MAKA Jr
JF-Expert Member
- Nov 17, 2016
- 267
- 209
Ninachoweza kusema ni "Mungu atusaidie" kwa huruma yake na akipenda vinginevyo tunachezacheza tena bila utaratibu.
Jamii inajua kuvuruga vichwa vya watu haiwezi kuwa na msingi wa jambo lolote lile. Nasema haya kwa sababu wizara ya elimu imekuwa ikichezewa kama vile haina msingi kwenye maendeleo ya nchi.
Leo tunaambiwa tunaenda kwenye 'Uchumi wa Viwanda', neno ambalo naogopa hadi kulisema maana nahisi linaonewa tu. Unawaandaje vijana wa kufanya kazi viwandani kama mfumo mzima wa elimu unawajenga kufanya kazi ofisini? Hapa tunacheza tu.
Leo hii kamuulize Mwanafunzi wa kidato cha NNE alime bustani ya mbogamboga halafu uone mwitikio wake!
Tuna safari ndefu!