Sijui kwanini namchukia mke wangu

Sijui kwanini namchukia mke wangu

Mimba inaharibu muonekano wa mtu; mtu anakuwa anatembea kama greda n.k, kutokana na mabadiliko ya muonekano anayoyapata mkeo, yanakufanya umkinai. Ila, jaribu kumnunulia aina fulani ya mavazi wanavaaga wajawazito yanaishia kwenye magoti, ajipendezeshe kwa kwenda saluni n.k pia mpatie salio anunue lotion zile nzuri nzuri, muda wote awe ananukia; hapo lazima stimu zitarudi.

Yaan hata sijamaliza kusoma nimefika hapo kwa greda nimecheka mbaka wife kabaki kaduwaa
 
Mimba inaharibu muonekano wa mtu; mtu anakuwa anatembea kama greda n.k, kutokana na mabadiliko ya muonekano anayoyapata mkeo, yanakufanya umkinai. Ila, jaribu kumnunulia aina fulani ya mavazi wanavaaga wajawazito yanaishia kwenye magoti, ajipendezeshe kwa kwenda saluni n.k pia mpatie salio anunue lotion zile nzuri nzuri, muda wote awe ananukia; hapo lazima stimu zitarudi.

Daah mkuu umepigilia nchi 6
We ni nomaa
 
Kuna besti yangu alihamia kwao kwa muda had mkewe akajifunguahali ikaisha baada ya kupata mtoto basi
 
Hii hali hujitokeza kwenye ndoa, imewahi kujitokeza kwangu pia, niliishinda kwa kuwa na mawazo chanya kwa mke wangu, kila likinijia wazo mbaya, nalishinda kwa kutafuta chochote kizuri kwake.
 
Mke siyo mpenzi.
Mke ni taasisi mwenza wa kujenga familia.
Mke ndio Polisi wako, hakimu, mshauri wako wako na jirani yako namba moja.

Ukimchukulia mke kama mpenzi ni rahisi kumwacha na kutafuta mke mwingine.

Muweke mke katika nafasi yake ya mtawala wa nyumbani kwako.
Hiyo ndiyo thamani ya mke.
 
Ulifanya vyema sana mkuu
 
Hapana mkuu simchukulii kama mpenz nampenda san mkewangu ila shida ni hiyo hali ilijitokeza kwangu ndo tatizo
 
hahaha kumekucha, labda kajazwa Singida huyo, who knows ?
 
Habari wana JF, natumaini wote wazima, niende kwenye mada moja kwa moja.

Kiukweli nipo na mke wangu nampenda sana mke wangu na tunaishi vizuri tu. Mwezi huu umeanza nashukuru Mungu mke wangu ni mjamzito, na nilimpeleka hospital akapima kweli ni mjamzito wote tukafurahi kwa hilo maisha yanaendelea.

Lakini sielewi nimepatwa na nini, yaani kila siku zinavyozidi kwenda najikuta nimepatwa na hali ya kumchukia mke wangu. Sielew hii hali inatokana na nini, wakati yeye mke wangu ndiyo upendo umezidi hatari, ananipenda sana. Nashangaa sana wakati yeye ndiyo mjamzito, yaani hata nikiwa kazini siku hizi amekuwa muda wowote anapiga simu, yaani nikiona tu simu yake hali yangu inabadilika.

Siku hizi hata kurudi nyumbani najikuta nachelewa kidogo ili nikute kashapumzika, basi nikifika nilale tu tutaonana asubuhi. Na kashaanza kugundua hali yangu hii lakini anabaki akijiuliza kwanini? kiukweli mke nampenda lakini hii hali imekuja tu ghafla baada ya ujauzito wa mke daah.

Wakuu embu niambieni hii imekaaje kitaalamu zaidi na inauhusiano wowote na mimba ya mke wangu? Karibuni wataalamu labda mnaweza nishauri nifanye kitu au labda ni hali tu ya muda itaisha au ni vipi?

Mungu awabariki.
Huyo ni mtoto wa kiume anakuja. Mwanamke akibeba mtoto wakiume chuki kali uanza baina ya mume na mke lakini akijifungua huisha.vumilia tu itaisha
 
Changamoto za mimba zimehamia kwako yaani kiufupi zile mishe mishe zote za mimba, kuchukia/kukasirika Bila sababu, kujisikia kichefu chefu, kula udongo, kuchagua vyakula, usishangae unatamani kuvaa tishet na brouz za mkeo zenye majasho, yakianza kujitokeza wala usiwaze Ndio hivyo, utakapoanza kumtuma mkeo akuletee vitumbua Kwa mama mwajuma usiku ujue ndio hivyo mkuu
 
Huyo ni mtoto wa kiume anakuja. Mwanamke akibeba mtoto wakiume chuki kali uanza baina ya mume na mke lakini akijifungua huisha.vumilia tu itaisha
Hiyo Roho ya chuki nilishaikataa, Kuna sababu gani za kitaalamu kwamba Mke ambaye nimeweka mbegu kwake anichukie mwenye mbegu??? Wangu alinipenda mpaka kutambi kilitoka Kwa beby boy wa kwanza
 
Back
Top Bottom