Nashukuru kwa mawazo yako mema Mkulu!
Ila kuna msemo kwamba sikio la kufa halisikii na nabii hakubaliki kwao!
Kadogo ametoa masharti kwamba Kanisa liombe radhi na ameyataja ya kuyaombea radhi
Nimejiuliza kama kanisa nani aombe radhi Luambano Pengo Malasusa Kilaini Pope Benedicti ima Mtikila
mf;Mtikila alimsema sana Nyerere kuhusu uongozi wake! akamsema Mkapa kwamba hana uchungu na nchi hii kwa sababu ni Mmetu toka msumbiji Kilaini alitamka kwamba Kikwete ni chaguo la Mungu wengi wakapinga hao Wote ni Kanisa kwa mujibu wa kadogoo wote waombe radhi.
Ameshindwa kutenganisha kauli ya mtu binafsi na Kanisa. na hilo ni tatizo
Mf;Kanisa katoliki wana taratibu ya kutoa matamko yao kupitia NYARAKA ZA KICHUNGAJI na wanahimiza matendo mema na kuelekeza kuchagua viongozi waadilifu leo mkichagua kiongozi asiye muadilifu Kanisa Katoliki linahusika vipi?
Suluhisho!;
Waislamu wanaamini kwamba kisasi ni haki lakini Allaah amemshushia Mtume wake(Mohammad Saw) Uvuvio kwamba KUSAMEHE NI BORA!! Kumbe basi kusamehe kama ni bora tufuate kilicho bora ni kauli ya Haki Mungu, Kama mmeona mmeonewa Sameheni!
MSAMAHA NI BORA!
Tuanze mkutano wa katiba inayo kidhi haja ya wote wenye nchi.....
Kalamazoo,
Ni Maaskofu haohao ambao mwaka 2005 walisema JK ni chaguo la Mungu. Kwa nini sasa wamemgeuka hivi? Kwa upande wa elimu wala hauwezi kubisha kwamba Maaskofu wengi (ukiacha akina KAkobe, Mwingira, wa Upako) wamesoma vizuri mno kuliko Masheikh. Masheikh waliosoma vizuri wanajua JK hayuko Ikulu kwa kuwa ni Mwislamu.
Wao wanaamini shida walizonazo zinatokana na wao kuwa waislamu na kutokupewa haki sawa kwa kuwa wao ni waislamu na si kama watanzania as if shida zimegawanyika kutokana na dini au effect za ufisadi zinaenda kwa watu wa dini fulani tu..........
Nilianza kujisikia vibaya but thanks to God kwamba kuna watu wanajaribu kufikiria!Hivi hawa watu ambao kila kukicha wana hoja za kuwagawa wenzao kimafungu(kimakundi) wanatafuta nini hawa? [/B]
Kalamazoo,
Ni Maaskofu haohao ambao mwaka 2005 walisema JK ni chaguo la Mungu. Kwa nini sasa wamemgeuka hivi?
Tena kwenye mdahalo wao wa jana Redio Iman masheikh walisema umefika wakati wa nchi hii kugawanywa pande mbili. Sehemu yenye wakristo wengi iwe yao na ile yenye waislam wengi iwe yao. Wanasema lengo la kufanya hivyo ni kutekeleza azimio la Nyerere alipotaka Nigeria itenge eneo la Biafra kwa ajili ya wakristo wa Nigeria waliokuwa wanateswa na waislam.
[/COLOR]
Wengine wetu hatukufurahishwa na tabia ya maaskofu ya kumtagza mtu kuwa ni chaguo la Mungu.Lakini wao walijua ni kwanini waliamua kufanya hivyo.Kwani nini sasa wamemgeuka? Jibu ni rahisi,walidhani ataendeleza yaleyale ya Nyerere aliyowaahidi wakrsitu kuwa atalipa kanisa fursa maalum(soma kitabu cha Padri John Sivalon cha Siasa za Tz na Kanisa Katoliki). Alipoingia madarakani yeye akajenga nchi ya wote badala ya kujenga kanisa,akaboresha maslahi ya madaktari na manesi hivyo baadhi yao wakaanza kuhama hospitali za kanisa kwenda serikalini,akaanzisha shule za kata zikaonekana ni tishio kwa shule za seminari,akataka kuondoa misamaha ya kodi kwa taasisi za kidni kwani wanazitumia vibaya.Hapo ndo walianza kumchukia lakini wakajificha kwenye kisingizio cha mahakama ya kadhi huku wakijua kuwa hata wakati wanamtangaza chaguo la Mungu kwenye ilani ya uchaguzi kilikuwepo.
Kwa mtazamo wako finyu unadhani kuwa maaskofu wamesoma kuliko mashekh,ni elimu gani unayozungumzia? Muislam hawi sheikh hadi awe amehitimu kiwango fulani cha elimu ya dini ya kiislamu.Kama walivyo maaskofu wengi wenye degree za theolojia pia wako mashekh wengi wenye degree za elimu ya kiislamu,wapo hadi maprofesa na madokta wa elimu ya kiislamu.
Suala sio jk kuwa ikulu kama muislamu suala ni kuona anapigwa vita na maaskofu hadi wameambukiza chuki hata kwa waumini wao kama wewe.Hili waislamu wote wanaliona waliosoma na wasiosoma alike
1) Kanisa liombe radhi kwa Watanzania kwa kufurahia madhambi yote yaliyofanywa na Serikali tangu ya awamu ya kwanza, ya pili, na ya 3! baadhi ya madhambi hayo ni Utawala wa Julius kuwakamata na kuwatia jela viongozi wa dini ya Kiislamu bila ya kuwafikisha mahakamani!
Mfano ni Mufti mkuu wa kwanza Tanzania Sheikh Mohamed Bin Ameir, Rais wa Jumuiya ya EAMWA Tanzania Sheikh Tewa Saidi tewa, Katibu Mkuu wa EAMWA Bibi Titi Mohamed na Julius kuivunja jumuiya hiyo tukufu iliyowaletea maendeleo makubwa Waislamu wa Tanzania na kuwaletea BAKWATA iliyoasisiwa kwa kutumia katiba inayofanana na katiba ya TANU! ndio maana mpaka leo tuna Shehe wa Mkoa, wilaya, kata na kijiji kama ilivyo kwa CCM mwenyekiti wa CCM mkoa, wilaya nk.
2) Kanisa liombe radhi kwa kushirikiana na Serikali ya Nyerere kumpachika Padre ktk Wizara ya Elimu ili asimamie uchakachuaji wa mitihani ya Secondary, high school na hata Chuo kikuu cha Dar, ili kuwachuja wanafunzi walio waislamu na kuwapendelea wakristo!
Mfano mimi mwenyewe nikiwa darasa la 7 jumla ya wanafunzi tulikuwa 30, waislamu walikuwa 17, wakristo 8, na Hindus 5 na kila mtihani kuanzia darasa la 4-7 mitihani yote walikuwa waislamu wakiongoza kuanzia namba 1,2,3,4,5,mpaka 7 lakini cha kusikitisha matokeo ya kuingia Secondary walifaulu wakristo 7, waislamu 2 na baniani 1 kwanini? ina maana hawa waislamu hawakudurusu?
Ukifuatilia ya Secondary mpaka chuo kikuu utakuta mapungufu kama hayo!
3) Kanisa liombe radhi kwa kunyamaza wakati Serikali ya Mwinyi ilipowauwa Waislamu wa zanzibar walipoandamana mwaka 1988 wakipinga kauli ya Mama Sofia kauwawa ya kutaka Qurani ifanyiwe mabadiliko!
4) Kanisa liombe radhi kwa kuishinikiza serikali ya Mkapa kuwakamata Waislamu na kisha kuwauwa ndani ya msikiti wa Mwembechai na kusababisha wengine kuwa walemavu wa maisha mfano ni Mtoto Chiku alimiminiwa risasi kama maji! Rejea kauli ya Paroko Camilius Lwambano
4) Kanisa liombe radhi kwa kubariki mauaji ya Wafuasi wa CUF huko Unguja na Pemba mwaka 2001!
5) Kanisa lisijiingize ktk madai ya Waislamu kwa Serikali kuhusu Mahakama ya Kadhi na OIC!
6) Makanisa hasa ya Kilokole yawache tabia ya kutembelea nyumba wanazoishi waislamu na kugawa Biblia bure kwani Waislamu wakijibu mapigo sidhani kama Kanisa litafurahi!
7) Makanisa ya Kisabato na Kilokole waache tabia ya kuja na magari ya tarumbeta na kuimba kwa sauti kubwa karibu na Misikiti wakati Waislamu wako ktk sala hivyo kusababisha usumbufu na kukosa utulivu ndani ya ibada zao! huo ni uchokozi!!
8) Mwisho na muhimu- Kanisa liwe na tabia ya uvumilivu pale Waislamu wanapohubiri kuwa Yesu si Mungu kwani wao nao huvumilia wakisikia Wakristo wakimuita Yesu kuwa ni Mungu!
Sekondari za KATA ni tishio kwa seminari? Masheikh wengi tulionao mitaani wameupata Usheikh kwa kutoa kiwanja ili msikiti ujengwe. Wengine wameupata Usheikh kwa kukubalika tu na jamii inayowazunguka na busara za kawaida.
Sekondari za KATA ni tishio kwa seminari? Masheikh wengi tulionao mitaani wameupata Usheikh kwa kutoa kiwanja ili msikiti ujengwe. Wengine wameupata Usheikh kwa kukubalika tu na jamii inayowazunguka na busara za kawaida.
Sekondari za KATA ni tishio kwa seminari? Masheikh wengi tulionao mitaani wameupata Usheikh kwa kutoa kiwanja ili msikiti ujengwe. Wengine wameupata Usheikh kwa kukubalika tu na jamii inayowazunguka na busara za kawaida.
Msheikh wameshtuka baada ya kugundua kuwa anapokuwepo muislam ikulu ndo maaskofu hutoa matamko na mawaraka mengi lakaini akiwepo mkristu mwenzao hutasikia kabisa utadhani wamefungwa mdomo au kama vile mambo yamenyooka.Vuta kumbukumbuku utawala wa Nyerere amabapo watu wengi walikufa wakati wa vijiji vya ujamaa,hali mbaya ya uchumi amabapo nchi ilifilisika kabisa hata sabuni ya magwanji au nguo ya mtumba vilikuwa shida kupatikana.Maskofu walisema kitu? Njoo utawala wa Mwinyi nenda kwenye maktaba za makanisa utakuta mawaraka na matamko kibao.Njoo kwa Mkapa ambapo mengi mabaya yalitokea hata watu walikufa kwa njaa lakini maaskofu kimyaaa.Sasa Kikwete ona maaskofu wanavyotoa matamko na mawaraka kibao utadhani nchi inakaribia kuanagamia sasa wanataka kuikoa.Wakao kuwepo wasuburi akija Rais mkiristu utaona kama watafungua mdomo kuikemea serikali.Haya yote ni unafiki wa maaskofu na chuki dhidi ya waislamu.
Ukweli ni kwamba, baada ya mauaji ya raia 23 wasio na hatia yaliyotokea Zanzibar tarehe 26 na 27 Januari mwaka 2001, Maaskofu wakatoliki walitoa Tamko lao tarehe 23 Februari 2001 la kuelezea masikitiko yao juu ya ukatili uliofanywa na jeshi la polisi dhidi ya raia hao, na kuitaka Serikali ya Rais Mkapa wakati ule kufanya uchunguzi na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wote waliohusika.
Baada ya hapo, Maaskofu wa Kanisa katoliki hawakuishia hapo, wakawa mstari wa mbele ili kuhakikisha kwamba matukio ya kusikitisha kama hayo, hayajirudii tena katika nchi hii. Wakashawishi kuundwa kwa jukwaa la Viongozi wa dini mbali mbali kwa ajili ya kushughulikia amani na mazungumzano linalohirikisha wajumbe kutoka BAKWATA, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Jumuiya ya Kikristo Tanzania na Ofisi ya Mufti Zanzaibar. Tangu wakati huo mpaka sasa, Maaskofu Katoliki wamekuwa wakibeba gharama zote za uendeshaji wa Jukwaa hilo ikiwemo mikutano n.k.[
SOURCE !!!!
Mchango Huu nimeudaka kwenye forum ya wanabidii, nadhani unatoa picha ya masuala mengi kuhusiana na mada hii:
Kwa mujibu wa baadhi ya Magazeti, halikuwa Tamko la BAKWATA, ingawa katika Kongamano kulikuwa na baadhi ya Viongozi wa BAKWATA waliotajwa ambao yasemekana walililiunga mkono na kusema kwamba Tamko hili "ni la maana sana na likifanikiwa litaleta faraja kwa Waislamu na wananchi wote" (taz. Tanzania Daima ya jana).
Kimsingi Tamko hilo lilikuwa na mambo mengi ambayo mengi mengine tumeyazoea kuyasikia kutoka kwa Shehe Issa Ponda na Bassaleh. Nisingependa kuyarudia yote yaiyosemwa na viongozi hao lakini ningeomba kuongelea yale yaliyowatofautisha na maaskofu mintarafu vurugu za Arusha. Kwa ufupi wao walitofautiana na Maaskofu kwa kusema kwamba "yaliyotokea Arusha ni mgogoro wa kisiasa kwa hio si busara kwa Maaskofu kusimama mbele ya Chadema" na kuongeza kwamba: "kwa nini Maaskofu walikaa kimya wakati wa mauaji ya Zanzibar na sasa wanapiga kelele juu ya mauaji ya Arusha".
Kwanza sina uhakika kwamba ni kwa kiwango gani tunaweza kusema vurugu za Aurusha ni mgogoro wa kisiasa tu na hivyo Maaskofu hawapaswi kuingilia... Lakini zaidi ya hayo ni kwamba, Tamko hilo lilikuwa na mapungufu ya ukweli wa kihistoria, ama lilitaka kupotosha kwa makusudi umma kwa kusema kwamba Maaskofu walikaa kimya wakati wa mauaji ya Zanzibar.
Ukweli ni kwamba, baada ya mauaji ya raia 23 wasio na hatia yaliyotokea Zanzibar tarehe 26 na 27 Januari mwaka 2001, Maaskofu wakatoliki walitoa Tamko lao tarehe 23 Februari 2001 la kuelezea masikitiko yao juu ya ukatili uliofanywa na jeshi la polisi dhidi ya raia hao, na kuitaka Serikali ya Rais Mkapa wakati ule kufanya uchunguzi na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wote waliohusika.
Baada ya hapo, Maaskofu wa Kanisa katoliki hawakuishia hapo, wakawa mstari wa mbele ili kuhakikisha kwamba matukio ya kusikitisha kama hayo, hayajirudii tena katika nchi hii. Wakashawishi kuundwa kwa jukwaa la Viongozi wa dini mbali mbali kwa ajili ya kushughulikia amani na mazungumzano linalohirikisha wajumbe kutoka BAKWATA, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Jumuiya ya Kikristo Tanzania na Ofisi ya Mufti Zanzaibar. Tangu wakati huo mpaka sasa, Maaskofu Katoliki wamekuwa wakibeba gharama zote za uendeshaji wa Jukwaa hilo ikiwemo mikutano n.k.
Wakati wa uchaguzi uliopita, Jukwaa hilo liliwatembelea viongozi wa vyama mbali mbali na kuwasihi wawaelekeze wafuasi wao kuwa na uvumilivu wa kisiasa wakati w kampeni, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi; na lilifaulu kuwatembelea, Maalim Seif Shariff Hamad, Dr. Slaa, Prof. Lipumba na Mhe. Kikwete. Baada ya kuyasema hayo, naomba niseme kwamba, mshangao wangu ulikuwa mkubwa zaidi niliposoma katika gazeti hilo kwamba kiongozi huyo wa BAKWATA ambaye ni mjumbe wa Jukwaa hilo aliunga mkono Tamko hilo wakati yeye mwenyewe anajua mchango wa viongozi wenzake (Maaskofu) katika ujenzi wa amani na mazungumzano miongoni mwa wanajamii hapa Tanzania.
Amekuwa akishiriki vikao vingi tu na kuonyesha angalau apparently, nia yake ya kutaka kupigania amani na maelewano miongoni mwa Watanzania. Sina uhakika kama aliyasema maneno hayo ambayo magazeti yalimnukuu ama kama alikuwa anaunga mkono yote yaliyokuwemo katika Tamko hilo. Kama kweli aliyatamka hayo, na anaunga mkono yote yaliyo katika Tamko hilo, naanza kupata mashaka mengi juu ya baadhi ya viongozi wa dini kama wana nia ya kutusaidia kujenga na kulinda amani katika nchi hii.
Na moja kwa moja naelekea kupata mawazo kwamba pengine viongozi wengine wa dini wanatumika kwa maslahi ya kisiasa. Na jambo hili, licha ya kuwashushia heshima, ushawishi na mvuto baadhi ya viongozi wa dini mbele ya jamii, ni hatari kwa amani ya nchi yetu!
Source:
fromEdgar Mbegu <embegu@hotmail.com>reply-to wanabidii@googlegroups.com
toWanabidii Mawazo <wanabidii@googlegroups.com>
date18 January 2011 17:11subject RE: [wanabidii] TAMKO LA BAKWATA DSM KUHUSU ARUSHAmailing list <wanabidii.googlegroups.com>
Msheikh wameshtuka baada ya kugundua kuwa anapokuwepo muislam ikulu ndo maaskofu hutoa matamko na mawaraka mengi lakaini akiwepo mkristu mwenzao hutasikia kabisa utadhani wamefungwa mdomo au kama vile mambo yamenyooka.Vuta kumbukumbuku utawala wa Nyerere amabapo watu wengi walikufa wakati wa vijiji vya ujamaa,hali mbaya ya uchumi amabapo nchi ilifilisika kabisa hata sabuni ya magwanji au nguo ya mtumba vilikuwa shida kupatikana.Maskofu walisema kitu? Njoo utawala wa Mwinyi nenda kwenye maktaba za makanisa utakuta mawaraka na matamko kibao.Njoo kwa Mkapa ambapo mengi mabaya yalitokea hata watu walikufa kwa njaa lakini maaskofu kimyaaa.Sasa Kikwete ona maaskofu wanavyotoa matamko na mawaraka kibao utadhani nchi inakaribia kuanagamia sasa wanataka kuikoa.Wakao kuwepo wasuburi akija Rais mkiristu utaona kama watafungua mdomo kuikemea serikali.Haya yote ni unafiki wa maaskofu na chuki dhidi ya waislamu.
Kuna baadhi ya wakristu wantoa kashfa kwa masheikh eti hawana elimu.Hivi kwao elimu ni kujua kusoma kingereza tu? Unawezaje kusema mtu mwenye degree ya Uislam kutoka chuo kikuu kwa mfano cha Al-azhar Misri kuwa hana elimu? Unawezaje kusema kuwa mtu anaeweza kusoma Quran na kuitafsiri kwa kiswahi eti hana elimu?
Nilianza kujisikia vibaya but thanks to God kwamba kuna watu wanajaribu kufikiria!Hivi hawa watu ambao kila kukicha wana hoja za kuwagawa wenzao kimafungu(kimakundi) wanatafuta nini hawa?Kwa nini tusiangalie tu hata swala la wakati,mwamko wa wananchi na mengine kama hayo ambayo yanawezakuwa kuwa yalifanya watu wasiseme at that time?Au ni nani amewahi kusema labda Bosi Mkapa ni msafi kwenye hilo la ufisadi.Lakini hivi na hawa wanaona kuwa hata huyo "mwenzao" hataki huyo bosi agusweguswe? Hivi ni kweli HATUONI KUWA HOJA YA MAASKOFU NA WATANZANIA WOTE NI KWA MASLAHI YA NCHI? Au mimi sifuatilii haya mambo vizuri hivi hata pale Arusha Maaskofu walisema kwa sababu wameuawa wananchi wasio na hatia au kwa sababu aliyeathirika ni Mkristo? Hivi hapakuwa na Mwislamu Pale?......SHAME ON THEM! Ifikie wakati tuanze kufikiria! Au nitoe msimamo binafsi Guys......no offence but naanza kupata wasiwasi na Elimu plus Thinking capacity za baadhi ya ndugu zetu. NA HAWA WA JAMII HIYO WALIOSOMA WAJITOLEE KUWASAIDIA WENZAO KUWASILISHA MAWAZO SAHIHI!
anadhani hawana wajibu katika kuleta amani nchini: angeongeza hii: makanisa yooooooooooooooote, na misikiti yooooooooooooooote iwe sound proof na nyumba yoyote ya ibada isiwe na supika za nje. Mihadhara yoooooooooooooooooooooote na mikutano yooooooooooooooote ya kiroho isiitaje dini nyingine.