Sijawahi kukutana na Afisa Usalama wa Taifa

Sijawahi kukutana na Afisa Usalama wa Taifa

Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2010
Posts
4,845
Reaction score
4,776
Habari wanabodi,

Kwa muda mrefu nimekuwa nikisikia habari kuhusu idara ya Usalama wa Taifa, nilivutiwa kuwafahamu hawa watu, nimesoma vitabu vingi na makala nyingi kuhusiana na watu hawa ila sijawahi kukutana nao katika maisha yangu.


Namaanisha sijawahi kukutana nao ana kwa ana, nasikia wapo kila sehemu nimetembea sehemu nyingi ila sijawahi hata kuhisi kuwa fulani ni Afisa usalama wa taifa.

Kuna wachache nilisikia wakitambulishwa kuwa ni watumishi wa TISS ila ni wale wenye nyadhifa kubwa mf. Mh Diwani Athumani (inasemekana hata kamanda Siro alikuwa hajui kuwa huyu bwana ni TISS) hapo nikachanganyikiwa zaidi hii inakuwaje?

Hawa watu wapo kweli au ni nafasi za kusadikika ambazo zinafanya watu waishi kwa nidhamu na kuheshimiana sababu hatujui nani ni nani?

Kama kweli wapo kwenye nchi hii basi watakuwa na mafunzo ya hali ya juu na maadili maana nadhani kwa jinsi nilivyotafuta taarifa zao ningekuwa nimemfahamu hata mmoja tu bila kuambiwa na mtu, wewe unamfahamu?

Nani alikwambia? (Achana na wale tunaowaona wakimlinda Mh Rais, nataka kujua hawa tunaoishi nao)
 
Nitukane au niandike vibaya mkuu,nitakufukunyua adi chumbani ili unifahamu japo Mie tu.
Habari wanabodi,
Kwa muda mrefu nimekuwa nikisikia habari kuhusu idara ya Usalama wa Taifa, nilivutiwa kuwafahamu hawa watu, nimesoma vitabu vingi na makala nyingi kuhusiana na watu hawa ila sijawahi kukutana nao katika maisha yangu.
Namaanisha sijawahi kukutana nao ana kwa ana, nasikia wapo kila sehemu nimetembea sehemu nyingi ila sijawahi hata kuhisi kuwa fulani ni Afisa usalama wa taifa.... Kuna wachache nilisikia wakitambulishwa kuwa ni watumishi wa TISS ila ni wale wenye nyadhifa kubwa mf. Mh Diwani Athumani (inasemekana hata kamanda Siro alikuwa hajui kuwa huyu bwana ni TISS) hapo nikachanganyikiwa zaidi hii inakuwaje?

Hawa watu wapo kweli au ni nafasi za kusadikika ambazo zinafanya watu waishi kwa nidhamu na kuheshimiana sababu hatujui nani ni nani?
Kama kweli wapo kwenye nchi hii basi watakuwa na mafunzo ya hali ya juu na maadili maana nadhani kwa jinsi nilivyotafuta taarifa zao ningekuwa nimemfahamu hata mmoja tu bila kuambiwa na mtu, wewe unamfahamu? nani alikwambia? (Achana na wale tunaowaona wakimlinda Mh Rais, nataka kujua hawa tunaoishi nao)
 
[emoji2222][emoji2222][emoji2222][emoji2222][emoji2222][emoji2222][emoji2222][emoji2222][emoji2222][emoji2222][emoji2222][emoji2222]
 
Katika Watanzania 10,:-
2 ni kwa ajira.
3 ni kwa asili yao.
3 ni kwa nafasi za kazi zao.
2 ni raia wa kawaida.
Ingawa inatofautiana ni wakati gani,wapi na mahala gani.
mfano
Usiku....ni 5:2:2:1
Jioni/asubuhi....ni 1:2:2:5
Mitaani kwenye miji mikubwa ....4:1:3:2
Makazini.....ni 4:2:2:2
Usalama wa kila mtu ndio usalama wa nchi.
Pamoja na shida zetu tulizonazo sisi kama Taifa,lakini haimaanishi kiusalama tuko nyuma.
Kwa asili kila Mtanzania ni mlinzi wa Amani wa Mtanzania/mtu mwingine,ingawa kuna special task for special elites kutumika ipasavyo kuliko wengine ili tuendelee kuwa na usalama endelevu @24/7/365...$#
 
Nimesoma nao,
Nimeishi nao (majirani),
Nimefanya nao kazi,
Wengine shemeji zetu,
Wengine washkaji tupo nao kitaa.
Jana nilikua nae mmoja tunapiga nae story zaidi ya masaa matatu.
Wengine walinifundisha chuo.

Wapo wengi wamejazana kila kona, tatizo wewe ndio huwajui.
 
Namaanisha sijawahi kukutana nao ana kwa ana, nasikia wapo kila sehemu nimetembea sehemu nyingi ila sijawahi hata kuhisi kuwa fulani ni Afisa usalama wa taifa.

Mkashifu raisi utakutana nao. Tena hata wale wa kikosi cha wasiojulikana watakuja kukutembelea mfahamiane
 
Back
Top Bottom