Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 948
- 806
Kama unamsikiliza mtu kupata taarifa zinazokusaidia kujibu maswali tuliyozoea— ‘nini’, ‘wapi’, ‘nani’, ‘lini’, bado hujamsikiliza vizuri. Unaweza kujibu maswali hayo yote na usimuelewe mtu.
Ukimsikiliza mtu vizuri, kwa kawaida, unaelewa hisia nyuma ya taarifa anazokupa na hata zile asizoweza kukupa. Unagundua ‘kwa nini’ anasema, ‘kwa nini’ hawezi kusema, ‘kwa nini’ anakuambia wewe, ‘kwa nini’ hicho unachokisikia kina maana kwake, ‘kwa nini’ ni muhimu aseme kwa namna anavyosema na kadhalika na kadhalika.
Usiposikia hisia nyuma ya maneno au kimya cha mtu bado hujamsikiliza. Mawasiliano, kwa kawaida, huchimba kuelewa hisia zisizosemwa wazi wazi—matumaini, matarajio, masikitiko, maumivu, mahitaji yasiyofikiwa, hasira isiyozungumzwa, upweke usiozungumzika na mengine yanayohitaji uende zaidi ya facts— ‘nini’, ‘wapi’, ‘nani’, ‘lini’.