TANZANNIA
JF-Expert Member
- Sep 29, 2015
- 1,047
- 384
ni simulizi ya kusikitisha ililotokea miaka ya mwishoni mwa themanini enzi hizo majumba ya sinema kama avalon,empire,empress,drive in na mengineyo yakisurvive,wakati huo video eidha hazijaingia au zilikuwa chache.kuna jamaa alikuwa akitoka kuangalia move ya kihindi kwenye ukumbi mmojawapo ilikuwa ni mida ya saa sita na za usiku,alipofika mitaa ya uswahilini akasikia sauti ya mwanamke ikiita kuomba msaada.hisia za ubinadamu zikamwingia hivyo akaamua kufuatilia sauti inakotokea ili kutoa msaada.alipokaribia akaona vijana kama wanne hivi wakimbaka mdada,walipoona mtu anakuja wakamwachia na kukimbia,wakati akiwa kwenye harakati za kutoa msaada na wakati huo yule mdada akiwa amekata kauli ghafla wakatokea askari wa doria ambao nao walisikia sauti ile na kumkuta yule jamaa.bila kuhitaji maelezo wakamkamata kwa kosa la ubakaji na bahati mbaya zaidi yule mdada alifariki wakati anapelekwa hospitali,hivyo jamaa akahukumiwa kifungo cha maisha.na ndio maana najiuliza sijui kama bado yuko hai
funzo...si wote walioko jela wana makosa
funzo...si wote walioko jela wana makosa