Sijawahi kuona mtu muongo kama Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Taarifa ya GAG juu ya ufisadi wa uniform za polisi ulifanyika lini? Ni wazi ni kabla ya Lugola kuwa waziri wa Mambo ya Ndani. Taarifa ya CAG inasema malipo ya uniform za polisi yalifanywa mwaka 2015, na tunaelewa mwaka wa mwisho wa ukaguzi wa CAG ni 2016.

Sasa leo Kangi Lugola, miaka zaidi ya mitatu baada ya GAC kufanya ukaguzi na kukuta fedha za uniform zimetumika lakini uniform hakuna, anasema CAG aende kwenye maghala ya Polisi akaonyweshe uniform

Sasa jiulize - uniform zilizonunuliwa miaka mitatu iliyopita zinafanya nini ghalani au kwenye container hadi leo? Si zitakuwa zimevunda na kuoza? Lugola angekuwa na hata chembe ya busara, angesema uniform zilifika baada ya ukaguzi wa CAG. Lakini sasa kaamua kujifanya kikaragosi (puppet) wa Ndugai. Nimemtoa kabisa heshima kwa hili.

Kwa kweli sijawahi kuona mtu mwongo kama Kangi Lugola! Halafu eti ni waziri anaesimamia jeshi la polisi. Kama kweli Magufuli yuko serious na nchi hii Lugola aondolewe mara moja. Kumbuka juzi tu hapa Magufuli mwenyewe alitamka kwamba kuna ufisadi wa sare za polisi, kuwa hela zimelipwa sare hazipo na alitoa maagizo kwa Lugola, IGP, PS Meja Generali Rwegasira na makamishna wa polisi. Lugola si tu ni muongo, bali ni mwepesi kuongea na mzito kukumbuka, na kamtukana CAG na Magufuli kwa pamoja.
 
Pimeni wenyewe. Uniform zilizonunuliwa mwaka 2015 Lugola anasema zipo stoo. Na CAG aliwaomba hati ya kupokea mzigo hawakutoa. Kama huo sio wendawazimu basi ni ulevi wa kisiasa kwa Lugola

1081978
 
Uwaziri ni dhamana ambayo shurti iambatane na kukubaliana na ukweli toka vyombo rasmi vya serikali.
Lugola, aliyekuwa afisa wa cheo cha chini katika jeshi la Polisi, ameonyesha udhaifu mkubwa kiuongozi, kimaadili na hata kiakili binafsi.
Kimsingi huweze kupinga personally audit querry iliyotayarishwa kitaalam kwa maneno ya kihuni.
 
Kweli kabisa Mkuu. Katika collective responsibility ya serikali Lugola amefanya dhambi kubwa sana. Anasahau yeye na CAG wote wako serikalini na ni viongozi wakuu wa serikali. Ni sawa na waziri wa ulinzi aseme jambo, halafu waziri wa mambo ya ndani aseme waziri wa ulinzi mwongo sana.

Kwa tamko hili Lugola anapaswa kujiuzuru au kufukuzwa kazi.
 
Pimeni wenyewe. Uniform zilizonunuliwa mwaka 2015 Lugola anasema zipo stoo. Na CAG aliwaomba hati ya kupokea mzigo hawakutoa. Kama huo sio wendawazimu basi ni ulevi wa kisiasa kwa Lugola

View attachment 1081978
But Kangi will get away with this as if nothing has happened! Hivi Mawaziri wote walioguswa na hoja za ukaguzi za CAG ndivyo wanavyotakiwa kujibu kwa style hiyo kama alivyofanya Waziri wa Mambo ya Ndani?
 
Kangi hakuwa waziri 2015 hivyo basi wala hukua na haja ya kudanganya, angeweza tu kuelezea uchunguzi umefikia wapi, sasa anaonekana mzandiki na mwongo mkubwa.
Kwa heshima na taadhima,the Hon Minister amuombe radhi HE The President halafu aachie ngazi.Hali kadhalika yule aliyetumia Flip chart kuwafundisha wa TZ mahesabu ya KG II pia amuombe radhi Chairman na asepe zake.
Tuweni serious watanzania wenzangu,kwa tabia hizo tunampa kiongozi wetu wakati mgumu saana wa kuongoza nchi.
 
binafsi kwa mtazamo wangu lugola kapewa nafasi kubwa sana kuliko uwezo wake. nimesikiliza majibu yake dhidi ya sakata La lissu kupigwa risasi ni Zaidi ya kituko...
Sakata la lisu yuko sahihi 95%.Nakubaliana na wewe kuwa Nafasi ni kubwa kuliko Lugola.
 
Kweli kabisa Mkuu. Katika collective responsibility ya serikali Lugola amefanya dhambi kubwa sana. Anasahau yeye na CAG wote wako serikalini na ni viongozi wakuu wa serikali. Ni sawa na waziri wa ulinzi aseme jambo, halafu waziri wa mambo ya ndani aseme waziri wa ulinzi mwongo sana.

Kwa tamko hili Lugola anapaswa kujiuzuru au kufukuzwa kazi.
Hiyo collective responsibility haiapply kwa CAG Kusema bunge ni Dhaifu?
 
Back
Top Bottom