Sijawahi kumpenda mke wangu kiasi hiki

Sijawahi kumpenda mke wangu kiasi hiki

hongera sana.!!!
Unanipa hofu kwamba kashikwa uchungu jumapili kajifungua leo jumatano???? huyo mtoto kalia baada ya kuzaliwa? uchungu hautakiwi kuzidi masaa 12 kama unataka mtoto anayeweza kuwa engineer au daktari siku moja
 
Chabo, pole na hongera sana, Mungu wetu ni mwema sana, mama na mtoto watakuwa na afya njema sana very soon

Wewe ndio umegoma kabisa kumpenda zaidi Mama watoto pamoja na kusababishia uchungu zaidi ya mara saba kamna kwamba hiyo haitoshi saiv upo busy unahangaika na MwaJ!!

rudisha moyo wako nyuma kama kijana wako Chabo hapa!
 
Last edited by a moderator:
huenda jamaa alikosa msaada wa pembeni.. sasa hapa nafikiri anataka tumchangie sijui!!

twampongeza lakin. Utu uzima dawa


lol....
Hamna kijana amesema ana lita kama 40 za usingizi hivi..

Sure, anastahili pongezi sana, kubwa zaidi kwa kukiri anampenda zaidi my wife wake!
 
Hongera kwa kupata mtoto, nadhani mmekwisha jiandaa na mambo ya kumlea mtoto katika njia iliyo njema ili akuwe katika afya ya roho na mwili.

Hongereni nyote, mpe pole mkeo, mwambie huku wana jF, wanakupa hongera sana kwa kuitika mapenzi ya Mungu.
 
Hongera sana kwa mtoto na uhai wa mama! ILA INAONESHA HAMSOMI BIBLIA kwani baada ya kula tunda lile la katikati MUNGU aliwapa adhabu Adam (atakula kwa jasho) na Hawa (atazaa kwa Uchungu)... kwahiyo hiyo ni utimimifu wa maneno ya MUNGU...

Mi naona yamekuwa vice versa maana sasa wanawake wanakula kwa jasho na wanazaa kwa uchungu.Mungu awaongezee nguvu
 
Halow wandugu,
ilikuwa jumapili usiku aliposhikwa na uchungu mida ya saa nane.niliona ni jinsi gani uchungu unavyowauma wanawake,nikampeleka hospital fulani ya masista mbezi alikaa mpaka j3 usiku saa8 ikashindikana kujifungua ndipo nikampeleka mwananyamala huku nashuhudia anavyohangaika.hatimaye amejifungua leo saa 12 asb kwa operation.japokuwa nimevunjika moyo lakini namshukuru mungu muweza yote.

I hope utampa break ya mwaka, kabla ya kuanza match!
 
Hongereni sana na pole nyingi sana kwa mama, we just wish her a very quick recovery ... Aaaah haaa haaa, kama nakuona vile Chabo, chabo zikakutokea puani ....
 
Nami nilitaka kumuuliza hilo anasema "amevunjika moyo" ni tatizo??
 
Hongereni kwa mtoto ndo sasa uzidishe penzi sio tena huruma ya ng'ombe mara unasahau unaanza kurukaruka mama analea
 
Kaanza uchungu jumapili saa nane usiku na kajifungua jumanne saa 12asbh na mtoto alilia sana.
hongera sana.!!!
Unanipa hofu kwamba kashikwa uchungu jumapili kajifungua leo jumatano???? huyo mtoto kalia baada ya kuzaliwa? uchungu hautakiwi kuzidi masaa 12 kama unataka mtoto anayeweza kuwa engineer au daktari siku moja
 
Sababu ya upasuaji ndugu yangu,si unajua tena ni mwanamke mchakarikaji,so anaona uchungu kwamba kazi mingi kwake basi.
Nami nilitaka kumuuliza hilo anasema "amevunjika moyo" ni tatizo??
 
Hongera sanaa Na pole mama, mungu amjalie afya njema pamoja na mtoto.

Hilo la operation nalo huwa linaumiza sana especially kama hukutegemea, but with time Mungu atamponya na mtalichukulia positive.

Mshukuru Mungu mtoto mzima na mama. Wapo wengi wanaingia theatre na wanatoka bila mtoto. Mshukuru Mungu kwa wema wake.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hongera sana. Mungu akuzidishie upendo na heshima kwa kina mama wote. Nini kimekuvunja moyo?
 
Sababu ya upasuaji ndugu yangu,si unajua tena ni mwanamke mchakarikaji,so anaona uchungu kwamba kazi mingi kwake basi.

chabo mkuu wangu kwanza hongera sana wewe pamoja na mkeo. mungu atamfanyia wepesi mkeo atapona haraka. na mtt twamtakia afya njema sana.
Pili unavunyika moyo na nini na nguvu za kutamka hayo unazitoa wapi badala ya kumtukuza mungu sasa kwani nani alikuambia operesheni ni mwisho wa kuchakarika wewe? hizo labda za zamani ndugu, huyo muache auguze kidonda tena baada ya muda mfupi tu utashangaa amechangamka baada ya miaka miwili basi yuko barabarani wasiwasi wa nini wewe sasa hivi unatakiwa umshukuru mungu na kumbuka kila kitu yeye ndo mpangaji.Operesheni kwa nyakati hizi wala sio ishu kabisa kuwa na amani mfurahie mtoto vinginevyo kwa maneno hayo utampa stress mkeo atajiona ndio baaas tena hataweza chochote kitu ambacho si kweli. Once again hongera sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom