Sijui nina mkosi

Sijui nina mkosi

Kama inawezekana kwa mganga,kwanini hyo usaili asiende mwenyewe mganga?
 
Mkuu pole sana ndo maisha!!
Nilikua na tabia ya ku-note kila application...
Now nilishaacha kabisa
 
Habar wana JF yaaani nimefanya interview tatu na zoote nimekosa kazi yani itabidi niende kwa mganga aise muda mwingine najihisi nina mkosi
Dogo kuzaliwa ukiwa maskini ni kawaida na liko nje ya uwezo wako lakini kufa ukiwa maskini ni juu yako ...think twice and never say never keep trying u will get it. belive youself go and get job>>>:cool2:
 
Habar wana JF yaaani nimefanya interview tatu na zoote nimekosa kazi yani itabidi niende kwa mganga aise muda mwingine najihisi nina mkosi
Pole,wewe umefanya interview kuna watu hawajawahi kuitwa hata interview so usijisikie vibaya.
Je nataka nikuulize Jua huchomoza mashariki na kuzama magharibi,hii ni universal law,je kwako kuna universal law inayosema "wewe ukiitwa interview ni lazima upate kazi"?jibu najua hakuna,so kwa nini uumie wakati kuitwa interview haimanishi umehakikishiwa kazi?
"Pia nataka ujijuze kwamba mudamwingi kinachituumiza wanadamu si yale yanayotutokea maishani mwetu ila ni jinsi tunavyoyatafasiri matukio hayo."
Wewe umeenda interview umekosa kazi umeamua mwenyewe kutafasiri kitendo hicho kama ni mkosi,nani alikuambia kukosa kazi ni mkosi?Je kama Mungu amekuepusha na baya kwenye kazi hiyo na kuna nyingine nzuri ipo just around the corner utajisikiaje?
Nilichojifunza hapa Jf ni kwamba watafuta kazi wengi kun ufahamu fulani au technique za kuatafuta kazi na mambo ya interview hawajui.Kwa mfano,hizo interview ulizoenda ukakosa kazi ,je ulijaribu kuwafuata hao waliokufanyia interview ukawambia ni kweli umekosa kazi ila unawaomba wakusaidie ni nini ulipungukiwa au ni maswali gani hukuyajibu vizuri ili next interview uyafanye vizuri incase yataulizwa?najua hukufanya hivyo,what if huwa kuna swali unaulizwa kila interview na umekuwa ukichemka na haujui kama unachemka?
Mganga ni mwadamu kama wewe na "amelaniwa amtegemeaye mwanadamu" mwombe Mungu akusaidie,sasa kwa mfano ukienda kwa mganga then ukapata kazi utasema umepata kazi kwa sababu umequalify au nguvu za giza?Vipi washikaji wakikuuliza ulipataje hiyo kazi?Utawambaia ulienda kwa "kalumnzila"?
"If you lose something do not lose the lesson and count your blessings,unapoitwa interview maana yake unaqualify for that job,lakini pia kumbuka interview si kipimo kamili cha ufahamu wa mtu.Ukifail interview wanakuona hufai kumbe waliyouliza siku hiyo kidogo umepishana nao.
Kumbuka siku hizi kazi nyingi ni "know who" na si "know how" namanisha "undugunization umetawala"
 
Back
Top Bottom