Sijui maana ya dili lakini hali ni mbaya

Sijui maana ya dili lakini hali ni mbaya

tuliambiwa walioishi kama malaika wataishi kama mashetani, tukacheeeka tukidhani kuna kundi fulani la malaika ndo wataishi hvyo.
tulisahau nchi yetu asilimia kubwa tunategemeana sisi kwa sisi siyo raia kwa serikali.

sasa wale malaika kweli wamebanwa lakin kumbe hao hao malaika walikuwa hawali peke yao, wao ndo walikuwa wanatoa dili ntaani, vijana wengi walikuwa wanajipatia kula yao kupitia hao malaika kwa kazi mbali mbali sababu siyo wote waliweza ajiriwa na serikali. sasa kinachotokea malaika wameshuka kiwango kidogo, ila wale wachini ndo wamekuwa mizimu kabisa. kilichopo mtaani ni kufarijiana tu kwamba pesa ipo ila ki uhalisia hali tata
 
Kweli hali ni mbaya mi nna madeni lukuki na kazini kulipwa magumashi,nlitaka nifungue business ndogo tra wakanitolea macho kodi nimeshindwa,kiufupi serikali ya Pombe Magufuli imekuja kuaharibu maisha ya watu
 
Kwani wewe kakutaja au ashuo tu?
Kuna mtu katajwa specifically na mleta uzi? Mimi nimejibu hoja number3 inayouliza nani anamaisha mazuri sasa wakati Hali ni mbaya. Sio kila mtu ana Hali mbaya wengine tupo poa kabisa.
 
Kuna mtu katajwa specifically na mleta uzi? Mimi nimejibu hoja number3 inayouliza nani anamaisha mazuri sasa wakati Hali ni mbaya. Sio kila mtu ana Hali mbaya wengine tupo poa kabisa.

Hongera ngoja nije pm tuyajenge
 
Nimebaini ww ni mke wa ndg John Chiman, hutojua kitu ktk hili ila naamini jamaa ana msalaba mzito sana
KAMA ni mke wa jon basi hana mamlaka ya kuchangia mihangaiko ya wanaume...amwambie mumewe aje kwenye kikao cha wanaume wenzake.
 
Nimeanza kazi 2014, mshahara afadhali, Sina familia, increment ipo, madanga ya kumwaga teh...maisha mazuri.
2015 nimeongeza familia, katoto, kuna gharama za msichana wa kazi, bili za Maziwa, kodi ya nyumba imeongezeka n.k. halafu no increment, bodi hata walikotokea wakachukua 15%, mishe nyingine haziendi.
Hayo yote yakitokea huku sukari kilo 2700, unga 2000. Mshahara umezidi kupungua bora ungebaki palepale
Mbaya zaidi hawataki kufungulia uhamisho nimfate mume wangu tuisome namba kwa pamoja labda tutaelewa mapema.

Hapo nikilalamika maisha magumu naitwa mpiga dili
Wewe ni mpiga dili tuu....vip bado unapokea madanga hasa ukichukulia baby dad yupo mbali anasoma namba kivyake.
 
Kuna jirani yangu alikuwa na biashara zake nzuri kweli na mwanachama nguli. Kila mtu anapopita dukani kwake ilikuwa ni mahubiri ya sera utafikiri paroko. Ghafula kalisika mpk kuhama mji. Akija mara moja ukimkumbusha tu anaporomosha matusi kama mwendawazimu
 
Nikweli maisha ni magumu kipindi hiki ila watanzania tunaishi maisha ya kukariri hatupendi sana kubadilika. Unakuta mtu anabiashara inamnyonya tu haoni faida lakini bado anaikopea anateseka kurudisha mikopo kwa mfumo huo huwezi ona hela usione aibu kufunga biashara nakwenda kufanya kitu kingine kitakachokupa faida..naamin kesho itakuwa bora kuliko kesho ..chakula kinaanza kuvunwa baadhi ya sehemu Arusha unga sasa ni 1200-1300 kwa kilo moja so tuweni nadesturi yakuiona kesho kimaono hivyo vitu vikishuka bei nunueni wekeni akiba...ili tusirudi tena huko...
 
Wewe ni mpiga dili tuu....vip bado unapokea madanga hasa ukichukulia baby dad yupo mbali anasoma namba kivyake.

Dah haya bwana, kudanga nimeacha kabisaa, nimeolewaaa, halafu nilikuwa nachuna tu wanaojipendekeza, siku hizi mke wa mtu sitaki utani, yaliyotokea Mwanza juzi si umesikia? Michepuko inaua nalea.
 
Back
Top Bottom