Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,479
- 30,144
Kuliitishwa kikao cha dharula cha Baraza la mawaziri, kuongelea kitu kimoja pekee, ajali ya ndege ya Precision Air, iliyotokea zaidi ya wiki moja iliyopita!
Hata hivyo kilichonishangaza zaidi ni taarifa ya msemaji mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, baada ya kumalizika kwa kikao hicho, ambapo ametuomba watanzania tuwe watulivu, wakati huu ambapo Tume ya kuchunguza ajali hiyo inaendelea na uchunguzi wake!
Nimuulize Bwana Msigwa, hivi intelejinsia yao ndivyo inavyowaambia kuwa watanzania wanategemea kufanya vurugu, kuhusiana na ajali hiyo?🥺
Hivi hii ni mara ya kwanza, Taifa letu linapata ajali?
Mbona Kila mwezi, mabasi yetu yanaua mamia wa abiria huko barabarani, mbona hatujawahi sikia, hata mara moja, kikiitishwa kikao cha dharula cha Baraza la mawaziri, kujadili suala hilo?
Nchi hii kumewahi kutokea ajali nyingi Sana, majini na barabarani, zilizochukua uhai wa watanzania wenzetu kwa maelfu, lakini sijawahi kusikia Baraza la mawaziri likifanya kikao chake kwa njia ya dharula, kama ilivyotokea kwa ajali ya ndege ya Precision Air!
Najiuliza ni sababu zipi zinazowafanya watawala wetu wa CCM "waweseke" kiasi hiki kwa ajili ya ajali hii ya ndege ya Precision Air?
Kumewahi kutokea ajali nyingi tu na Tume mbalimbali zimeundwa na Serikali hii ya CCM, lakini matokeo yake hayajatolewa kwa Umma wa watanzania na badala yake ripoti hizo zimefichwa kwenye "makabati" ya watawala wetu wa CCM.
Kwa kuzitaja chache ya Tume hizo:-
1. Iliundwa Tume ya kuchunguza namna pesa "zilivyochotwa" huko BoT, baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wetu, Hayati Magufuli, lakini hadi leo, taarifa hiyo haikutolewa kwa Umma wa watanzania na badala yake zikafichwa na watawala wetu.
2. Iliundwa pia Tume ya kuchunguza moto uliounguza soko la Kariakoo, lakini baada ya Tume hiyo kukamilisha Kazi yake na kukabidhi ripoti hiyo kwa watawala wetu, hatukusomewa yalibainika nini kwenye Tume hiyo.
3. Iliundwa pia Tume ya kuchunguza Mauaji ya mfanyibiashara wa madini huko Mtwara, Mussa Hamisi, ambapo inadaiwa aliuawa na Polisi na wakampora pesa zake za madini, zaidi ya shilingi milioni 70, hata hivyo matokeo ya Tume hiyo pia, hatukujulishwa watanzania.
Najiuliza hivi ni kwanini watawala wetu wameingia "kiwewe" kwa ajali hii ya ndege ya Precision Air?
Lakini jibu ninalolipata ni kuwa tofauti na Tume zilizopita, ambazo watawala wetu ndiyo waliokuwa wanaunda Tume hizo na baada ya Tume hizo kukamilisha uchunguzi wao, watawala wetu wamekuwa wakituficha, Ili tusijue nini kimebainika na Tume hizo.
Tokea ajali hiyo ya ndege ya Precision Air, iliyotokea zaidi ya wiki moja iliyopita, kumekuwa na shutuma nyingi kutoka kwa Umma wa watanzania, kuwa kulitokea uzembe wa Hali ya juu kwa vikundi vya uokoaji kutotimiza wajibu wao, hadi kusababisha vifo hivyo 19.
Kutokana na safari hii Tume ya uchunguzi kuwa ni huru, ambayo inawahusisha wataalamu waliotengeneza ndege hiyo ya Precision Air, kutoka Ufaransa, ndiko nadhani kumewatia "kiwewe" watawala wetu na hasa baada ya Tume hiyo kusema hadharani kuwa matokeo ya Tume hiyo yatatolewa baada ya wiki 2 tokea ajali hiyo ilipotokea na watawala wetu hawama "ubavu" wa kuizuia Tume hiyo isitoe taarifa yao kwa Umma