Sijui nifanyeje wanajukwaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sijui nifanyeje wanajukwaa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by great 2012, Jul 9, 2012.

 1. g

  great 2012 Member

  #1
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilikuwa na mpenzi ambaye tulianza uhusiano mnamo mwaka 2010 kipindi hicho yeye alikuwa anasoma lakini wakaja wakakosana na wazazi wake hivyo akawa ni mtu wa kutanga tanga, mimi nikaona sio vizuri aendelee kuhangaika so nikachukua jukumu la kumsaidia kwa kumsomesha huku nikiwa na matumaini kwamba siku moja Mungu akijalia atakuja kuwa mke wangu,nilimlipia school fees tsh 600,000/= na kila wiki nilikuwa nampatia elfu 40,000/= ya matumizi lakini siku zilivyozidi kwenda mbele nikaja kugundua kuwa kumbe alikikuwa hasomi wala shule alikuw haendi, nilipo muuliza akakataa kata kata.

  So mimi nikaona huyu mwanamke hanifai nikaamua kumwambia ukweli kuwa mimi na yeye basi lkn akaendelea kuning'ang'ania na kunitishia kuwa endapo nitamuacha ataniua, mimi nikaamua kutafuata mpenzi mwingine ambaye nilimpeleka kwa wazazi wangu, na wote walimfurahia na ndipo tukaanza process zote za kutoa mahali, hadi ninavyoandika post hii tayari vikao vya ndoa vimeshaanza na ndoa itafungwa mwezi ujao, cha kushangaza yule mwanamke wangu wa kwanza alipopata habari za mimi kuoa alinijia juu na kuniambia kuwa ana ujauzito wangu na tayari ameshawaambia wazazi wangu, na anapanga kupinga ndoa kanisani. JAMANI HAPA NILIPO MWENZENU NIMECHANGANYIKIWA HATA SIJUI NIFANYEJE?
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,231
  Trophy Points: 280
  wala usijitie presha, kuwa na ujauzito wako (ambao haijulikani kama ni wako kweli au la) hakuwezi kuzuia ndoa yako, kinachoweza kuzuia ndoa kanisani ni cheti cha ndoa pekee........

  ilimradi hukumuoa basi hana kigezo cha kuzuia ndoa.....
   
 3. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ..Pole sana. Endelea na mipango yako ya kuoa, muite huyo mpenzi wako wa zamani mkalishe na marafiki zako au watu wazima na mumueleze aache utoto, akuache uendelee na mipango yako kwa vile mlishaachana. Kuhusu kuzuia ndoa kanisani hilo haliwezekani kwa sababu kanisa litawakutanisha nyote wawili kujua ukweli, kuhusu Ujauzito wewe pia hili utapaswa ulifahamu ni lini ulikutana nae kimwili ukizingatia lini mliachana. Ni vizuri Huyu mchumba wako wa sasa umueleze ukweli kuhusu mahusiano yako yaliyopita na huyo wa zamani ili ajue incase of anything to happen.
   
 4. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Sijui ni kwa nini wanaume wanaendelea kuangukia kwenye huu mtego wa kusomesha mabinti kwa mategemeo ya kuja kuwaoa??? Hivi wapo waliofanikiwa kuwaoa mabinti waliowasomesha??
   
 5. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,681
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 160
  Let me get this straight...Kama ana ujauzito wako na wewe hukujua ina maana ulilala na huyo mwanamke within 9moths ago...probably less tuchukulie average ni 5months ago. Ulianza uhusiano na mkeo mtarajiwa baada ya kuachana na huyo mwanamke...so mkuu ndani ya 5months ulishamwona, ukampenda, ukamtongoza, ukakuza uhusiano, ukaengage, mkatambulishana nyumbani pande mbili, ukalipa mahari, ukaandikisha ndoa na sasa mipango ya harusi yenyewe? Mbona ndoa za siku hizi zina kazi!
  Kama si hivyo basi ulicheat...
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,231
  Trophy Points: 280
  waliofanikiwa wapo, ila wachache, haswa kama alikuwa na msichana then baada ya matatizo kutokea akamsomesha, lakini ukikutana na msichana na shida zake za elimu ukamsomesha akimaliza ujue imekula kwako. ingawa ukisikiliza maelezo ya mtoa mada inaonyesha huyo msichana ana allergy na shule, ndo maana wazazi wake walikataa mkumsomesha, walishagundua ni hasara tupu, halafua anampa msichana 40,000 kila wiki loh....




   
 7. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #7
  Jul 9, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mara ya mwisho wewe kulala nae ni lini, halafu piga calculation either unasingiziwa au utakuwa umemcheat pia mchumba wako. Sidhani kama atapendezewa kujua kama wakati mko kwenye mikakati ya kujulisha family wewe unachobeka mimba!
   
 8. kapistrano

  kapistrano JF-Expert Member

  #8
  Jul 9, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,204
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  mkuu huyo binti ni ya mkosaji hivyo anajaribu kutafuta vikwazo ambavo havina msingi wowote na kanisani wanavigezo vya kusitisha ndoa lkn si kama anavyovileta yeye.
   
 9. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #9
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Hakuna hata mmoja; yupo jaama yangu kasomesha zaidi ya wanne lakini hadi leo ni bachela over 48 yrs sasa!
   
 10. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #10
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Kamdai cheti cha chuo alikokuwa akisoma, akikikosa mwambie kuwa sina muda wa kuwa na mwanamke mwongo. Most of women r of that type.
  HATA KWETU WAPO.
  Usitishike hata kidogo, hizo ni kelele za chura ......
   
 11. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #11
  Jul 9, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mapenzi kaka
   
 12. Jimjuls

  Jimjuls JF-Expert Member

  #12
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 461
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mbona kazi ndogo hiyo....huyo mwanamke wa zamani asijekujiingiza akakuharibia ndoa yako unayotarajia.we mkalishe kikao na wazee na uwaeleze ukweli kwamba ulimsaidiaga zamani na baada ya kutokuona hana mwelwkeo ukamtema.Na hakikisha hiyo mimba siyo yako kweli...kazi ndogo sana.Na pia utoe taarifa kwa baba paroko mapema, huyo mwanamke asije kujidai kwamba yeye ndio yeye.Kwa kweli hata Mungu aliona kwamba ulikwisha msaidia...so you palyed your part!Go ahead with your new wife.
   
 13. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #13
  Jul 9, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hapo atapinga nini wakati hana cheti cha ndoa na wewe. Kwa hiyo hana ushahidi wowote
   
 14. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #14
  Jul 9, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Smile, nadhani kuna haja wanaume waelewe kwamba wanawake ni kwa mapenzi, hata ndani ya ndoa, mapenzi yanatakiwa kuchukua zaidi ya asilimia tisini. ukianza kubland mambo mengine unaharibu kabisa, binaadamu anakiu kubwa sana ya mapenzi.

  shule ni kazi ya wazazi jamani, kwani mwanamke ambaye hajaenda shule anatofauti gani na aliyekwenda shule?? na kama shule ni issue mbuna huwa hatureview certificate zao kabla roho zetu hazijawadondokea???
   
 15. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #15
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  \
  Nimeipenda hiyo red coloured
   
 16. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #16
  Jul 9, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,748
  Likes Received: 12,842
  Trophy Points: 280
  Fanya maamuzi magumu!
   
 17. N

  NALO LITAPITA JF-Expert Member

  #17
  Jul 9, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 294
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  HONGERA SANA BROO,NI WATU WACHACHE SANA WENYE UWEZO WA KUONA NA KUCHUKUA HATUA MAANA WENGINE HUKAA NA KULILIA MUDA NA GHARAMA WALIZOTUMIA. huyo si mke ikiwa leo anakwambia ukikataa atakuua vipi akiletwa ndani. Ndoa haipingwi kirahisi hivyo tena hata kama ujauzito ungekuwa wako sheria haikufungi wewe kuoa ila tu ungelazimika kumtunza mwanao
   
 18. g

  great 2012 Member

  #18
  Jul 10, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asanteni sana wanajukwaa kwa ushauri wenu mlionipa na Mungu awabariki sana
   
 19. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #19
  Jul 10, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,984
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  Pet cash umewaza kama mimi lakin pia ngoja nimtetee huyu kaka yawezekana kabisa, huyu binti kapata ujauzito nje na anataka amsingizie tu huyu bwana. miye ningemshauri kama imeshapita miez sita toka waachane basi akonside kuwa hiy mimba siyo yake na ukweli ni kwamba mimmba si jiwe useme itadumu humo tumboni. atulie mtoto azaliwe tu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #20
  Jul 10, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  kakuona mpole ndio maana analeta hata vituko vyake,muwekee uso wa mbuzi:baby:
   
Loading...