Sijui hili unalijua kama unataka ndoa

QEEN ADEMU1

Senior Member
Dec 24, 2019
134
324
Hakuna mwanaume aliye single ambaye kila siku akitoka nyumbani kwake anajisemea ngoja nitafute mke kama vile anavyotafuta funguo, simu au fedha aliyopoteza. Haipo hiyo.
.
Mwanaume siku zote anataka awe na mwanamke Katika uchumba na katika safari hiyo ya Mahusiano wazo la kukuoa wewe au Mwingine humjia kutokana na namna alivyo-expirience mahusiano hayo.
.
Na pale mwanaume anapokuchagua wewe, huwa ni wewe tu anayekuhitaji. Wala mwanamke hutatumia nguvu nyingi kuyafanya mahusiano hayo yanyooke. Sasa baadhi ya wanawake wamejipa hadi kazi ya ushushushu wa kutafuta ni nani anatoka na mwanaume wake, na wanapobaini unakuta wanamchimba hadi mkwara huyo wanaembaini. Hiyo haisaidii kama mwanaume mwenyewe hana jitihada ya kusimamia mahusiano hayo.
.
Ndio maana mahusiano mengi yaliyosimama ni yale ambayo Mwanaume ameamua kuyasimamia kidete kuhakikisha Mwanamke wake anayo furaha.
.
Wanawake wengi labda kwa kunogewa na mahusiano wamekuwa wakijiachia mno, kuwa-post mabae zao kwenye Mitandao ya kijamii na wengine kufikia hatua ya kuwazalia kabisa wakiamini kuwa hao ndio tayari Wanaume zao wa ndoa. Lakini baadae kinachokujaga kuwatokea anajua Mungu mwenyewe.
.
Dada zetu wajifunze kuwa na uvumilivu, unapokuwa na mwanaume kwenye mahusiano usijione kama ndio umeshafika, ukahamisha na akili zako zote bila kufikiria mustakabali wa maisha yako. Jifunze kuwa na kifua cha kuficha mambo mpaka pale utakapoona kuna uelekeo chanya wa mahusiano hayo.
.
Unavyoingia katika Mahusiano, beba na akili zako, usiziache nyuma. Ni rahisi mno kufahamu u-serious wa mtu katika mahusiano endapo utashirikisha akili yako.
.
Usijichukulie majukumu ya kuwa Mke wakati bado hata hujaolewa. Maisha hayaendi hivyo. Na unavyoona mahala ulipo hapaeleweki, ondoka mapema kabla mambo hayajakuharibikia.
.
Nimeshawahi kusema kwamba, MALENGO YA MAHUSIANO hayahusiani na kupiga selfie pamoja, kukumbatiana, kushikana mikono, kupelekana maeneo ya starehe na kuvaa nguo zinazofanana.
.
Hizo mbwembwe waachieni vijana wa Vyuoni. MALENGO YA MAHUSIANO ni kuwa muaminifu na mkweli, kuwa committed, kushirikiana pamoja ili kuweza kufikia ndoto za ku-win ECONOMIC FREEDOM, kujijenga kuwa bora zaidi na kusaidiana kwa pamoja kuwa karibu na MUNGU.......

Sent using i phone x
 
Speed yako ya kuwafunda watoto wa kike ni kali sana, na inasemekana kwamba watu ambao mnatoa ushauri murua kama huu, ni watu ambao mlishakumbana na mengi sana kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Anyway ujumbe mzuri kwa warembo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yule mbunge Joseph Haule kaoa baby mama wake?

Na Sugu je nae kaoa baby mama wa mtoto wake wa pili?

Kwa kifupi mapenzi na mahusiano hayana formula. Usikopi wala kuiga mahusiano ya wengine.

We fanya yako na huu ushauri baki nao acha wadada wafanye watakavyo.
 
Back
Top Bottom