Siasa sio uadui
 
Hana jipya huyu mtoa tamko,anapenda sana camera za wahandishi wa habari.
 
Mbona mnaharaka, mambo yanafanyiwa kazi, hivi hamjui kuwa kuna issues za maana na za ghafla zimetokea?
 
1,2,3,4,5,6,7,8,9,10,11,12,13,14,15,16,17,18.....n

n = namba yoyote ambayo ni chanya

kama walisema baada ya siku 7 si usubiri, wangesema siku ya 7 kweli ungekuwa sahihi kudoubt.
 
Hawa wanasiasa siyo wa kuwaamini sana. Huyo Mnyika na Nape kuna siku niliwakuta kwenye mgahawa mmoja hivi katikati ya jiji wakipiga kitu cha juisi ya matikiti huku wakicheeeeeka unaweza kusema ni mtu na shemeji yake. Narudia wanasiasa siyo watu wa kuwasikiliza hata kidogo. Watu wengine bwana.

Ndugu siyo vizuri hata kidogo kujaribu kuonyesha ujinga ulionao kwa watu hasa hasa hadharani kama hapa! Kuwa wapinzani wa siasa si ugomvi!
 
hiyo mbaya mbaya sana

Ndugu zangu.

si vema kuwataka wanasiasa wetu wachukiane, kisa ni upinzani wao wa kivyama.
sasa watawezaje kupeana mawazo mazuri ya kuijenga nchi yetu kama hawatakua marafiki?
 
Hey, jamani,tupo kwenye mambo makubwa yanayohusu uhai wa watanzani,nashauri cdm waweke nguvu kubwa kwenye hili kwanza, wawahakikishie watu usalama, then after, habari za nape zitafanyiwa kazi,hebu tuwe na vipaumbele.

Naamini issue ya nape aliyodai chadema wanajifanyia vurugu,ndiyo utekelezaji wake kupitia pilisccm.kwapamoja tuwaunge mkono viongozi wetu na tusiondoe imani kwao naamini kila kitu kitafanyika kama ilivyopangwa.waombaji waombe for cdm,waswaliji wafanye dua pia.

naamini tutashida vita dhidi ya huu uzalimu wa ccm na polis.

long live cdm
 
CHADEMA wana mambo mengi muhimu ya kufanya kwa sasa kuliko hizi porojo za Nape na Mnyika
 
Mkuu Mnyika heshima mbele sana,

Mnamo tarehe 25 Agost, Ulionekana kwenye TV na hata magazetini ukifanya mkutano na waandishi wa habari na kutoa siku 7, vipi mpango wako umeishia wapi na kama mmeyamaliza mezani huna budi kuita waandishi wa habari na kuufahamisha umma kuwa mmeyamaliza mezani na mahakamani hamtaenda tena laa sivyo credibility itashuka kwa kasi sana.

Nini kilichojili Kiongozi.??
 
Back
Top Bottom