Sijawahi kupanda ndege....Nielimisheni

Sijawahi kupanda ndege....Nielimisheni

Joined
Sep 9, 2013
Posts
52
Reaction score
28
Wadau..mi kusema cha ukweli sijawahi kupanda ndege toka nimezaliwa. Nataman sana siku moja kuipanda. Umri wangu ni miaka 35. Naomba tuelimishane....siku ya kwanza inakuagaje?..Nikifika pale airpot JINIA...naelekea wapi na wapi mpaka naingia ndani ya ndege?..na humo kwenye ndege nasikia kuna mikanda unajifunga....je unaweza kutembea humo ndani wakati ndege ikiwa juu?..natamani kujua kiujumla...habari za ndege. Sagari za ndani na za yale madege makubwa ya nje.
 
Namna bora ya kujua jambo kwa ufasaha ni pale utakapo husika nalo moja kwa moja (first hand experience).

Fastjet wana nauli za hadi sh 43,000 kwa safari ya Mwanza au Kilimanjaro....unaweza kwenda Mwanza asbuhi kisha urudi jioni.

Sijui uko wapi lakini kama uko Dar, Mwanza au Moshi mmi ntakuchangia nauli ya kwenda wewe ulipie kurudi.... Kama uko nje miji nilotaja itamaanisha uongeze gharama ya kukufikisha miji husika.

Vinginevyo ni usafiri wa kawaida tu....ingawa first timers huwa wanajulikana (wakijipiga picha, kwenda msalani hata kama hawako pressed...lol)
 
Aisee first nilihisi km inadondoka...nilikua naogopa mwanzo mwisho....hasa vindege vidogo uwiiiiiiii....vinayumba yumba tu angani..
 
Unabeba unga hata kama ni wa mahindi ili upitishwe VIP.

Halafu kama umezoea kupanda basi dk 5 kabla ya kuondoka ni vyema kwenye ndege ukafika dk 3 kabla (unachezea kwenye chaki kama okocha), lazma rubani atasimamisha ndege na utapata favour ya kupitia mlango wa dereva.

Pia huwa kuna seat za konda, ukiona imejaa unaongea na wale wadada wanakuuzia seat kwa bei nafuu, au unakaa kwenye bonet la injini pembeni ya rubani, lazma wakufanyie 20,000/= to KIA
 
Wadau..mi kusema cha ukweli sijawahi kupanda ndege toka nimezaliwa. Nataman sana siku moja kuipanda. Umri wangu ni miaka 35. Naomba tuelimishane....siku ya kwanza inakuagaje?..Nikifika pale airpot JINIA...naelekea wapi na wapi mpaka naingia ndani ya ndege?..na humo kwenye ndege nasikia kuna mikanda unajifunga....je unaweza kutembea humo ndani wakati ndege ikiwa juu?..natamani kujua kiujumla...habari za ndege. Sagari za ndani na za yale madege makubwa ya nje.

..., mkuu' "godoro-la-comfy" usiwe na wasi... Siku ukiwa na safari ya kutumia usafiri wa ndege..., jitahi kila unakotakiwa fika mapema kwa muda uliopangwa "waoene wahudu wa eneo husika" waeleze kuwa hujawahi tumia usafiri wa ndege, waulize utaratibu watakusaidia"
 
Back
Top Bottom