Sijajibizana na mtu miaka 10, nikaona nipate wa kujibizana nao

Wamamba

Senior Member
Jan 5, 2024
125
226
Sometimes mtu una miss tu ugomvi na kutukanana na majibizano ya hapa na pale na hauna watu wa kugombana nao

Huku kwetu kila mtu na habari zake yaani kila mtu yupo ndani ya yard yake hauwezi kwenda kwa nyumba ya yeyote kwenda kupiga story au kuangalia mpira ufupi hauna nafasi ya kujibizana na mtu sana sana umletee mtu ujehuri.

Sasa najikuta nimemis tu ilee mizozo ya uswahilini mitusi na mikimbizano ya hapa na pale mda ambao nakuwa nipo off yaani mda ambao napumzika kazi.

Uswahilini raha sanaa, utakuta kuna vigoma siku ya wiki endi, mara kuna vipubu vya hapa na pare, vigoma vya urugway, mara watu wamegombana yaani tafrani ilimradi mtu uboreke tu au umboe mwenzako

Sasa nimemisi yalee maisha ya kitaa ya malumbano kila mda nikaona ile raha siipati popote sio Instagram, Facebook wala wapi? Nikaona ni hapa JF na nimeridhika na mitusi na majibizano ya hapa na pale uzuri wenyewe wanakwambia JF ukitaka chochote utakipata, elimu mpaka burudani

Ila nilichogundua watu wa JF, wanajifanya tu na wengi wao hawana kitu

Wengi wao wanastress
Yaani wanaakili mpaka zimewazidia na inajulikana ukiwa na akili kupitiliza unaweza ukawa mwendawazimu yaani mtu ana ropokwa tu na ndivyo vitu nilivyovimis mpaka nikavifata

Wengi wanajifanya wana uelewa mkubwa na ni uongo
Yaani unakuta mtu anavyoosha maelezo kwenye uzi fulani lakini unakuta ataanzisha uzi anaongea ujinga mtupu yaani unajiuliza huyu ule uzi aliemwaga pwenti amekopi kwenye kitabu gani? yaani watu kama wana mashetani , ila wenye uelewa wapo sijakataa maana unakuta unasoma vyuzi mpaka unajiona umeshafanikiwa

Wengi wanajifanya wana uwezo na hawana kitu
Kwenye hili nafurah watu wa jf wanabebwa na watu wachache wa jf wenye uwezo wa kweli na waliofanikiwa, naamini wenye uwezo wapo na wanasaidia Kweli, mtu akija na akaanza kulalamika hana kitu unakuta watu wanamtumia vicent na anakuja kushukuru, ongereni kwenu ila wengi hawana kitu na wanajifanya wana maisha mazuri na naamini wapo wengi wanaishi ng’ambo

Wanangu wakula tunda kwa masikhara sijawataja, hamjui, kumbukeni ukimwi upo, ndomu muhimu

Narefresh nikimaliza narudi mwenye ID yangu yenyewe hiyo nasoma vyuzi za big thinker na stories change tu hapa habari mchanganyiko mnazingua tu bora mtu uende kwenye habari za mapenzi tu
 
Back
Top Bottom