Sijawahi kuona Jiji la hovyo kama Arusha

Sijawahi kuona Jiji la hovyo kama Arusha

Ni mongoni mwa majiji sita ya nchi hii. Inajulikana pia kama Geneva ya Afrika na pia kitovu cha utalii Tanzania.

Lakini ukweli ni kuwa, ni miongoni mwa miji mibovu na ya hovyo hapa Tanzania. Nimeishi Arusha mwaka wa saba sasa. Tanzania hii nimeizunguka takribani mikoa yote isipokuwa Ruvuma, Mtwara na Lindi.

Tofauti na inavyosifiwa, huu mkoa wa Arusha (na hapa naongelea Arusha Jiji) ni pabovu mno. Miundombinu yake inatia kichefuchefu. Ukitoka barabara kuu, ndani ya mita chache tu hapatamaniki. Mathalani, ukiwa katika barabara ya kuelekea Babati, labda maeneo ya Ngarenaro ni kinyaa kitupu. Nenda Matejoo ni uozo mtu. Nenda Mbauda au Morombo. Kipindi cha masika madimbwi ya maji kila eneo. Nenda uswahilini, Muriet hadi intel, ndio usiseme. Barabara mbovu hata kwa pikipiki hapafikiki. Nenda Ngusero, mamaaaa!! Hapafai. Hata Njiro wanapokaa mataita, barabara zake ni za hovyo sana.

Mbunge yupo. Madiwani wapo. Wenyeviti wa mitaa wapo. TARURA ipo. Shida ni nini?

Arusha ni pazuri ukiwa katikati ya mji. Kwingine, hapana
Jamni naomba mnipatie sifa za Tatu mzuka pale Arusha wananini wale vijana wa pale🤣🤣🤣ili ntapofika niwe makini zaidi
 
😁😁😁
Feels like.. Actual 24 😂
Kaka njoo upunge upepo..
IMG_1698.png
 
The only shit I Hate in Arusha 🥹
Lakini unaweza wadhibiti.. ikifika saa 12 usipite chocho zao, macho yako yawe kwenye utajiri wako.
Weeeeeeh sema kwer Sasa apa utajiri wangu ni 1200 zangu 🤣🤣🤣
 
The only shit I Hate in Arusha 🥹
Lakini unaweza wadhibiti.. ikifika saa 12 usipite chocho zao, macho yako yawe kwenye utajiri wako.
Sasa ndo maisha gani haya mnaishi kama digidigi kuwa ikifika saa 12 hutakiwi kutembea baadh ya mitaa
 
Sasa ndo maisha gani haya mnaishi kama digidigi kuwa ikifika saa 12 hutakiwi kutembea baadh ya mitaa
Huko ushwahilini huko.

Unavyoongea as if huko Dar uwa hamuibiwi?? Dar huko si mnaporwa na jua linawaka?
 
Back
Top Bottom