Sijui kama siku hizi zipo hizi

Dah nimeheka sana jf noma
Kuweka shati la shule Jv ya vidonda kwa kuwa huna hela ya kununulia blue
Kutemea mate embe bichi ili mwenzio asikuombe
Kuvaa saa za discolight halafu ikipiga mziki mnacheza darasani.

Hahahahahaaahahahaaaa!!!! Yaan hapa cna mbavu! Nmecheka mpk basi. JF N noma
 
kodray soap, mshindi soap, tanbond, 7 up ya fidodido, vimto, tv za mbao zisizo na remote, misanya bingi.
 
Nakumbuka tulikuwa tunafukiza vifuu na majani ya mkibosho ndani kuua mbu
yaani tunavikoka vitoe moshi jamani tumetoka mbali
 
Wanawake wa kitanga kuloweka nguo za mwanaume ili asichomoke
Kupanga foleni kwa ajili ya kununua sukari, sembe n.k
 
Duh! Yakuandika barua za mapenzi na kuchora moyo huku katikati una bonge la mkuki nimemkumbuka mshkaji wangu mmoja anaitwa Kizito alimuandikia msichana wake halafu mwalimu akainasa kwenye daftari la huyo msichana! Hahahahaha kengele iligongwa watu wote wakakusanyika mstarini (assembly) mshakaji akaambiwa aisome mbele ya wanafunzi.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
-kumiliki vidonda kama vi5 hivi kwa wiki
-Kusingizia unaumwa siku za usingizi mzuri ili usiende skuli
-kupiga picha huku umepakata radio aina ya phillips(sauti safi sauti kubwa)
-Kupiga picha kwa kamera za filim
-Kuchonga kabati kubwa la tv lenye kufuli na kuliweka sebuleni
-kupaka mafuta ya rays na shant
-kuitikia salam'' ayeya''''dole tupu''
-Barua za mapenzi zenye picha za mikuki inatoboa mioyo

Charger, usinikumbushe hayo mafuta lol, yalikua yanachafua nguo sana hasa mashati ya shule, maana yalikua na rangi ya orange, mmh tumetoka mbali
 
-kuvaa raba mtoni kuliashiria baba yako katoka g'ambo
wengine ni chacha na telemka tubonge
 
Back
Top Bottom