Sijui kama siku hizi zipo hizi

Sijui kama siku hizi zipo hizi

Kutahiriwa kwa babu kienyeji kwa wembe au kisu kidogo kikali hakuna cha ganzi wala nini!
 
Kuvaa chilimeni siku za siku kuu.(Hii sizani kama viajana wa sasa wanaijua)
 
SIJUI KAMA SIKU HIZI ZIPO HIZI

1. Kupakwa GV kwenye kidonda
2. Kung'olewa jino kwa uzi
3. Ubwabwa kupikwa j2 tu
4. Kidonda kuwekwa unga wa 'rangi mbili'
5. Kupamba kadi sebuleni
6. Ukumbi wa sherehe kupambwa kwa toilet paper
7. Kunyolewa na mkasi
8. Kufunga pesa kwenye leso au pindo la kanga
9. Kwenda kuangalia sinema za Ukimwi na Lishe sokoni
10. Ku rewind kanda kwa peni
11. Ndala kuchemshwa ili zisiishe
12. Kucheza umeshikilia kaptula sababu mpira umekatika
13. Kuchonga penseli na meno
14. Kukata ndala, ati ni kifutio

15. Kunyolewa msalaba shuleni kisa nywele ndefu
16.Kwenda shuleni na tofali na kidumu cha maji

Wewe unakumbuka nini...?

mzee hizo red zilihusika sanakwa upande wangu.
  • kulilia nguo za sikukuu
  • kutoroka shule kwenda kwenye maembe
  • kudefine what is history kila morning speech,nk.
  • kusoma kitabu kimoja cha Mr Daudi watu zaid ya 10
  • kamali ya chelewa+wizi wa mifagio
 
Ukiwa unaenda shue miguu michafu unajiosha kwa umande (unapita kwenye nyasi zenye maji maji yale ya asubuhi).
 
Kuendesha magari yaliyotengenezwa kwa maboksi huku ukiunguruma kama injini pamoja na kupiga lesi wewe mwenyewe.
 
Na hii ya kulala na nguo mpya au viatu vipya mnaikumbuka wanajamii?
 
kunya bila kutawaza alafu mwisho wa siku kaptula zote zinakua na ukoko wa kinyeeeeeesi katkat
 
Kudandia magari, kukaa road msimu wa mvua ili kusubiri gari ikwame msukume mpate pesa, watu wazima kutembea road wamening'iniza rundo la funguo kwenye luksi, kuogelea kwenye vidimbwi, kukopa kacholi xul kwa ticha, kucheki tv dirishani kwa watu coz mtaa mzima tv adimu, vibiriti vyenye picha za mastelingi wa kihindi, kufuga samaki aka gapi,black,zebra. Kukata ndala matairi ya magari, kubeba vibegi vya spoti, kunywa uji wa mchele au maharage msibani, kupanda chaimaharage, dah siezi maliza yote.
 
Mmetisha wana jf ila bado kubeba madaftari mengi darasa la saba ili uonekane msomi!
 
Dah nimeheka sana jf noma
Kuweka shati la shule Jv ya vidonda kwa kuwa huna hela ya kununulia blue
Kutemea mate embe bichi ili mwenzio asikuombe
Kuvaa saa za discolight halafu ikipiga mziki mnacheza darasani.
 
Back
Top Bottom