Sijahesabiwa Bado na Deadline Inakaribia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sijahesabiwa Bado na Deadline Inakaribia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ng'wanangwa, Aug 31, 2012.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  hivi kwa nini huyu JK ni failure kwa kila kitu? hivi inakuwaje mimi mpaka dakika hii sijahesabiwa? au Chadema hatuhesabiwi?
   
 2. S

  Starn JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 400
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwani JK ndio anahesabu watu?
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  acha maswali ya kitoto.
   
 4. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ng'wanangwa Hujui sense nayo ilikuwa in geresha nafikiri ilikuwa ni sehemu ya kuhalalishia malipo makubwa kwani kila sehemu wameshastukiwa
   
 5. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Wewe si SIMBA SC fan? Hata mimi, nadhan sensa yetu bado. LOL!
   
 6. m

  mamajack JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  na tahimin imeshatolewaa tayari!tumefanikiwa kwa 80% hivyo ambao bado hautwahitajii sana,maana makadilio yetu ilikuwa ni 60%.tumevuka lengo!!!!
   
 7. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #7
  Aug 31, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mimi sina chama lakini sijahesabiwa. Jana walipita kwa jirani yangu walipomalizana nae wakamuuliza vipi huyu jirani yako yupo? jirani akawajibu yupo. baadae wakaanza kuulizana vipi tumuhesabu na huyo? mmoja wao akasema ahhh tumechoka bwana, na akaongezea, mtaa huu waliobaki tuwaache kesho twende mtaa mwingine siku zinaisha. Kwa hiyo mimi na familia yangu hatutahesabiwa. kwa hiyo ni wengi tu ambao hawatahesabiwa na kwa ujumla takwimu zitakazopatikana hazitakuwa sahihi.
   
 8. HASSAN SHEN

  HASSAN SHEN JF-Expert Member

  #8
  Aug 31, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 428
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Acha utoto kwani we umechukua hatua gani kuhakikisha unahesabiwa.
   
 9. S

  Ssanyu New Member

  #9
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 31, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana, but we are in the same boat. Mimi na familia yangu pia hatujahesabiwa. Jana nilienda kwa mwenyekiti wa mtaa kutoa taarifa sikumkuta ila niliacha ujumbe but mpaka ninaondoka nyumbani leo saa mbili asubuhi hakuna aliyekuja. Kinachonishangaza ni kuwa baadhi ya majirani wamehesabiwa, sielewi kama sensa ya mwaka huu italeta real picture ya idadi ya watanzania ukizingatia kuna maeneo tunasikia makarani waliishiwa vitendea kazi toka jumamatatu tarehe 27/08/12
   
 10. KATATANAMA

  KATATANAMA Member

  #10
  Aug 31, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama hujahesabiwa nenda ofisi za serikali ya mtaa utahesabiwa huko na huo ndiyo utaratibu uliotolewa kwa wale ambao hawatafikiwa.
   
 11. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #11
  Aug 31, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mimi nimehesabiwa nasubiri hayo maendeleo wanayoyasema kwenye kauli mbiu zao eti sensa kwa maendeleo ya taifa
   
 12. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #12
  Aug 31, 2012
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  TULIAMBIWA TUWASUBIRI WATAKUJA NA MJUMBE NA WATAKUWA NA VITAMBULISHO
  SASA SISI TUKAFANYE NN SERIKALI ZA MITAA??? DOUBLE STANDARDS
  BADO NAWASUBIRI :rant:
   
 13. yatima

  yatima JF-Expert Member

  #13
  Aug 31, 2012
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 354
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0


  Hapo kwenye red - yaani utaratibu rasmi ni kufuatwa kwenye KAYA yako na kuhesabiwa or tuseme mahali ulipolala tarehe 25 usku kuamkia 26.

  Watu wamepewa mafunzo juu ya kuhesabu watu, wamelipwa, wamepewa vitambulisho ...........halafu washindwe kufanya zoezi kamili.

  MIMI NITOKE KWANGU - KWA JASHO LANGU..............KWA MGUU AU USAFIRI WANGU.............. KWA MUDA WANGU......HADI SERIKALI ZA MITAA ............NIMTAFUTE MWENYEKITI NA KAMA KATOKA NIMSUBIRI ILI TU

  NIHESABIWE!!!!!!!!!!!!!!!!!!! VERY FUNNY INDEED ............... ??????????????????????????? :eek2::eek2:
   
 14. Nokla

  Nokla JF-Expert Member

  #14
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 12, 2012
  Messages: 2,121
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 160
  mi najiuliza yule mama mkurugenzi wa sensa zile asilimia za mafanikio ya sensa sijui zaidi ya 90 kazitoa wapi? Kaazi kweli kweli.
   
 15. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #15
  Aug 31, 2012
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Acheni kulalamika kama wale majamaa, chukueni hatua. Imekwishatolewa tamko kwamba kama hujahesabiwa nenda kwa mwenyekiti wako wa serikali ya mtaa. Sasa ninyi mmechukua hatua gani kabla hamjaja humu JF?
   
 16. Clarity

  Clarity JF-Expert Member

  #16
  Aug 31, 2012
  Joined: Jul 6, 2010
  Messages: 811
  Likes Received: 329
  Trophy Points: 80
  Mie bado nawasubiri kwangu wasipokuja basi siwezi kupoteza muda kumtafuta huyo cjui ndio mkiti kwani hawa makarani wa sensa wanalipwa posho kubwa tu.
  Jirani yangu wameshapita!!!!!ajabu
   
 17. Nokla

  Nokla JF-Expert Member

  #17
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 12, 2012
  Messages: 2,121
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 160
  mkuu sio sahihi kabisa kwasababu kama ni hivyo basi kusingekuwa na haja ya kutumia mapesa yote yale ya kuwalipa makarani na isitoshe nilishapoteza muda kuwasubiri, bado niendelee kupoteza muda tena kuwatafuta? Liwalo na Liwe!
   
 18. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #18
  Aug 31, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Utasubiri sana bornagain.....kiukweli watu wengi sana hawajahesabiwa mpaka wakati huu!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #19
  Sep 1, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Hahaha ni kweli ndugu yangu ntasubiri sana maana all I see here is just politics basi
   
 20. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #20
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Sielewi mtazamo wako ni upi hasa sambamba na haki yako ya msingi: kuna mantiki gani makarani kulipwa pesa za walipa kodi kwa ajiri ya kupita nyumba kwa nyumba kuhesabu watu alafu kwangu wasipite tena kwa makusudi kama si uzembe alafu leo uniambie niende kwa M/kiti wa serikali za mitaa kupanga foleni!!!!!.

  Ambao hatujaesabiwa ni wengi mno, mi naishi kwenye apartment yenye jumla ya familia 12 cha ajabu hakuna hata mmoja aliyehesabiwa.

  Katika pitapita zangu nilikutana na makarani wa sensa mitaani nikawaomba wanihesabu wakagoma wakadai kuhesabiwa kwangu ni mpaka niwe mtaani kwangu ninakoishi, nilishindwa kuwaelewa kwani mi nilifikiri kila mtu anahesabiwa popote pale anapokua amepatikana kwa muda muhafaka kumbe siyo na wao wana maana nyingine.

  Mimi niko Dar es salaam sikuhesabiwa japo nilitamani Je yule wa Namtumbo, Vyadigwa, Lupembe na Butakya?????.
   
Loading...