Sijui nimfanyeje huyu rafiki yangu

Sijui nimfanyeje huyu rafiki yangu

dikembe

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2012
Posts
1,645
Reaction score
1,439
Hi, you guys..namaste...
Tuanzie hapa,

Mie naishi Dar es Salaam, niko single. Lakini kwa sasa nipo nje ya nchi kikazi.

Toka nitoke Tanzania ni karibu miezi saba sasa. Kipindi nipo Tz nlikua na marafiki but wote walikua watu wazima namaana wamenizidi sana umri, mimi nina 30 but all wana 45 plus.

Hii nilifanya kusudi kutokana na kutoamini urafiki wa vijana wenzangu kwani nliamini umejaa vishawishi na upotoshanaji tu. Na nliamini ntajifunza kutoka kwa hao marafiki wtu wazuma walipokosea mie nisipapite.

So..Nlikua na girl friend ambaye alikua anakuja kwangu most of the wekend time.

Huyu rafiki yangu ambaye aliwahi kufanya kazi kwenye mashirika ya dini alikua karibu na mimi na alinishauri nisiachane na huyu binti kwani alionekana ni mtulivu.

Basi time nachomoka TZ nlimuachia rafiki funguo za nyumba yangu because ni jirani yangu na pia funguo za gari langu, kiufupi ni mtu niliekua namwamini saana. Baada ya muda kupita akaanza kunidis appoint kwa kumiss use gari langu, then nkaamua aliuze ili nkirudi TZ ninunue lingine. Ikawa solved.

Yule binti akawa anaenda kwangu kwa ajili ya kufanya usafi kila mwisho wa mwezi, but kama miezi miwili iliyopita akakuta mipira ya kiume iliyotumika chumbani kwangu, means kuna mtu amefanya mapenzi chumbani kwangu, that friend akamwambia ni mgeni wake ndio alilala huko so mgeni ndio atakua amefanya uchafu huo, demu akanambia but sikuona kama ni issue nkachukulia poa.
Sakata likaanza, juzi wakati wa Valentine rafiki akamwomba binti watoke out, binti hakumpa jibu but alinifahamisha mimi nkamwambia haina tatizo labda ni kwa wema tu, mchana wa siku ya valentine jamaa akamtumia binti hela kwa mobile money, binti akanitaarifu. Then kengele ya hatari ikalia kichwani kwangu but sikumwambia binti lolote.

Usiku wa valentine, jamaa akamwita binti kwenye majira ya saa nne usiku, binti akaninipigi na kuweka simu hewani, nkamsikia jamaa. Jamaa akampabinti hela nyingi tu, then akamwambia achukue usafiri amfuate Mahali kwa ajili ya Dina, Binti akarudi kwao, nkamwambia aende yeye akakataa...asubuh ya pili baada ya valentine akakuta sms za rafiki akilaumu kwanini hajaenda.

Note that, Jamaa familia yake iko mkoa ana mke na watoto na binti ana age 21yrs...
So, nifanyeje wa JF?
 
aisee wewe humpendi huyo binti mbona kama unataka rafiki yako amfanyie mambo mabaya? au unamtafutia hoja?
 
Naona umemkabidhi fisi bucha sio...🙂

Sio hivyo, jamaa ni mtu wa dini vibaya, so sikua naamini kama kweli ana nia mbaya na huyo binti..Nlikasirika sana but sikumwambia kitu. mpaka sas nawaza jinsi ya kumfanya?
 
aisee wewe humpendi huyo binti mbona kama unataka rafiki yako amfanyie mambo mabaya? au unamtafutia hoja?
Binti nampenda, ila sikutegemea kama hata huyu mzee ambaye ana 50yrs na huwa namsaidia kiuchumi mambo mengi anaweza kuwa msaliti?
 
Sio hivyo, jamaa ni mtu wa dini vibaya, so sikua naamini kama kweli ana nia mbaya na huyo binti..Nlikasirika sana but sikumwambia kitu. mpaka sas nawaza jinsi ya kumfanya?
kaka pole but usimwamini mtu kisa dini moyo wa mtu ni kiza kinene sana watu wengi hutumia dini kama kivuli but matendo ni jehanam tupu mtu ka huyo anaitwa ma.la.ya mpole.
 
kaka pole but usimwamini mtu kisa dini moyo wa mtu ni kiza kinene sana watu wengi hutumia dini kama kivuli but matendo ni jehanam tupu mtu ka huyo anaitwa ma.la.ya mpole.
Your very true bro, Hapa ninapoandika hii post kwenye akaunti yake ana hela zangu nyingi tu kwa ajili ya kazi fulani,
Nadhani nsimwambie kitu mpaka amalize hiyo kazi kwani kama miezi miwili ijayo ntarudi tz kwa mapumziko, nadhani utakua wakati muafaka wa kufanya maamuz
 
mi naona funguo ungewaachia nduguzo
Dsm niko peke yangu, na wakati naondoka nlikua bize sana. sikuweza hata kwenda kuaga home kwa wazee. Home kwetu ni mkoani. But mie naishi DSM.
 
Sio hivyo, jamaa ni mtu wa dini vibaya, so sikua naamini kama kweli ana nia mbaya na huyo binti..Nlikasirika sana but sikumwambia kitu. mpaka sas nawaza jinsi ya kumfanya?

Trust nobody bro. Hata wenye dini wanamihemiko ya kimwili na taamaa za mapenzi mtu wangu.
 
Utamwambiaje mwanaume mwenzako atoke na mpenzi wako??

Hukudhania kama kuna jambo lolote baya lingeweza kufanyika?

Mtu kuwa mwenye dini haina maana kuwa hawezi patwa na vishawishi,

Huyo Demu wako atakuwa amekushangaa sana wewe ni mtu wa aina gani,
Au ulikuwa unatafuta sababu ya kumwacha??
 
dah,kwanza pole mkaka!!..pili nataka nikuulize swali,huo ufunguo wa nyumba na gari kwann usingemuachia huyo binti?!,au umwamini?!,pia imani ya dini ya mtu anayokuonyesha isikufanye ukamwamin kupindukia.
 
Your very true bro, Hapa ninapoandika hii post kwenye akaunti yake ana hela zangu nyingi tu kwa ajili ya kazi fulani, Nadhani nsimwambie kitu mpaka amalize hiyo kazi kwani kama miezi miwili ijayo ntarudi tz kwa mapumziko, nadhani utakua wakati muafaka wa kufanya maamuz
duh!mpaka hela umempa aisee usirudie tena kufanya hvyo mkuu sorry umeniita bro mi ni "ke"
 
Hua nakumbuka maneno yake..hupenda kusema hivii( usijali broo..., haina tatizo broo, thanks broo, God bless you broo.....)
 
Sio hivyo, jamaa ni mtu wa dini vibaya, so sikua naamini kama kweli ana nia mbaya na huyo binti..Nlikasirika sana but sikumwambia kitu. mpaka sas nawaza jinsi ya kumfanya?

Inawezekana kabisa ..nimefanya kosa kumwamini huyu kiumbe msaliti

Mkuu sijui ni usasa au ni utu wema sana, najaribu tu kufikiria unaanzia wapi kumkabidhi mpenzi kwa rafiki eti akuangalizie...

Ina maana huyo binti si mtu mzima awezaye kufanya maamuzi binafsi au?

Halafu wenzako waendao ughaibuni kitu kama funguo ya nyumba unaiacha nyumbani, unamuachia nduguyo yoyote kama ni kaka au dada.
 
Hua nakumbuka maneno yake..hupenda kusema hivii( usijali broo..., haina tatizo broo, thanks broo, God bless you broo.....)
hayo ni maneno tu hata kwenye cake yapo mi nadhani mpige marufuku GF wako kua karibu na kizee huyo pili usimwambie chochote coz kumbuka ana hela zako huyo mtu n ukirudi hakikisha unachukua kila kinachokuhusu toka kwa hicho kibabu kwani huko kijijini kwenu hakuna mtu umlete akuangalizie room yako?
 
Thanks,
Kuhusu funguo, nliogopa kumwachia sababu hakua mchumba officialy so when ndugu yangu akija dsm wakati sipo akute Binti ndio anafunguo ingeleta picha mbaya kidogo, hiyo ni kutokana na maisha yangu ninayoishi na ndugu zangu.
 
Binti nampenda, ila sikutegemea kama hata huyu mzee ambaye ana 50yrs na huwa namsaidia kiuchumi mambo mengi anaweza kuwa msaliti?

Then how come ume smel ktu then unamtel aende naye dina??
 
Back
Top Bottom