Tatizo la ATCL siyo abiria kuwa wengi ni mambo yafuatayo.
1. Safari zime pangwa nyingi muda wa karibu hivyo kuleta uhaba wa marubani kurusha ndege katika muda stahiki. Rubani hutakiwa kurusha ndege angalao masaa nane kwa siku na kwenda pumzika Hivyo hawezi pangiwa kurusha ndege tena hadi masaa ya kupumzika yatimie. Kutokana na hali hiyo inabidi kuchelewesha ndege kuondoka ili kusubiri muda ambao marubani watakuwa tayari kuruka.
2. Kitengo cha kupanga ratiba za ndege, marubani na wahudumu (cabin attendants), OPS kichunguzwe kwanini haya yanatokea. Kitengo hiki cha crew scheduling lazima kiwe madhubuti kuondoa kero hii na wawe na mtazamo wa muda wakupata marubani kwa wiki zisizo pungua mbili ili kama kuna wakati kutatokea marubani hawaja kuwa tayati basi safari iahirishwe na abiria wapewe taarifa mapema.
3. Ndani ya shirika kuna kamati ya wawakilishi toka idara mbali mbali hukutana na kupitia mienendo ya safari zilizo pita nakuona changamoto zilizo jitokeza zina chukuliwa hatua na kuzitafutia ufumbuzi. Kamati hii ya OTP, yaani On Time Performance, ni muhimu sana na ikutane si chini ya mara tatu au nne kwa wiki. Ikiwezekana kila siku. Changamoto zinazo jadiliwa ni sababu mbali mbali zilizo chelewesha ndege kuruka katika muda uliyo pangwa. Changamoto hizo ni pamoja na kuchelewa marubani na wahudumu, matatizo ya kiufundi, kuchelewa kupakia chakula, shida za abiria zilizo jitokeza kwenye ndege na kadhalika.
4. CEO awe mkweli kwa yale yanayojiri kwani shirika hili limekuwa na matatizo mengi kutokana na uwongozi kushindwa kuliendesha. Hii ni kujiona kwamba wao ndiyo shirika huku chini ni amri tu. Wataalamu washiriki mikutano ya management ili kusaidia kutatua kero kitaalamu. Muwakilishi mmoja toka fani mbali mbali ndani ya shirika ahudhurie vikao.
5. Upendeleo na makundi vimeshamiri ndani ya ATCL. Ipo haja kukomesha hili kwani utakuta wale wenye uwelewa na ujuzi wakibaguliwa hujirudisha nyuma matokeo ni wanao pendelewa ku fail na kampuni kuyumba mwisho kuanguka. Vyeo kupewa watu wanaojiona na kuwa karibu na viongozi iwe nje au ndani ya shirika. Hili nalo huchangia utendaji mbovu.
6. CEO asitafute mchawi. Yeye na management yake inabidi wabadilike wasizoee vyeo walivyo navyo waone ni dhamana to.