Hapana mkuu kwenye ukweli inabidi usemwe tu siwezi kutetea kila wanachosema wanaume eti kwa vile na mimi ni mwanaume kama wanaume wameongea ukweli nitatetea ila kama ni uongo nitapinga vile vile hata wanawake kama wameongea ukweli nitatetea ila kama ni uongo nitapinga ila all in all nilichogundua humu mitandaoni wanaoongoza kutupa lawama kwa jinsia nyingine ni wanaume
Hii inafanya wanawake ndo waonekane wabaya kuliko sisi wakati uhalisia tunaona humu mitaani kuwa sisi wanaume ndo pasua vichwa wenyewe na sisi tuna matatizo yetu lakini sishangai nature ya mwanaume ni kutupa lawama kwa mwanamke kwenye kila kitu ilianzia kwa Adam alipomtupia lawama Evah kwa Mungu