Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,474
- 39,987
Ndiyo haya nilikuwa nayazungumzia...Nimemuona huyu CEO kwenye taarifa ya habari akilalamika kwamba eti abiria wanaotaka kutumia usafiri wa ndege wamekuwa wengi hivyo kuathiri na kusababisha kusitishwa na kucheleweshewa ratiba ya Safari za ndege.
Aliyemwelewa naomba anisaidie manake idadi ya siti kwenye ndege inajulikana wakishakata wanaotosheleza si chombo kinaondoka any how ndege Zina ratiba zake hata ikiwa haijaja inatakiwa iondoke kufuatana na ratiba.
Eti analalamika abiria wamekuwa wengi hivyo kusababisha kusitishwa kwa Safari.
Ana mpango wa kuongeza bodi hayo madege au ndio kazi imemshinda anaongea mapumba na mashudu yasiyoeleweka.
Biashara ya ndege ni ngumu tumeingizwa choo Cha kike na jiwe.
Itabidi jiwe azitapike hizo hela zetu alizotumia kienyeji kununulia ndege.
Aiingii akiline eti abiria kuongezeka kusababishe kusitisha Safari.
Kama Kuna anayeelewa vizuri / au alimwelewa yule Komba anieleweshe alikuwa anamaanisha Nini kwenye ongezeko la abiria na kusitishwa kwa Safari za ndege