Sijaelewa baadhi ya vipengele katika hii salary slip

Status
Not open for further replies.

kipapi

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
1,056
1,374
Habari zenu Wanajamii,

Naomba msaada wenu kwa mwenye kujua/kutambua baadhi ya vipengele katika salary slip.
Vipengele hivyo ni;

1. Total Company Contributions

2. Total Deductions

Haswa hii Total Company Contribution sijaielewa kabisa, yaani inatoka wapi/kwa nani? inaenda wapi/kwanani?

Maana mtu akiacha kazi ofisini kwetu malipo anayopewa ni yale ya PPF/NSSF tu hakuna mengine, labda kama hukwenda likizo ndio utapewa pesa ya likizo.

Naomba kuwasilisha.

1476170896110.jpg
 
Habari. Total Company Contribution ni pesa ambayo kampuni inachangia kwenye mapato yako. nadhani hapo ni 10%
Anayokuchangia PPF na SDL kutoka kwenye mshahara wako.

Total Deduction ni sum ya PAYE na PPF unayokatwa kwenye mshahara wako.

Kama nimekosea nadhani kuna wennye uelewa zaidi watadadavua
 
sehemu zote ukiacha kazi kwa mwajiri wako upewi chochote zaidi ya mafao yako tu nssd au ppf ambao nao siku hizi hawayatoiiiii
 
Hakuna kitu kibaya kama dhihaka, maana hakuna aijuae kesho yake
Upo sahihi..kwanini wabongo hatupendi kuambiwa ukweli..Daimondo anenunua nyumba sauzi kwa zaidi ya mil 300...sasa nambie kwa huo mshahara anapaswa afanye kazi miaka mingapi ili aweze kuipata hyo ela?
 
Mr. MTUI
Alichouliza na unachokishadadia wewe ni vitu tofauti sana, we unamjua jamaa ana nini na nini nje ya mshahara wake? Usimdharau usiyemjua ukajifanya unamjua..... Kwani wewe huo mshahara wako wa kujenga nyumba kama ya diamond huko sauzi, unafikiri ndo umefunika humu ndani? Watu wana yao lakini hawana dharau hizo... Sasa kama ni ndogo aache kazi afanye ya kwako ya kuvaa vimodo na kujipodoa? Una kasoro ndg yangu, mwenzio kaona hiyo biashara yako hiyo haimfai ni bora kalaki mbili zake anaheshimika kama mwanaume.
 
Upo sahihi..kwanini wabongo hatupendi kuambiwa ukweli..Daimondo anenunua nyumba sauzi kwa zaidi ya mil 300...sasa nambie kwa huo mshahara anapaswa afanye kazi miaka mingapi ili aweze kuipata hyo ela?
Kwani mleta mada alizungumzia kwamba anataka kununua nyumba bondeni?
Hapo umeona ametaja jina la Diamond?
Ebu usipende kuonyesha ujinga wako kwenye hadhara, na hii ni dalili ya utoto na kuto kukomaa kiakili.
Mleta uzi ameuliza kitu kingine kabisaaaa.... alafu wewe unakuja kumlazimisha na kile unacho kiwaza wewe...
 
Upo sahihi..kwanini wabongo hatupendi kuambiwa ukweli..Daimondo anenunua nyumba sauzi kwa zaidi ya mil 300...sasa nambie kwa huo mshahara anapaswa afanye kazi miaka mingapi ili aweze kuipata hyo ela?

Mmmh hapana unakosea. Kila mtu anabei yake ya maisha. Hiyo anayopata anaridhika na inamtosha na huenda anaweza kuwa na mipangilio mizuri japo ya kawaida na maisha ya furaha.
Kila mtu anajipangia maisha kutokana na kipato chake kilivyo. Kuna watu wanapata mshahara wa Zaidi ya milioni moja ila ukienda kwake unaweza lia kwa kumuonea huruma na ugumu wa maisha yake na wakti huo kuna mtu anapata mshahara wa laki 4 na ukifika kwake kila kitu kimepangiliwa na anafuraha kabisa. Sababu za huo utofauti ni nyingi, kubwa ni mwenye kupata mshahara mkubwa anajigamba ngoja nile maisha tuu si itaingia tena hivyo kutaka makuu wakati mwenye mshahara mdogo anakuwa makini na apatacho na kukipangilia matumizi haswa maana hajui kesho itakuwaje.

Tusijudge mshahara wake tumsaidie maelezo ya hayo makato tu:
Total Company contributions: Ni jumla ya michango uliyochangiwa na kampuni yako hapo ni PPF
Total Deduction: Ni jumla ya makato kutoka mshahara wako kuchangia mfuko wako wa jamiii (PPF ambapo mwajili yeye kakuchangia yake - Total Company contributions) na PAYE( Pay As You Earn = hii ni kodi ya serikali kwa kile ulichopata katika mshahara wako)
 
Hili jibu lina mantiki gani na swali alilouliza mtoa mada? Dhihaka nyingine hata maana hazina. Wewe nyumba yako kama ya Diamond iko wapi?
Mkuu iwas just trying to think loudly..sory kama nme muoffend mtu
 
Hiyo nahisi ni kiwango cha NSSF/PPF kilichowakilishwa na kampuni yako tangu uajiriwe.
 
Kwani mleta mada alizungumzia kwamba anataka kununua nyumba bondeni?
Hapo umeona ametaja jina la Diamond?
Ebu usipende kuonyesha ujinga wako kwenye hadhara, na hii ni dalili ya utoto na kuto kukomaa kiakili.
Mleta uzi ameuliza kitu kingine kabisaaaa.... alafu wewe unakuja kumlazimisha na kile unacho kiwaza wewe...
Iwas just trying to think loudly sory if nmemuoffend mtu...
 
Hizo story za vijiweni..ni mgodi gani huo ambao unawatu wenye mshahara wa laki moja but wanamiliki masemi
Kwa iyo unadhani wale wanaotumbuliwa wanategemea mishahara kujenga majumba, au ajira yao kujenga majumba na kununua masemi?
 
Hizo story za vijiweni..ni mgodi gani huo ambao unawatu wenye mshahara wa laki moja but wanamiliki masemi

Hahaaa tembea uone, si kila uonacho ndivyo kilivyo. Mfano tuu Mishahara ya wabunge au mawaziri unaijua? Ila malupulupu yao yanafanana na mshahara? Unafikiri wanaendaga kufuata mshahara? Baada ya miaka mitano wakivunja bunge hupewa kiinua mgongo cha kiasi gani? let say Milioni 250++, je mfanya kazi gani anapata hicho kwa miaka mitano? So hata huko migodini nasikiaga wanapata malupulupu, mfano Arusha mji umejengwa na wanaoitwa wanaapollo, inasemekana wanaweza sota muda mrefu bila kitu ni ugali na dagaa tu, mara anapata jiwe la milioni Zaidi ya 500++. So life kila mtu anaformula yake anajua anatokaje
 
Ok..
 
Mkuu iwas just trying to think loudly..sory kama nme muoffend mtu
You haven't thought anything substantial, you are an idiot. Mtoa mada hajauliza habari za nyumba popote iwe mjini, kijijini au SA . Sasa wewe umeitoa wapi issue ya diamond ? Kama ungesema Mimi nimenunua au kujenga....alafu ukalinganisha...japo Bado ungekuwa off topic lakini angalau. Sasa diamond ni nani kwako ? bwana hako au Nani wako? Unadhani diamond ndio wa kwanza kununua nyumba nje ya nchi? (Kama kweli kanunua). Au diamond ndio Tajiri kuliko watu wote tz?
 
Povu la nini mkuu..au ndo timu Kiba?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom