Sijawahi kuona Jiji la hovyo kama Arusha

kikaniki

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
502
938
Ni mongoni mwa majiji sita ya nchi hii. Inajulikana pia kama Geneva ya Afrika na pia kitovu cha utalii Tanzania.

Lakini ukweli ni kuwa, ni miongoni mwa miji mibovu na ya hovyo hapa Tanzania. Nimeishi Arusha mwaka wa saba sasa. Tanzania hii nimeizunguka takribani mikoa yote isipokuwa Ruvuma, Mtwara na Lindi.

Tofauti na inavyosifiwa, huu mkoa wa Arusha (na hapa naongelea Arusha Jiji) ni pabovu mno. Miundombinu yake inatia kichefuchefu. Ukitoka barabara kuu, ndani ya mita chache tu hapatamaniki. Mathalani, ukiwa katika barabara ya kuelekea Babati, labda maeneo ya Ngarenaro ni kinyaa kitupu. Nenda Matejoo ni uozo mtu. Nenda Mbauda au Morombo. Kipindi cha masika madimbwi ya maji kila eneo. Nenda uswahilini, Muriet hadi intel, ndio usiseme. Barabara mbovu hata kwa pikipiki hapafikiki. Nenda Ngusero, mamaaaa!! Hapafai. Hata Njiro wanapokaa mataita, barabara zake ni za hovyo sana.

Mbunge yupo. Madiwani wapo. Wenyeviti wa mitaa wapo. TARURA ipo. Shida ni nini?

Arusha ni pazuri ukiwa katikati ya mji. Kwingine, hapana
 
Nimevuta kiti nimekaa huku namsikiliza Rapcha…

Na hili jua la siku hizi, huko dar hamjaungua ngozi za kichwa? 😅
Dar kama Amsterdam.

1000123474.png
 
Back
Top Bottom