n00b
JF-Expert Member
- Apr 10, 2008
- 1,006
- 2,667
[h=2]Taarifa hii ni muhimu sana
Download documents kamili hapa
[/h][h=2][/h]
Tujiulize kuhusu utekelezaji wake. Pia kuna lile suala la taarifa za vifungu vya kasma kutofautiana linapokuja suala la implementation.Taarifa kwa vyombo vya habari, Jumanne, Novemba 29, 2011 Wananchi walioarifiwa Bajeti iliyoarifiwa
Taarifa kuhusu bajeti zilizotolewa hivi karibuni katika tovuti ya Wizara ya Fedha na Uchumi zimesaidia kuwawezesha wananchi kufuatilia mjadala wa bajeti na kuishauri serikali jinsi ya kutatua kero zinazowakabili.
Vitabu vya bajeti ni nyaraka muhimu inayo fafanua jinsi fedha za walipa kodi zinavyotumika katika taasisi mbalimbali za umma. Pamoja na umuhimu wake kwa umma, kwaki pindi cha miaka iliyopita, vilikuwa havitolewi kwa wananchi.
Kwa miaka kadhaa, Sikika pamoja na mashirika mengine ya kijamii kwa pamoja tumekuwa tukitoa rai kwa serikali kuchapisha vitabu vya bajeti hususan katika toleo la lugha rahisi na kuviweka kwenye tovuti.Wizaraya Fedha na Uchumi imeitikia rai yetu na kuweka matoleo ya
Lugha rahisi ya kitabu cha pili, cha tatu na cha nne katikat ovuti yake www.mof.go.tzhttp://www.mof.go.tz
Sikika inahimiza wananchi wote kutembelea tovuti ya Wizara ya Fedha na Uchumi na kutumia fursa hii kutafakari kuhusu maswali yafuatayo:
- Je, serikali imeweka kipaumbele katika elimu na afya?
- Je, kiasi gani cha fedha kimeelekezwa katika serikali za mitaa?
- Je,kuna mgawanyo sahihi warasilimali za umma?
Bajeti itakuwa na msaada kw awananchi pale tu itakapolenga kutatua kero na mahitaji yanayotoka kwa wananchi. Hivyo, Sikika inatoa rai kwa wananchi, kuhakikisha sauti zao zinasikika kwa kuwaagiza wawakilishi na wabunge wao kuhakikisha yafuatayo yanazingatiwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2012/13:
- Bajeti ina akisi lengo la kutokomeza ujinga na maradhi, kwa
- Kuwawezesha watoa huduma ili waweze kutoa huduma bora, na kwamba
- Rasilimali zilizopo zinagawanywa kwa usawa.
Sikika inakumbusha serikali na wabunge kusikiliza na kuzingatia kwa umakini maoni ya wananchi kwa kuwa wanawajibika kwao na pia wananchi wana kauli ya mwisho katika sanduku la kura.
Ili kuifanya bajeti ya 2012/13 ya wananchi zaidi, serikali inapaswa kukumbuka kuweka taarifa mpya za kibajeti katika tovuti siku 21 kabla ya kuanza kwa bunge lijalo la bajeti. Kwa kufanya hivyo wananchi na wabunge watakuwa na muda wa kutosha kutoa ushauri katika maeneo mbalimbali na ushauri wao kuwafanyiwa kazi ndani ya muda sahihi.
Bw. Irenei Kiria[/h][h=2]
MkurugenziMtendaji, Sikika, S. L. P 12183 Dar es Salaam,
Simu: +255 222 666355/57, Nukushi: 2668015, Baruapepe: info@sikika.or.tz, Tovuti: www.sikika.or.tz
Download documents kamili hapa
[/h][h=2][/h]