Sijawahi kutumia perfume, bodyspray wala lotion. Je, kuna kitu nakosa?

haszu

JF-Expert Member
Oct 10, 2017
837
1,550
Sina lotion, sina perfume, sina body spray, naogea sabuni ya jamaa, miguuni na mikononi tu ndo napaka baby Care, niko mjini . kuna kitu nakosa?
 
Hakuna unachokosa Hata kidogo !
Sanasana unapata faida kupitia uhakika wa afya yako Kwa kuepukana na Yale ambayo yangeweza sababishwa na matumizi ya hizo kemikali !
When otherthings remain constant !
Maana yaweza kuwa una epukana na hili lakini Kumbe upande mwingine ukawa unaenda kinyume na vile inavyofaa!
Mfano Kama u mlevi , Malaya , au unakula vyakula bila mpangilio bila kujali kanuni Za Lishe bora bado utakuwa under risk!
Au pengine siyo mwadilifu mfano ukiwa barabarani huzingatii sheria za usalama barabarani una mzoea ya kuendesha Gari Kwa mwendo kasi bado utakuwa at high risk!
N.k
 
Isipokuwa ujitahidi kuoga vizuri, sugua kwapa hizo na povu ya sabuni Mara mbili tatu n.k ili kusudi usinuke majasho na kuwakwaza Watu !
 
Sina lotion, sina perfume, sina body spray, naogea sabuni ya jamaa, miguuni na mikononi tu ndo napaka baby Care, niko mjini . kuna kitu nakosa?
Kuna sehemu niliona wakizungumzia lotion zinachangia kuleta mvi kwa kasi ya hatari
 
Kuna sehemu niliona wakizungumzia lotion zinachangia kuleta mvi kwa kasi ya hatari
Sio kweli mvi ni za kurithi...babu yangu ana 90+ ila ana mvi na nywele nyeusi. Kuna ambao wakiwa 20 tayari mvi kichwani.
Mzee wangu anapaka 'Vaseline na NIVEA for men' ila mvi zinahesabika.
 
Napenda Issey Miyake perfume,
Romance, NIVEA for men,
Olive oil ile ya kijani kwa nywele,
Protex nyeupe kuoga.
Maisha yanasonga vizuri kabisa.
Mtoa mada tumia lotion na perfume hazina matatizo.
 
Back
Top Bottom