#COVID19 Siku 100 za Rais Samia na janga la Covid-19

chase amante

JF-Expert Member
Feb 24, 2018
5,553
2,073
Habarini za asubuhi wanaJF. Namshukuru mungu kwa kutupa uzima kuiona siku ya leo.

Siku miamoja za rais Samia amejitahidi kuonesha mwanga zaidi, kuhusu namna ya kupambana na ugonjwa wa corona.

Nikiri wazi kua, Tanzania tuna bahati ya kupata viongozi wazuri, wenye maono na wanaoendana na Nyakati sahihi za mabadiliko ya kijamii na kiuchumi duniani.

Janga la ugonjwa wa uviko_19 limeleta madhara makubwa sana ya kiafya, kiuchumi na kijamii. Repoti ya the Global trends 2040 iliyotolewa na baraza la usalama la taifa la intelijensia ya marekani maarufu Kama The US national intelligence council, imekiri wazi kua janga la corona ndio janga pekee lililoweka hali ya usalama, siasa na kijamii katika hatari tangu kutokea kwa vita kuu ya pili ya dunia.

Madhara ya janga hili, yamepelekea nchi nyingi kukumbwa na tofauti nyingi za kiutawala na kusababisha hofu. Mfano huu ni hapa nchini Tanzania, ambapo vyama vya upinzani vimezidi kuishinikiza serikali kufanya mabadiliko ya kiutawala ikiwepo masuala ya Katiba mpya. Haya siyo mabaya, ila ni matokeo ya hali mbaya za kiuchumi, kiusalama, kisiasa na kijamii. Na ndio maana Nampongeza sana mheshimiwa rais samia kwa kutuvusha vyema katika kipindi hichi kigumu kwa kusisitiza umoja na mshikamano.

Nitoe rai kwa vyama vya upinzani na asasi nyingine za kiraia, kumpa ushirikiano rais kwa kuendeleza kuchukua tahadhari za ugonjwa wa corona kwa kufanya mikutano ya ndani ya kisiasa na sio mihadhara na maandamano.

Katika kupambana na uviko_19, mama katumia mbinu za kisayansi ikiwemo kuandaa mpango wa kupata chanjo,na kusisitiza wananchi tujikinge zaidi kwa kuvaa barakoa na kunawa mikono na mbinu nyinginezo nyingi ikiwemo tiba asilia.

ila katika masuala ya afya ya umma, uzoefu unaonyesha kupambana kuanzia ngazi za chini, yaani local initiatives, inasaidia sana kuliko kuanzia na sera za kitaifa na miongozo ya chanjo kwenda chini kwa wananchi (top down policies). Mfano ni katika wimbi La kwanza lililoikumba nchi yetu ambapo, juhudi za kujikinga na kuhudumia wagonjwa wa corona zilianzia ngazi ya chini kabisa ambapo hadi vijijini, watu walipewa elimu na walichukua tahadhari na matokeo yake, tulilishinda sana gonjwa hili ukilinganisha na nchi nyingine.

Natoa rai, kwa mheshimiwa rais kutumia zaidi uzoefu tulioupata kutokana na wimbi la kwanza ambapo, tulitumia zaidi mbinu za kujikinga na elimu zaidi kuanzia ngazi za chini kabisa za kaya na vijiji. Si kwamba chanjo na misaada ya kifedha ya dharula ya kupambana na madhara ya uviko_19 ni mibaya, la hasha ni mojawapo ya hatua nzuri zaidi ya kumaliza kabisa wimbi hili la tatu. Tatizo ni kwamba mbinu hiyo inatuchukua muda mwingi mpaka ilete matokeo kwa nchi Kama yetu , kwani mazingira halisi ya upatikanaji wa hizo chanjo ni mgumu na ni gharama sana.
 
Back
Top Bottom