Sijui kwanini namchukia mke wangu

Sijui kwanini namchukia mke wangu

Mkuu beba majukumu unaenda kuwa Baba, mimba haiji kama chafya, jiweke busy kumuandalia kijacho, muheshimu huyo aliyekubebea mimba, wahi kurudi nyumbani, usisahau kurudi na kimfuko cha vijizawadi hasa matunda. Zoea hali ya mkeo sababu ni suala la muda tu, akifanikiwa kuzaa salama atanawili kama awali na mambo yartakaa sawa, huyo ibilisi anakunyemelea
 
Habari wana JF, natumaini wote wazima, niende kwenye mada moja kwa moja.

Kiukweli nipo na mke wangu nampenda sana mke wangu na tunaishi vizuri tu. Mwezi huu umeanza nashukuru Mungu mke wangu ni mjamzito, na nilimpeleka hospital akapima kweli ni mjamzito wote tukafurahi kwa hilo maisha yanaendelea.

Lakini sielewi nimepatwa na nini, yaani kila siku zinavyozidi kwenda najikuta nimepatwa na hali ya kumchukia mke wangu. Sielew hii hali inatokana na nini, wakati yeye mke wangu ndiyo upendo umezidi hatari, ananipenda sana. Nashangaa sana wakati yeye ndiyo mjamzito, yaani hata nikiwa kazini siku hizi amekuwa muda wowote anapiga simu, yaani nikiona tu simu yake hali yangu inabadilika.

Siku hizi hata kurudi nyumbani najikuta nachelewa kidogo ili nikute kashapumzika, basi nikifika nilale tu tutaonana asubuhi. Na kashaanza kugundua hali yangu hii lakini anabaki akijiuliza kwanini? kiukweli mke nampenda lakini hii hali imekuja tu ghafla baada ya ujauzito wa mke daah.

Wakuu embu niambieni hii imekaaje kitaalamu zaidi na inauhusiano wowote na mimba ya mke wangu? Karibuni wataalamu labda mnaweza nishauri nifanye kitu au labda ni hali tu ya muda itaisha au ni vipi?

Mungu awabariki.
Mkeo hana chura? knows
 
Amina mkuu shukrani sana nimekuelewa nduguyangu
 
Mimba inaharibu muonekano wa mtu; mtu anakuwa anatembea kama greda n.k, kutokana na mabadiliko ya muonekano anayoyapata mkeo, yanakufanya umkinai. Ila, jaribu kumnunulia aina fulani ya mavazi wanavaaga wajawazito yanaishia kwenye magoti, ajipendezeshe kwa kwenda saluni n.k pia mpatie salio anunue lotion zile nzuri nzuri, muda wote awe ananukia; hapo lazima stimu zitarudi.
 
Habari wana JF, natumaini wote wazima, niende kwenye mada moja kwa moja.

Kiukweli nipo na mke wangu nampenda sana mke wangu na tunaishi vizuri tu. Mwezi huu umeanza nashukuru Mungu mke wangu ni mjamzito, na nilimpeleka hospital akapima kweli ni mjamzito wote tukafurahi kwa hilo maisha yanaendelea.

Lakini sielewi nimepatwa na nini, yaani kila siku zinavyozidi kwenda najikuta nimepatwa na hali ya kumchukia mke wangu. Sielew hii hali inatokana na nini, wakati yeye mke wangu ndiyo upendo umezidi hatari, ananipenda sana. Nashangaa sana wakati yeye ndiyo mjamzito, yaani hata nikiwa kazini siku hizi amekuwa muda wowote anapiga simu, yaani nikiona tu simu yake hali yangu inabadilika.

Siku hizi hata kurudi nyumbani najikuta nachelewa kidogo ili nikute kashapumzika, basi nikifika nilale tu tutaonana asubuhi. Na kashaanza kugundua hali yangu hii lakini anabaki akijiuliza kwanini? kiukweli mke nampenda lakini hii hali imekuja tu ghafla baada ya ujauzito wa mke daah.

Wakuu embu niambieni hii imekaaje kitaalamu zaidi na inauhusiano wowote na mimba ya mke wangu? Karibuni wataalamu labda mnaweza nishauri nifanye kitu au labda ni hali tu ya muda itaisha au ni vipi?

Mungu awabariki.
Huyo mkeo kabeba ujauzito na huyo mtoto jinsia yake ni ME,tafuta wataalamu wataalumuke
 
Ungekua muislamu kuna sura ningekwambia upende kuisoma ila ndo ivo tena
Mambo ya kiimani zaidi

Sioni ubaya mkuu kwani dini zote mbili nazi mudu vizur
 
Back
Top Bottom