Sijui tumemkosea nini jirani yetu

Kama mnafuga mbwa basi atakuwa ana hamu ya kutoa-mbwa bandani mruhusu.
 
Wewe ni kibonde kiasi hicho? Una moyo mkubwa kama wa tembo yote hayo umefanyiwa ukayavumilia? Grow up! be a man kabla hajakudhalilisha siku moja atakukata vibao mbele ya mkeo na watoto wako!
Mi mwanamke
 

Huna nyumba ila una fence kwani umegeuka mfugo?
 
Ndio maana alikuwa anakuwekea mipaka usizoeane na Majirani zako, sababu anajua fika ukizoeana nao (hao majirani) watakuambia ukweli kuwa yeye ni Kigagula
 
Hakuna kazi ngumu kama kuridhisha mtu, endeleeni na maisha yenu.
 
Atakuwa ni mchawi huyo jirani hivyo amegundua kuwa wewe na familia yako kuwa ni wachawi. Anachojifanya saizi ni kutaka kujua nani zaidi kati ya wewe na yeye ndo mana ameanza na hao paka wako wa kuchawi. Anapowakata miguu anataka aone kama utawapachikia miguu ya bondia ya kichawi. Kwani wewe paka wote hao tena weusi ni wa nini?
 
Utawezaje kuishi unaongea na mtu mmoja mtaani, coz yeye amegombana na karibia majiran wote, na ss ndo tunapakana nae kabisa,pia sisi hatujui ugomvi wao umeanzia wap, utaanzaje kuacha kuongea na mtu kwa sababu ya ugomvi usikuhusu na wala hauujui??

Hapo sasa,na jirani atakupangiaje maisha yako? Kama una uwezo weka fence,hata ya mabanzi kama alivyoshauri mdau hapo juu. Vitimbwi vikizidi mtokee tu na panga maana hamna namna nyingine.
 
Unapata wapi muda wa kuongeaongea na wapuuzi..fanya hivi ukitoka kazini nenda bar kapige tungi hadi giza liingie rudi nyumbani au kama ni mlokole kaa kwako jisomee vitabu vitakatifu huku ukinywa mirinda nyeusi..waepuke wapuuzi kama hao
 
ndio maana mie simwelewi na ninamshangaa Obama na sera yake ya kudhiiti silaha kuna mijtu kama huu inahitaji kununuliwa
hii kitu


 
hadi mda huu huyo jirani yako bado yupo hai?
 
Anawachukulia kwamba nyie ni watu waoga na dhaifu sana! Mtafutie vijana wa nguvu wamcharaze bakora za kutosha kama onyo!
 
Huyo dawa yake ni sala

Na msali sana amejaa nguvu za giza anaowaohopa lazima wana nguvu za Mungu.

Na lazima anawatenda mengine hamyajui. Salini sana tena sana mtaona atakavyowakimbia na kuacha kuwasumbua.
 
Jirani wa namna hio ni kumtupia jini mahaba tu.
Andaa mikwanja nikurushie kwa simu..
Hatakuwa na muda na wewe tena.
Manake ndombolo ya solo 24/7.

Bado Unamuacha akuimbie na taarabu?

Teh teh teh.

Au huyo Matola nini?
Manake hizo ndio tabia zake huyo mtoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…