Sijui maana ya dili lakini hali ni mbaya

babake nasreen

JF-Expert Member
Oct 30, 2014
702
490
Wana forum habari za leo tena..

Kuna usemi siku hizi kuwa wanalalamika maisha magumu ni wale waliokuwa wapiga dili na sasa hv hizo njia zao za dili zimebanwa ndio maana wanalalamika.

Nina maswali haya yananiumiza kichwa:-

1. Nini maana ya hyo dili inayomaanishwa hapa tanzania?

2. Hivi hiyo kitu inayoitwa dili ni kitu haramu?

3. Nje ya wanasiasa je kuna mtu mwenye maisha ya unafuu kwa sasa?

4. Je, nchi za wenzetu hawapigi hicho kitu kinachoitwa dili? Maana kuna ndg na jamaa wapo nchi tofauti duniani wanazidi kuwa na neema na wanafurahi maisha yao kuzidi kuimarika na wakisifia hali ni nzuri zaidi, lkn hapa kwetu hali inazidi kuwa mbaya loo.

5. Kuna baadhi ya watu wanasema hali shwari tuu na nikiwaona hali zao ni bora na mimi cjajua wanafarijika na nini mpk kusema mambo yako shwari huku naona wanazidi kuwa na hali duni.

Mwisho wa yote jamani mimi cjui hicho kitu kinachoitwa dili lkn hali ya maisha imebadilika sana sijui nyie wenzangu mnaonaje lkn hakuna pakutokea, maana hela unayopata hauwezi ukaitumia ktk mambo mengine ya maendeleo zaidi ya kula na bado haitoshi vilevile.
 
Kwani ni lini labda utueleze ulikua na maisha ya raha na ulikua unajishughulisha na nini ili kupata riziki. Sasa hivi pia unajishughulisha na nini?
Pia unaishughulisha akili yako kwa kiasi gani pamoja na nguvu zako ili kutumia rasilimali zinazokuzunguka uweze kujikwamua na hali ngumu?

Maana ya dili katika muktadha huu ..ni shughuli ya ujanja isiyo halali, ya kitapeli au wizi inayoleta kipato kisicho halali.
 
Daaah umenena maisha yamekuwa mwiba sana,Yamekuwa magumu sana lakini kuna mjinga fulani anakupinga na kujifanya yeye hayajui haya pumbavu sana!!!
 
Mimi ni muajiliwa pia nimejiajili ili kukuza kipato nina biashara ambazo zinajiendesha lkn kwa sasa biashara mauzo yameshuka kwa wastani wa 70% lkn tra wamepandisha makadirio yao ya ukusaji wa kodi kwa 80%, kwahiyo mambo hayajakaa sawa, lkn kazini pia mshahara umestuck toka 2015 haujapanda na gharama za maisha zimepanda maradufu mfano tuu unga umeongezeka kwa asilimia kubwa sana na gharama zingine za maisha.
 
Daaah umenena maisha yamekuwa mwiba sana,Yamekuwa magumu sana lakini kuna mjinga fulani anakupinga na kujifanya yeye hayajui haya pumbavu sana!!!
Naamini ukimwona unaweza ukakuta yupo tuu kijiweni anasikilizia deiwaka, huku msosi ukiwa tayari anakuja kuitwa
 
Mimi ni mfanyabiashara wa siku nyingi tu,nina mwaka na nusu hivi mambo yamebadilika sana wateja hakuna!! Miaka ya nyuma nilikuwa nauza sana kwa siku milioni moja na nusu,milioni 2, hadi tatu siku pakichanganya sana nina duka la vifaa vya ujenzi lakini siku hizi nakomea laki,laki na nusu,elfu 60, 20, hali imekuwa ngumu sana na bahati mbaya sio kwangu tu hata kwa majirani zangu ndugu zangu walio mbali au wenye biashara tofauti na yangu ni vilio tu hali imekuwa sio hali na kama ikiendelea hivi matokeo ni kuna kufunga biashara hapo mbeleni
 
Mkuu mm nimeshafunga biashara yng moja na nimeelekeza nguvu ktk biashara hii ambayo ipo karibu na mm maana mtu anakwambia ameuza elfu 7 huwez amin, wakati before mauzo yalikuwa laki 9 minimum laki 3
 
Back
Top Bottom