Siitazami ajali ya ndege kama wengi mnavyoitazama, yawezekana kuna makubwa nyuma yake

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Hebu tushirikiane kuwaza mambo kadha wa kadha hapa na ya msingi;

Mara zote kwenye mambo ya msingi nakuwa firm Kabisa utani pembeni hata Kama kuna nyuki wa mama wananikaba Kwa kusema labda sikutakiwa kusema watakuwa wanakosea sana maana nilipumzika kuandika Makala ndefu ndefu nikaishia kuwa naona kama nishaandika kila kitu Kwa wakati sahihi linapotokea ndo nafufua uzi husika wa mada husika !

Swala la ajali hii ya ndege linafikirisha mengi sana nimekuta mtu sehemu anauliza mambo ya msingi Kabisa nikashirikiana naye kuwaza haya

1. Nikiwa nawaamini sana Marubani wa Precision air pengine kuliko wa mashirika mengine, pasi shaka hata chembe najiuliza kwa nini ndege hii imeelekea kwenye uelekeo tofauti wa runway? Katika hili najiuliza Control Tower ilikuwa na ofisa? Na kama ndio alikuwa anafanya kazi gani? Au kwa nini hakutoa vzr/alitoa maelekezo tofauti ya jinsi ya kutua? (Hili linakuja kaa kuwa Rubani yeyote anaweza kutua kiwanja chochote kipya kwa maelekezo kutoka chumba cha waongoza ndege akiwa 5-30miles) juu ya jinsi ya kutua, speed, distance ya kugusia runway, hali ya hewa etc).

Hapa najiuliza sipati majibu na inanipa maswali juu ya chanzo cha ajali hii.

2. Ndege inasema ilikuwa na abiria 43 lakini idadi ya majeruhi 26 na marehemu 19 inafanya maswali mengi. Sitaki kulaumu sana kwa kuwa ndege hii ina uwezo wa kubeba abiria 48 ila TAA ichunguze hii ATC ilitolewaje? Nani walihusika.

3. Ndege imezama, yaan iko sehemu salama kimfumo wa ajali za ndege, tena mita 100+ tu kutoka kiwanja ila uokoaji umechukua masaa zaidi ya manne, RPC anasema watu watulie kila kitu kiko under control, control ipi?...HII NI AIBU KUBWA KWA SERIKALI YETU.

4. Waziri Mkuu ameagiza uwanja ufungwe... Je kuna siri gani hapa nyuma ya pazia? Uwanja una shida gani kama kila kitu kilikuwa sawa? Kama kila kitu kilikuwa sawa ina maana watu wasisafiri tena kwenda Bukoba sababu ya ajali hii? KUNA NINI CHA KUFUNGIA UWANJA?

5. Nimemuangalia Mkurugenzi Mtendaji wa Precision Airways(Patrick Mwanri) akiomba watu tusipotoshe Umma juu ya ajali hii, amebeba uchungu mzito sana akizungumza akiwa analia machozi mbele ya waandishi... It is not normal, hata kama jamaa anaumia kibiashara ila anajua kabisa Bima watamlipa ila swali la chanzo cha ajali hii na matokeo yake yanawagusa sana Precision kuliko sisi wote.

Binafsi siitazami ajali hii kama wengi mnavyoitazama, yawezekana kuna makubwa nyuma yake.

Tuwe sometimes na Uwezo wa kuchunguza yanayoendelea chini ya carpet bila kusubiria kulishwa kila taarifa

Kwako Pascal Mayalla

Britanicca
 
Kati ya wote aliyepuyanga ni Mkuu wa Mkoa na yule Mama sijui Afisa wa Uwanja.

Hii video imeumiza sana Moyo wangu,inakuwaje watu wapo kwenye maji halafu anayesoma taarifa na wenzake pembeni wanacheka kama ni jambo la kawaida.

Wabarikiwe sana Wavuvi na Wananchi wote kwa ushupavu na Moyo wa kila namna katika kuokoa wenzetu 26.

Mtu anatusome majina hovyo hovyo kama kitu cha kawaida.

Yule Mkurugenzi wa PA, hakika kifua chake kimebeba mengi mno.

Wamulikwe wote walioleta utani kwa siku ya jana.Wasichekewe...
 
Nimekusoma naona ni kama vile unataka kuaminisha kwa hisia zako washindani wa Precision wanahusika kwenye hii ajali, jambo ambalo siliafiki, ajali mara nyingi huwa haichagui pakutokea, wala muda.

Masuala mengine kama muda wa uokoaji kuwa mrefu, na kufungia uwanja hapo nakubaliana nawe, naona kama Majaliwa alikurupuka jambo litakalosababishia usumbufu abiria na watumiaji wengine wa uwanja wa ndege wa Bukoba.

Kuhusu machozi ya mtendaji/bosi wa Precision yanaweza kuwa ni hisia za kibinadamu tu, wala sio sababu za kibiashara kama unavyodhani, uhai wa mwanadamu una thamani zaidi ya ushindani wa kibiashara, usiusemee moyo wa mtu.
 
Kuna mtu kafungua Uzi huko anasema matairi yaligoma kufunguka wakati wa kutaka kutua.

Rubani alitoa taarifa control tower kwa ushauri ni ni afanye inaonekana ushirikiano kutika control tower ukawa mdogo.

Inasemekana baada ya kuzunguka angani Kwa nusi saa rubani akaomba ushauri, akaambiwa kutoka control tower kuwa we ipeleke ziwani tutakuja kuwaokoa.

Ukifuatilia hayo maelezo na ukifuatilia ule uzi wa jamaa alietabiri kuwa itatokea ajali ya ndege hivi karibuni. Utagundua kuwa huu ni mpango ulipangwa.
 
Hebu tushirikiane kuwaza mambo kadha wa kadha hapa na ya msingi;

Mara zote kwenye mambo ya msingi nakuwa firm Kabisa utani pembeni hata Kama kuna nyuki wa mama wananikaba Kwa kusema labda sikutakiwa kusema watakuwa wanakosea sana maana nilipumzika kuandika Makala ndefu ndefu nikaishia kuwa naona kama nishaandika kila kitu Kwa wakati sahihi linapotokea ndo nafufua uzi husika wa mada husika !

Swala la ajali hii ya ndege linafikirisha mengi sana nimekuta mtu sehemu anauliza mambo ya msingi Kabisa nikashirikiana naye kuwaza haya

1. Nikiwa nawaamini sana Marubani wa Precision air pengine kuliko wa mashirika mengine, pasi shaka hata chembe najiuliza kwa nini ndege hii imeelekea kwenye uelekeo tofauti wa runway? Katika hili najiuliza Control Tower ilikuwa na ofisa? Na kama ndio alikuwa anafanya kazi gani? Au kwa nini hakutoa vzr/alitoa maelekezo tofauti ya jinsi ya kutua? (Hili linakuja kaa kuwa Rubani yeyote anaweza kutua kiwanja chochote kipya kwa maelekezo kutoka chumba cha waongoza ndege akiwa 5-30miles) juu ya jinsi ya kutua, speed, distance ya kugusia runway, hali ya hewa etc).

Hapa najiuliza sipati majibu na inanipa maswali juu ya chanzo cha ajali hii.

2. Ndege inasema ilikuwa na abiria 43 lakini idadi ya majeruhi 26 na marehemu 19 inafanya maswali mengi. Sitaki kulaumu sana kwa kuwa ndege hii ina uwezo wa kubeba abiria 48 ila TAA ichunguze hii ATC ilitolewaje? Nani walihusika.

3. Ndege imezama, yaan iko sehemu salama kimfumo wa ajali za ndege, tena mita 100+ tu kutoka kiwanja ila uokoaji umechukua masaa zaidi ya manne, RPC anasema watu watulie kila kitu kiko under control, control ipi?...HII NI AIBU KUBWA KWA SERIKALI YETU.

4. Waziri Mkuu ameagiza uwanja ufungwe... Je kuna siri gani hapa nyuma ya pazia? Uwanja una shida gani kama kila kitu kilikuwa sawa? Kama kila kitu kilikuwa sawa ina maana watu wasisafiri tena kwenda Bukoba sababu ya ajali hii? KUNA NINI CHA KUFUNGIA UWANJA?

5. Nimemuangalia Mkurugenzi Mtendaji wa Precision Airways(Patrick Mwanri) akiomba watu tusipotoshe Umma juu ya ajali hii, amebeba uchungu mzito sana akizungumza akiwa analia machozi mbele ya waandishi... It is not normal, hata kama jamaa anaumia kibiashara ila anajua kabisa Bima watamlipa ila swali la chanzo cha ajali hii na matokeo yake yanawagusa sana Precision kuliko sisi wote.

Binafsi siitazami ajali hii kama wengi mnavyoitazama, yawezekana kuna makubwa nyuma yake.

Tuwe sometimes na Uwezo wa kuchunguza yanayoendelea chini ya carpet bila kusubiria kulishwa kila taarifa

Kwako Pascal Mayalla

Britanicca
Kuna taarifa juu ya watu 2 kuzidi ndani ya ndege??

Kuna Bomba unaweza shika ndani ya ndege kama daladala za RANGI tatu mbagala??
 
Kuna mtu kafungua Uzi huko anasema matairi yaligoma kufunguka wakati wa kutaka kutua.

Rubani alitoa taarifa control tower kwa ushauri ni ni afanye inaonekana ushirikiano kutika control tower ukawa mdogo.

Inasemekana baada ya kuzunguka angani Kwa nusi saa rubani akaomba ushauri, akaambiwa kutoka control tower kuwa we ipeleke ziwani tutakuja kuwaokoa.

Ukifuatilia hayo maelezo na ukifuatilia ule uzi wa jamaa alietabiri kuwa itatokea ajali ya ndege hivi karibuni. Utagundua kuwa huu ni mpango ulipangwa.
Huo uzi wa utabiri wa ajari tunaweza kupata link yake mkuu?
 
Kuna mdau alidokeza chanzo ni maofisa wa uwanja hasa wa control tower kutoresponse alichokuwa anasema ruban mana alidai matairi yanagoma kufunguka , maofisa wakamwambia azunguke ziwani asubiri wampe maelekezo , jamaa akazunguka , mwisho akawajuza kuwa mafuta yanaisha wampe jibu chap , wakamwambia aipeleke ziwani , mana ni karbu watu wa rescue watakuja chap ....

Matokeo yake ndo hayo hapo watu wa rescue hawajatokea , ndo mana huyo mkrugenzi alijua ni uzembe wa maofisa wa uwanja wa ndege kutowajibika mpak watu wanakufa ..... sema ikabd alilie moyoni tuu... Alaf huyo jamaa mwingine aliyetabir ndege kuanguka ndo wale wale tuu waliohusika kuyaharbu matairi kishetani , na yeye aulizwe , utabir wa kisenge senge tuuu
 
Kuna mdau alidokeza chanzo ni maofisa wa uwanja hasa wa control tower kutoresponse alichokuwa anasema ruban mana alidai matairi yanagoma kufunguka , maofisa wakamwambia azunguke ziwani asubiri wampe maelekezo , jamaa akazunguka , mwisho akawajuza kuwa mafuta yanaisha wampe jibu chap , wakamwambia aipeleke ziwani , mana ni karbu watu wa rescue watakuja chap .... Matokeo yake ndo hayo hapo watu wa rescue hawajatokea , ndo mana huyo mkrugenzi alijua ni uzembe wa maofisa wa uwanja wa ndege kutowajibika mpak watu wanakufa ..... sema ikabd alilie moyoni tuu... Alaf huyo jamaa mwingine aliyetabir ndege kuanguka ndo wale wale tuu waliohusika kuyaharbu matairi kishetani , na yeye aulizwe , utabir wa kisenge senge tuuu
Mkuu unaweza kupandisha link ya uzi wa utabiri wa ajari hii?
 
Back
Top Bottom