Sijui kwanini namchukia mke wangu

Sijui kwanini namchukia mke wangu

Habari wana JF, natumaini wote wazima, niende kwenye mada moja kwa moja.

Kiukweli nipo na mke wangu nampenda sana mke wangu na tunaishi vizuri tu. Mwezi huu umeanza nashukuru Mungu mke wangu ni mjamzito, na nilimpeleka hospital akapima kweli ni mjamzito wote tukafurahi kwa hilo maisha yanaendelea.

Lakini sielewi nimepatwa na nini, yaani kila siku zinavyozidi kwenda najikuta nimepatwa na hali ya kumchukia mke wangu. Sielew hii hali inatokana na nini, wakati yeye mke wangu ndiyo upendo umezidi hatari, ananipenda sana. Nashangaa sana wakati yeye ndiyo mjamzito, yaani hata nikiwa kazini siku hizi amekuwa muda wowote anapiga simu, yaani nikiona tu simu yake hali yangu inabadilika.

Siku hizi hata kurudi nyumbani najikuta nachelewa kidogo ili nikute kashapumzika, basi nikifika nilale tu tutaonana asubuhi. Na kashaanza kugundua hali yangu hii lakini anabaki akijiuliza kwanini? kiukweli mke nampenda lakini hii hali imekuja tu ghafla baada ya ujauzito wa mke daah.

Wakuu embu niambieni hii imekaaje kitaalamu zaidi na inauhusiano wowote na mimba ya mke wangu? Karibuni wataalamu labda mnaweza nishauri nifanye kitu au labda ni hali tu ya muda itaisha au ni vipi?

Mungu awabariki.
Mpeleke kwao au kwa wazazi wako kwa kisingizio cha kwamba akapumzike huko sababu ya hali yake ya mimba akae karibu na mama then akishajifungua utamfuata utakuwa ushammiss sana
 
Una matatizo weyeh sio bure kabisa
 
Huyo ni mtoto wa kiume anakuja. Mwanamke akibeba mtoto wakiume chuki kali uanza baina ya mume na mke lakini akijifungua huisha.vumilia tu itaisha

Duuh ikawe kher mkuu
 
Changamoto za mimba zimehamia kwako yaani kiufupi zile mishe mishe zote za mimba, kuchukia/kukasirika Bila sababu, kujisikia kichefu chefu, kula udongo, kuchagua vyakula, usishangae unatamani kuvaa tishet na brouz za mkeo zenye majasho, yakianza kujitokeza wala usiwaze Ndio hivyo, utakapoanza kumtuma mkeo akuletee vitumbua Kwa mama mwajuma usiku ujue ndio hivyo mkuu

mkuu seriously
 
Hiyo Roho ya chuki nilishaikataa, Kuna sababu gani za kitaalamu kwamba Mke ambaye nimeweka mbegu kwake anichukie mwenye mbegu??? Wangu alinipenda mpaka kutambi kilitoka Kwa beby boy wa kwanza

Duuh hongera sana
 
Mpeleke kwao au kwa wazazi wako kwa kisingizio cha kwamba akapumzike huko sababu ya hali yake ya mimba akae karibu na mama then akishajifungua utamfuata utakuwa ushammiss sana

Kweli mkuu lakini mkewangu namjua hawez kukaa mbali na mimi yaan kwakwe ni ngumu sana
 
Mmh sjui lakini mi sijaona mapungufu yoyote kwake mkuu
Kuna wanaume wengine pale wake zao wanapokuwa wajawazito basi wao ndiyo hujisikia kutapika na dalili nyingine za mimba. Mwanamke akishajifungua inapotea
 
Back
Top Bottom